NIKUKUMBESHE MAMBO KUMI NA MBILI (12) MUHIMU UNAYOTAKIWA KUYAFANYA
KATIKA KIPINDI HIKI CHA UJANA WAKO;
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unajijenga kielimu, imarisha misingi kwenye
taaluma mbalimbali yaani elimu ya msingi ya darasani na elimu ya stadi za
maisha ya mtaani. Jijengee Maarifa makubwa yatakayokusaidia kuhamisha milima
yaani changamoto. Pia katika elimu usisahau elimu ya dini, elimu ya afya,
biashara, ujasiriamali na mahusiano.
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unapata ardhi au kiwanja chako na uanze kuweka
malengo ya kujenga.
² wekeza kwenye
chochote unachohisi au unachoona kinaweza kukuingizia kipato chako, usiogope
kuwekeza kwenye fursa ndogo ndogo zinazoweza kukuingizia kipato.
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unaingia kwenye mahusiano ya kweli na ndoa.
Unapofikia ujana hakikisha unajijengea mahusiano mazuri, unitumie silaha ya
ujana kujiingiza katika mahusiano na kila inayemuona mbele yako.
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unakwepa kujiingiza kwenye starehe zisizokuwa
za lazima, achana na tabia za ulevi, matumizi mabaya ya muda na pesa, kumbuka
wakati wa ujana ni wakati wa kukusanya utakachokula uzeeni.
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unafungua akaunti ya pesa ili uweze kuanza
kuweka akiba kwa matumizi ya baadaye. katika kipindi hiki cha ujana
hakikisha unajenga uaminifu kwa kila mtu yaani uaminifu katika ahadi na matendo
yako.
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unakuwa na marafiki wenye tija, pia marafiki
wanakujenga kiakili na kukusaidia kutimiza kusudi lako, achana na marafiki
wanafiki, wafitini na wenye wivu wa kijinga. Pia angalia marafiki wanaokutia
moyo na kukukosoa pale unapokosea.
² katika
kipindi hiki cha ujana hakikisha unaanza kufanya mambo yako kwa malengo.
Usifanya mambo bora yaenda, Fanya mipango kwa utuluvi mkubwa usikurupuke, weka
mikakati makini inayoweza kukutoa katika maisha yako.
hapo kuakikisha unatumia fursa zinazo jitokeza isipokuwa uwishi uasherati namengine mabaya
ReplyDelete