Skip to main content

ILI KUYAFIKIA MALENGO YAKO ZINGATIA YAFUATAYO

ILI KUYAFIKIA MALENGO YAKO ZINGATIA YAFUATAYO
u  Muda, muda hauna urafiki na mtu, hausimami labda usimamishe saa yako, haukusubiri ujiweke sawa. Wenyewe unasongambele na haurudi nyuma, kinachotakwa ni wewe kuwa na mpango na ratiba yako
u  kuwa na mtizamo chanya, kuwa na malengo na fikiria kufanikiwa na sio kusindwa, siku zote kinacho kwamisha watu ni mawazo hasi na yanatokana na changamoto unazokumbana nayo,jifunze kuwa mvumilivu na mtatatuzi wa changamoto zako, acha kufuata historia na kusikiliza wailioshindwa na wenye wivu kwakuwa watakukatisha tamaa daima ili uendelee kufanana nao .
u  kuwa mtafiti penda kukijua unachotaka kukifanya au unachofanya kiundani zaidi na jua faida na hasara zake, utanufaika vip na kwa wakati gan na kina nani watakuwa wateja wako ,
u  Jitumekuwa na nia ya dhati kwa kile unachokifanya , tumia uwezo wako kia kili na kifikra kuhakikisha unafanikisha lengo lako kuu ambalo ndilo lililo kupelekea kuwa na wazo hilo, siku zote  uvivu ndi adui wa maendeleo, usikubali kuishia katikati kwakuwa utakuwa umepoteza muda na rasilimali nyingi pale mwanzon na usifaidike na chochote,
u  Uvumilivu hiki ndicho kitu cha msingi kuwa mvumilivu, kuna uvumilivu wa vitu vingi:; ~Changamoto zikizidi
~Maneno ya kukatisha tamaa
~kuchekwa
~Kuzaraulika
~Maneno ya kukera
Uvumilivu utakufanya uwe mkaka mavu na mwenye binu mbadala.
u  Kujiheshimu na kuheshimu wengine, kila mtu atakupenda na jua sio wote watakao kupenda hivyo, fanya yaliyo sahihi na usifanye ili kumfurahisha flani wakati kwako haitakuwa na manufaa yeyote, ishi vema na jamii yako itakusaidia kujiweka katika mazingira salama na endelevu yenye amani.

u   Uaminifu, ni gharama kubwa sana kumwamini mtu lakini huna budi ,inakupasa kujenga mazingira ya kuaminika na kuwaamini wengine kwakuwa katika dunia ya sasa ya utandawazi watu hufanya vitu kwa pamoja  na kwa kushirikiana , zama za ubinafsi zimepitwa na wakati.

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana kama uta

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3.     Ujana ni hatua ambayo mtu anapi