MJUE
ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA
WITO
NI NINI?
Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake
amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu
mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita
amtumikie katika eneo Fulani.
Wito:
Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito
wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na
Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo.
NITAJUAJE
NIMEITWA?
1.Utaisikia
sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa
kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu
mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza
agizo fulani.MUSA kabla ya kuanza kumtumikia
Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya
uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa
uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana kama utajiita kwenye
utumishi,tulia umsikie Mungu akisema na wewe na kukuelekeza nini cha kufanya
kaika wito aliokuitia. “Bwana alipoona
ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti,
akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.”KUTOKA 3:4
SAMWELI
“basi,
wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.Akamwendea Eli kwa
haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena.
Naye akaenda, akalala tena.Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli!
Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita,
mwanangu; kalale tena.Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana
lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye
akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli
akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto.Kwa hivyo Eli akamwambia
Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa
mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.Bwana akaja,
akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli
akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.”1SAMWELI 3:4-10Hapa
tunaona umuhimu wa kuitambua sauti ya Mungu.Yamkini Mungu amekuwa akikuita kwa
ajili ya utumishi lakini umekuwa ukisita ukifikiri ni akili na mawazo yako na umeshindwa kuitikia wito kama Samweli
kabla hajaijua sauti ya Mungu.Lakini baada ya kuijua sauti ya Bwana Samweli
aliitika.
YAKOBO
Mungu kabla ya kumtuma mtu katika
utumishi wowote uanza na kumwita mtu huyo.Hata mzee Yakobo/Israel alipoambiwa na Mungu ashuke Misri,Mungu
alisema nae kwa njia ya ndoto.Hata wewe Mungu atakuita kama bado haupo kwenye
utumishi.“Mungu akanena na Israeli
katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa.”YAKOBO 46:2
2.Mungu
akikuita atjitambulisha kwako:Kabla ya kuingia
kwenye wito wowote jitahidi kujua ni nani aliyekuita kwenye wito huo.Kuna watu
wanatumika wakidhani wanamtumikia Mungu kumbe siyo Mungu bali miungu.Wengine
wanatumika lakini hawafahamu ni nani wanayemtumikia.Mfano Musa alipo itwa Mungu
alijitambulisha kwake “Tena akasema,
Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa
Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.”KUTOKA
3:6
3.Mungu
atakuambia cha kufanya:Katika maisha ya kawaida hata mzazi akimwita mtoto
wake umwambia cha kufanya.Hata sisi Mungu anapoweka wito wa kazi yake ndani ya
mioyo yetu utuelekeza tufanye nini.Musa aliambiwa awaokoe watu wa Mungu “Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili
upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”KUTOKA 3:10
Asante
sana msomaji wangu kwa kuendelea kujifunza..Somo letu litaendelea tena wiki
ijayo.Mungu akubariki
Subira
Mlaga
Mwl,Mwandishi
naMzungumzaji
Simu:0672745219
Barua
pepe:subira.mlaga@yahoo..com
Nimebarikiwa Sana ila Kuna wakati mwingine huwezi sikia saut Kama ya msa nasikiaga msukumo hiyo ikoje?
ReplyDeleteHiyo pia Ni sauti ya MUNGU.
DeleteJe na kufanya kazi ya serikali ni wito au ni utandawazi wa kijamii
ReplyDeleteIyoo nikazi tofautisha wito na kazi
ReplyDeleteWenaye huelewi
DeleteUbarikiwe mtumishi wa Mungu ila akuna Yakobo 46
ReplyDeleteOkay 👍
ReplyDeleteAmen amen nimebarikiwa sana
ReplyDelete