UKITAKA MAMBO YAKO YAENDE VIZURI
KATIKA MALENGO ULIYOJIWEKEA FANYA MAMBO YAFUATAYO ;
B) Jijengee tabia ya kutumia vizuri muda (wakati), kwa lugha nyepesi unaweza kusema zingatia sana muda wako na ikiwezekana panga ratiba yako mapema. Usipoteze muda wako kwa vitu visivyokuwa vya msingi wowote katika maisha yako. Kila kukicha jiulize nitafanya nini Leo? Na nitaanza na nini?? Na kumalizia saa ngapi???. Muda ni mali usipoutumia vizuri utaisha bila kufanya kitu.
C) Jiamini na kujidai mbele ya maadui zako, hapa namaanisha usiogope changamoto zilizopo katika kile unachotaka kukifanya. Kumbuka Uoga ni adui wa mafanikio yako. Pia Uoga ni udhaifu na ni dhambi kwa watu wanao Amini. Mtu asiyejiamini ni ngumu sana kufanikiwa katika maisha yake.
D) Uwe na nidhamu na heshima kwa watu wote bila kujali umri, hadhi au madaraka au muonekano. Usimdharau mtu yeyote. Mtu mwenye nidhamu na heshima ni mtu mwenye hekima pia. Mtu mwenye hekima kichwa chake hujaa Maarifa na utayari wa kujifunza mambo mengi kuhusu maisha na kazi yake.
E) Uwe mwaminifu na mkweli, ukitaka kufanikiwa katika maisha yako jijengee tabia ya uaminifu na kuwa mkweli, hapa pia jifunze kuwa na siri na kutimiza ahadi zako. Kwa mfano kikao ni saa kumi jioni wewe unakuja saa moja jioni, umekosa uaminifu na hujawa mkweli na umeshindwa kutimiza ahadi yako.
F) Uwe na lugha ya ushawishi kwa shughuli au malengo yako. Unaweza kuwa na jambo zuri lenye kuleta tija kwako na kwa Jamii nzima, lakini ukakosa nguvu ya ushawishi. Mtu mwenye lugha ya ushawishi kwa biashara au huduma yake atapata wateja na walaji wa bidha au huduma yake zaidi.
G) Jifunze kuwa mtu wa kutoa maamuzi usipende kila kitu kiamliwe na watu wengine. Jijengea tabia ya kuamua juu ya hatima ya maisha yako.
Uongo
ReplyDelete