Skip to main content

MUHTASARI KUHUSU YOPOCODE TANZANIA

MUHTASARI KUHUSU SHIRIKA LA YOPOCODE
Ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililosajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 24 ya NGOs ya mwaka 2002. Lililosajiliwa rasimi na kupata cheti cha usajili tarehe 12/04/2017 chenye namba ya usajili 00NGO/0009139.
MAKAO MAKUU 
Makao makuu yake yapo mtaa wa Mazingula, kata ya Ilembo, Halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya nchini Tanzania. Pia YOPOCODE wana Tawi lake katika Kata ya Ipembe, wilaya ya Singida katika Mkoa wa Singida.
DHAMIRA YA YOPOCODE 
Dhamira yake ni kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uwezo Wa kujitambua na kutumia rasilimali zinazo wazunguka na fursa mbalimbali zinazopatikana katika maeneo yao kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii.
DIRA YA YOPOCODE 
Dira yake ni kuwa shirika kubwa Tanzania litakalo wawezesha vijana kujitambua kwa kutumia uwezo walionao au vipaji au taaluma au rasilimali zinazo wazunguka ili kujiletea maendeleo katika jamii.
MALENGO YA YOPOCODE:
1. Ni kutoa elimu itakayowajengea uwezo vijana Tanzania kutambua na kutumia fursa zilizopo katika Jamii zao kwa maendeleo yao na jamii yao.
2. Kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya ujasiriamali na uchumi kwa vijana Tanzania.
3. Kuwahamasisha vijana Tanzania kushiriki katika shughuli za maendeleo
4. Kutoa elimu ya uzazi na maambukizi ya ukimwi kwa vijana Tanzania.
5. Kuwachochea vijana Tanzania kushiriki na kukubali mabadiliko ya kisera na kushiriki katika utekelezaji kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Jamii zao na taifa kwa ujumla Wake.

PROJECTS:
BINTI JITAMBUE TANZANIA
KIJANA JIAJIRI TANZANIA
NANENANE FESTIVAL 2018
YOPOCODE TRAINING CENTRE.
htts://yopocodetanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3. ...

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kuto...