Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2017

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KIBIASHARA

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI SEHEMU YA KWANZA IMEDHANIWA NA YOPOCODE KWA KUSHIRIKIANA NA TAMASHA LA NANENANE 2017 UTANGULIZI Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nimeamua kuuleta kwenu ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo. A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI? 1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza. 2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini. 3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k 4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE) 5. Wana uwezo

MWALIKO NANENANE 2017

MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA NANENANE 2017 LITAKALOFANYIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI ILEMBO UMALILA MBEYA VIJIJINI, MKOANI MBEYA, TANZANIA. Rejea kichwa cha habari hapo juu kama kinavyojieleza. Shirika la vijana Tanzania la “Youth Pontential for Community development( YOPOCODE)” Kwa kushirikiana na kundi la sanaa na utamaduni la TANZANIA YOUTH TALENT ASSOCIATION (TAYOTA) linakuletea Tamasha La Nanenane 2017 litakalofanyika katika viwanja vya shule ya msingi ya I lembo Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya nchini Tanzania kuanzia 01/08/2017 hadi 08/08/2017. a) Lengo la tamasha hili ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo ili kuinua maisha yao kiuchumi. b)Kuhamasisha vijana kujali na kulinda afya zao kwa kushiriki michezo na burudani mbalimbali zenye tija na kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana Tanzania. c) Kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana Tanzania. d) Pia Katika tamasha la nanenane 2017 tutalenga kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vi

BARUA YA NANENANR

YOUTH POTENTIALS FOR COMMUNITY DEVELOPMENT (YOPOCODE)        SIMU: +255-758 051641 , +255-768 577408 ,0765300255,0653983001, 0768416619 Barua Pepe: yopocode@gmail.com KWA MADIWANI WOTE WILAYA YA MBEYA VIJIJI/VIONGOZI WA VIKUNDI/TIMU/BENDI NA MTU MMOJA MMOJA YAH : MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA NANENANE 2017 LITAKALOFANYIKA VIWANJA VYA ILEMBO MBEYA VIJIJINI. Rejea kichwa cha habar i hapo juu kama kinavyojieleza. S hirika la vijana Tanzania la   “ Youth Pontential for Community d evelopment( YOPOCODE)” linakuletea Tamasha La Nanenane 2017 litakalofanyika katika viwanjwa vya shule ya msingi ya Ilembo Mbeya Vijiji kuanzia 01/08/2017 hadi 08/08/2017 .Lengo la tamasha hili ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo ili kuinua maisha yao kiuchumi. Pia kuhamasisha vijana kujali na kulinda afya zao kwa kushiriki michezo na burudani mbalimbali zenye tija na kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana Tanzania.Ili kufanikisha ta

YOPOCODE

Na Alfred MWAHALENDE ✅  Ukitaka mambo yako yaende vizuri katika malengo uliyojiwekea mwaka huu 2017 Fanya mambo yafuatayo ; ✳  imarisha na kujenga mawasiliona mazuri na mahusiano mazuri pia kati yako na watu wanaokuzunguka. Kama ni malengo ya kibiashara jitahidi kuwa na mawasiliona mazuri na wateja wako. Ili kukuza mawasiliona jitengenezee kitu kinaitwa " business cards" yenye mawasiliona yako yote muhimu yaani namba ya simu, email na hata website kama IPO. ✳  jijengee tabia ya  kwenda na wakati kwa lugha nyepesi unaweza kusema zingatia sana muda wako na ikiwezekana panga ratiba yako mapema. Usipoteze muda wako kwa vitu visivyokuwa vya msingi wowote katika maisha yako. Kila kukicha jiulize nitafanya nini Leo? Na nitaanza na nini?? Na kumalizia nini??? ✳  jiamini na kujidai mbele ya maadui zako, hapa namaanisha usiogope changamoto zilizopo katika kile unachotaka kukifanya. Kumbuka Uoga ni adui wa mafanikio yako. Pia Uoga ni udhaifu na ni dhambi kwa watu wanao Amini. Mtu a

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3.     Ujana ni hatua ambayo mtu anapi