SABABU
ZINAZOPELEKEA FIKRA ZA VIJANA WENGI KUWA
HASI
MWANDISHI JOAS YUNUS JYB
Kadri binadamu anavyokua anakutana na mazingira mbalimbali .Mazingira
ni pamoja na watu tunaokutana nao,
vitabu tunavyosoma, mambo tunayoyaona na kusikia. Mazingira huanza kuathiri
mtazamo wa kijana wa kuzaliwa nao na kwa bahati mbaya vijana wengi mtazamo wao
chanya hubadilika na kuwa mtazamo hasi.
Mtu anapokuwa mdogo anapenda kufika mahali fulani lakini kadri
anavyoendelea mbele, ndoto zake huanza kuyeyuka kutokana na watu anaokutana nao
pamoja na vitu anavyosikia ambavyo hubadili mtazamo wake kutoka chanya kwenda
hasi. Wachache wanaokutana na mazingira sahihi ndio hao hufikia ndoto zao na
kuwa na mafanikio makubwa.
Zipo sababu kadha wa kadha zinazosababisha mtu kuwa na fikra hasi.
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na:
·
Marafiki
Vijana wengi wameshindwa kujua kuwa maisha tunayoishi na tutakaoishi
yanatokana na watu wanaotuzunguka.Kama unazungukwa na watu wenye mtazamo hasi
basi hata wewe utakuwa hivyo hivyo. Vijana wengi sasa wameshindwa kuwa na jicho
la tatu la kujua nani na kwanini anapaswa kuwa rafiki yake. Unapokuwa
umezungukwa na watu wanaomini kuwa mafanikio ni ajali, mafanikio ni bahati,
mafanikio ni kwa baadhi ya familia ni lazima mtazamo wako uanze kuamini vitu
hasi.
o
Vitabu
“Kimuingiacho mtu ndicho
kimtokacho”. Ukweli ni kwamba vitabu tunavyosoma vina athari kubwa kwenye maisha
yetu. Watu wengi wamekuwa wasomaji wa vitu ambavyo haviwajengi. Vijana wengi
hupenda vitabu vya udaku kuliko vitabu vya kuwaletea maendeleo yao na
vinavyojenga maadili.
Ubongo wako ni kama tumbo lako linalohitaji kula kila siku. Kama tumbo
likiingiliwa na kitu kibaya huathirika. Hata ubongo pia unapokuwa umepata vitu
vibaya huathirika vivyo hivyo.
o
Vitu
tunavyosikiliza na kuangalia.
Runinga zetu na redio zetu zina athari kubwa kwenye maisha yetu ya kila
siku. Vijana wamekuwa wakisikiliza na kuangalia sana nyimbo za kuamsha mapenzi
kwa muda mwingi badala ya kusikiliza vitu vya msingi vya kujenga maisha yao.
Unaposikiliza au kuangalia kitu kwa muda mrefu kinakaa akilini na
kuathiri sehemu ya ubongo. Unapotumia muda mwingi kusikiliza vitu vibaya maana
yake sehemu kubwa ya ubongo wako ambao ndio huratibu maisha yako utakaliwa na
vitu vibaya visivyo na tija.
o
Mfumo wa
Elimu yetu:
Mfumo wa elimu pia umesababisha kuwajenga watu kuwa na mitazamo hasi ya
kuamini kuajiriwa kuliko kutumia uwezo ulioko ndani yao katika kuzalisha na
kutengeneza ajira zao binafsi na za watu wengine .
Siku moja nikiwa nasoma chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Mlimani,
mhadhiri aliongea neno moja ambalo lilinishangaza mhadhiri alisema maneno haya “Ukimaliza chuo hiki si rahisi kukosa
ajira” maana yake kwamba mhadhiri anaamini katika kuajiriwa tu. Nilitegemea
mhadhiri angesema maneno haya “Ukimaliza
chuo hiki unao uwezo wa kuwa na kampuni yako na taasisi yako”. Msemo wa
hadhiri ulinionesha wazi kuwa elimu
tunayosoma darasani haituandai sana kusimamia shughuli zetu binafsi.
Naomba nieleweke kwamba
kuajiriwa si kubaya lakini kibaya ni
kuwajenga watu katika mitazamo ya kuajiriwa tu wakati wana uwezo mkubwa wa
kujiajiiri .
o
Mapokeo
Vijana wengi huamini katika kile walichokikuta katika familia zao, nchi
yao n.k. Huamini kuwa maisha ni bahati na nyota jambo ambalo si sahihi.Vijana
huamini kama maisha tunayoishi yanatokana na historia ya familia zetu jambo
ambalo siyo kweli .Kuzaliwa kwenye familia maskini siyo kigezo cha wewe kufa
maskini .Hatuwezi kuchagua tuzaliwe katika familia yenye hadhi gani lakini
tunaweza kuamua tufe tukiwa na familia za hadhi gani.
Comments
Post a Comment