Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MAENDELEO BINAFSI

ONDOKANA NA UTUMWA HUU

Nikusihii kitu kimoja mpenzi msomaji wa makala hizi za YAPOCODE TANZANIA kwamba maisha ambayo unaishi muda mwingine jua ni kwasababu ya utumwa ambao umeujenga katika fikra zako.Huu utumwa ambao umeujenga katika akili zako ni utumwa ambao umekufunga kufikiri vizuri juu ya maisha yako,ni utumwa ambao umekufanya kujiona huna thamani mpaka mtu flani akufanyie kitu flani ndipo ujione kwamba unathamani katika maisha yako.Mpaka lini utaogopa kufanya unachotaka kukifanya kwasababu mtu flani kafanya kitu kama kacho ambacho unaogopa kukifanya,lini utaacha uwoga wa kuwa mtu mnyenyekevu hata kwenye sehemu ambazo zinahitajjuhudi zako kuwa zaidi ya unyenyekevu sehemu ambazo sio? lini utasema sasa najijenga mwenyewe na niweze kuwa zaidi ya leo nilipo?. Nakusihii usiache utumwa wako wa kifikra kuacha lulu iliyoko ndani yako kupotea,usiache utajiri ambao uko ndani yako kupotea.leo hii anza na jitahidi kufanya kile ambacho unaogopa kukifanya lakini unajua kabisa kwamba ni kitu chema katika maisha ...

KUWA MSHUMAA WENYE MAANA NA FAIDA KWA WENGINE

Zig Ziglar aliwahi kusema kwamba Ukitaka kufanikiwa saidia wengine kufanikiwa na wewe utafanikiwa na mimi nakwambia kwamba Ukitaka kuangaza dunia nzima kuwa mshuma ambao unawasha mishumaa mingine sio kuizima ya wengine. Ukiwa na nafsi ya kutaka mshuma wako tu kuangaza dunia nzima hautafika sehemu yoyote itazima tu na wala hautakuwa na nguvu ya kuangaza mbali.Watu hawatasema kwamba huyu mtu alishawahi kuwasha mshumaa wake hata siku moja. Naomba nikueleweshe kitu kuhusu huu mshumaa, mishumaa nimeivisha taswira ya MAARIFA YAKO, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI ZAKO ambao wanakuzunguka. 1. Mshumaa Ni watoto wako Kama hutaweza kuwapa maarifa ya dunia ambayo umeweza kuyaona na kuyatatua hata siku ukiwa haupo hawatatambua uwepo wako. Ila Kama utaweza kukaa chini na kuzungumza nao pindi usipokiwepo watajua kuwa baba au mama walitusaidia kwelii na watu watasema kwelii wale watoto ni wa flani. Watoto wanachohitaji ni zawadi ambayo unayo ndani yako kama ni maarifa basi hauna budi kuwapa pia....