Skip to main content

SABABU ZINAZOCHANGIA WATU KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO YAO

TUNAWEKA MALENGO SAWA NA HATUFANIKIWI SAWA, NINI SABABU YA WATU KUSHINDWA KUYAFIKIA MALENGO YAO
Duniani kote kila mwishoni au mwanzoni mwa mwaka watu hupanga Malengo mengi sana, tena hupanga Malengo mazuri, ukiyaangalia unaona mafanikio makubwa mbele yao. Na umekuwa ni Utamaduni uliozoweleka sana watu kupanga Malengo kila mwishoni na mwanzoni mwa mwaka.
Kwa mujibu wa takwimu Bubu inaonyesha kwamba katika kila watu million moja ambao huweka Malengo, nusu yake huwa wanasahau kabisa ifikapo mwezi machi na robo 3 huishia kusingizia changamoto zinazowazunguka na 1/3 yake ndo huyafikia malengo yao.

HEBU TUANGALIE NI SABABU ZIPI ZINAZOCHANGIA HALI HII????
ü        Kukosa nidhamu ya matumizi ya pesa na muda. Utajiri wa kwanza duniani ni matumizi mazuri ya muda/wakati, ukitumia muda na pesa vibaya huwezi kuyafikia malengo yako.
ü        Aaina ya marafiki ulionao,     inayoweza kukufanya ushindwe kuyafikia mafanikio yako ni marafiki, hapa nazungumzia marafiki wasiokuwa na tija kwako, ukiendekeza kuwapa nafasi marafiki kuchezea Malengo yako huwezi kusonga mbele. Sisemi usiwe na marafiki, uwe na marafiki wenye ushawishi na ndoto zako. 
ü        Kukosekana kwa Maarifa na taarifa muhimu kuhusu Malengo yako, siku zote unapoweka Malengo yako, jitahidi kutafuta Maarifa na taarifa zinazoendena na Malengo yako. 
ü        Kukimbilia kila fursa inayojitokeza mbele yako huku ukisahau Malengo yako. Siyo fursa zote zinazokuja kwako zaweza kuwa na faida kwako, kinachotakiwa ni wewe kuzichunguza fursa na kuona katika zinawezekana kwako. Lakini pia fursa mpya zisikuharibie malengo na ndoto zako.
ü        Changamoto za afya na elimu, unapoweka Malengo yako huku ukisahau kuitunza afya yako utaishia kuutumia muda wa kutekeleza mipango yako kutibu afya, unapoweka Malengo yako, pia hakikisha unajali afya yako. Pi elimu, unapoweka Malengo yako usisahau kujiendeleza kielimu ili uendane na mabadiliko yanayoikumba duniani kisayansi na kiteknolojia.
ü        visingizio, ukiwa ni mtu wa kupenda kusingizia mambo mbalimbali huwezi kufanikiwa katika kuyafikia Malengo yako
KWA MFANO
u      Sina elimu
u      Rais kabana
u      Wazazi wangu hawakuniwekea msingi
u      Serikali hainijali
u      Ndugu zangu hawanipendi
u      Sina hela.
ü        Kukosa uthubutu, unaweza kuweka mipango mizuri sana lakini ukakosa nguvu ya uthubutu yaani nguvu ya kujaribu kufanya.
ü        Tamaa ya kutaka kufanya kila kitu bila kuweka vipaumbele katika malengo yako
ü         uvivu, Uoga na kutokujitambua, lazima ujitambue kuwa wewe ni wa pekee Sana na lazima ujue kama hutafanya wewe hakuna mwingine wa kufanya.


Comments

Post a Comment