TUNAWEKA
MALENGO SAWA NA HATUFANIKIWI SAWA, NINI SABABU YA WATU KUSHINDWA KUYAFIKIA
MALENGO YAO
Duniani
kote kila mwishoni au mwanzoni mwa mwaka watu hupanga Malengo mengi sana, tena
hupanga Malengo mazuri, ukiyaangalia unaona mafanikio makubwa mbele yao. Na
umekuwa ni Utamaduni uliozoweleka sana watu kupanga Malengo kila mwishoni na
mwanzoni mwa mwaka.
Kwa mujibu wa takwimu Bubu inaonyesha kwamba katika kila watu million moja ambao huweka Malengo, nusu yake huwa wanasahau kabisa ifikapo mwezi machi na robo 3 huishia kusingizia changamoto zinazowazunguka na 1/3 yake ndo huyafikia malengo yao.
Kwa mujibu wa takwimu Bubu inaonyesha kwamba katika kila watu million moja ambao huweka Malengo, nusu yake huwa wanasahau kabisa ifikapo mwezi machi na robo 3 huishia kusingizia changamoto zinazowazunguka na 1/3 yake ndo huyafikia malengo yao.
HEBU
TUANGALIE NI SABABU ZIPI ZINAZOCHANGIA HALI HII????
ü
Kukosa
nidhamu ya matumizi ya pesa na muda. Utajiri wa kwanza
duniani ni matumizi mazuri ya muda/wakati, ukitumia muda na pesa vibaya huwezi
kuyafikia malengo yako.
ü
Aaina ya
marafiki ulionao, inayoweza
kukufanya ushindwe kuyafikia
mafanikio yako ni marafiki, hapa nazungumzia marafiki wasiokuwa na tija kwako,
ukiendekeza kuwapa nafasi marafiki kuchezea Malengo yako huwezi kusonga mbele.
Sisemi usiwe na marafiki, uwe na marafiki wenye ushawishi na ndoto zako.
ü
Kukosekana kwa Maarifa na taarifa muhimu kuhusu Malengo yako, siku zote unapoweka Malengo yako, jitahidi kutafuta Maarifa na
taarifa zinazoendena na Malengo yako.
ü
Kukimbilia kila fursa inayojitokeza mbele yako huku ukisahau
Malengo yako. Siyo
fursa zote zinazokuja kwako zaweza kuwa na faida kwako, kinachotakiwa ni wewe
kuzichunguza fursa na kuona katika zinawezekana kwako. Lakini pia fursa mpya
zisikuharibie malengo na ndoto zako.
ü
Changamoto za afya na elimu,
unapoweka Malengo yako huku ukisahau kuitunza afya yako utaishia kuutumia muda
wa kutekeleza mipango yako kutibu afya, unapoweka Malengo yako, pia hakikisha
unajali afya yako. Pi elimu, unapoweka Malengo yako usisahau kujiendeleza
kielimu ili uendane na mabadiliko yanayoikumba duniani kisayansi na
kiteknolojia.
ü
visingizio, ukiwa ni mtu wa kupenda kusingizia
mambo mbalimbali huwezi kufanikiwa katika kuyafikia Malengo yako
KWA MFANO
KWA MFANO
u Sina
elimu
u Rais
kabana
u Wazazi
wangu hawakuniwekea msingi
u Serikali
hainijali
u Ndugu
zangu hawanipendi
u Sina
hela.
ü
Kukosa uthubutu, unaweza kuweka
mipango mizuri sana lakini ukakosa nguvu ya uthubutu yaani nguvu ya kujaribu
kufanya.
ü
Tamaa ya kutaka kufanya kila kitu bila
kuweka vipaumbele katika malengo yako
ü
uvivu, Uoga na kutokujitambua, lazima
ujitambue kuwa wewe ni wa pekee Sana na lazima ujue kama hutafanya wewe hakuna
mwingine wa kufanya.
Ni nzurii hii
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDeleteSafii
ReplyDeleteIt's so accurate,, be blessed
ReplyDeleteIt is Good
ReplyDelete