KIJANA NI NANI?
NA MWANDISHI,
JANEROSA
MAFWIMBO
Neno kijana limekuwa
na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa,
jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata
baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo:
Kijana ni mtu wa
miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa.
Mathalani nchini
Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya
maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya
maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema
kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.
Hivyo basi
kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa
mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea
na kufanya maamuzi yake binafsi.
Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa
kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na
sekondari kutokana na sababu mbalimbali hasa za kimakuzi. Kuna tofauti kati yao
na miongoni yake ni hizi:-
MTOTO
|
KIJANA
|
Umri miaka 0-10 hapa wengi wao ni watoto wasiopevuka,
11-17 ni walio katika upevukaji (balehe).
|
18-35 ni umri wa vijana ambao wamepevuka na wanakuwa na
tofauti kubwa katika maumbile yao.
|
Kisheria miaka 0-17 ni mtoto.
|
Kisheria miaka 18-35 ni kijana.
|
Akili yao haijapevuka na huwa na utoto mwingi.
|
Akili imepevuka na anaweza kuwa na mambo ya kiutu uzima.
|
Hana haki ya kufanya maamuzi yake bila kushirikisha wazazi au walezi.
|
Anahaki ya kufanya maamuzi yake bila wazazi au walezi kushiriki.
|
Hawezi kushiriki masuala mbalimbali kama vile siasa, ajira na
yasiyohusika kisheria.
|
Anauhuru wa kushiriki masuala mbalimbali kama vile siasa, ajira
na masuala yote yanayohusu jamii kwa ujumla.
|
MAMBO MUHIMU YA
KUANGALIA UNAPOELEZEA
MAANA YA KIJANA.
Utambuzi:
Kijana ni lazima awe na utambuzi binafsi, utambuzi wa jamii yake na mazingira
Kijana ni lazima awe na utambuzi binafsi, utambuzi wa jamii yake na mazingira
yanayomzunguka.
Kujitambua kunamfanya kijana kufanya mambo sahihi na kuenenda sawa na
maadili
ya jamii na Taifa kwa ujumla. Hapa kijana anakuwa na uelewa wa kipi nifanye na
kipi
nisifanye.
Ukomavu wa
akili:
Katika umri wa miaka 18 vijana wengi wanakuwa na akili ya kufanya
Katika umri wa miaka 18 vijana wengi wanakuwa na akili ya kufanya
Mambo
ambayo yanaendana na umri huo,kijana pia ataweza kuwa mshauri kwa wenzake,familia
na
jamii aliyomo. Hapa ndipo kijana anapanga malengo yake na kuanza ufuatiliaji
ili
yatimie,kamavile
kubuni wazo fulani lenye manufaa kwake au jamii, biashara au kufikiria kazi
nzuri
anayoweza kufanya.
Uelewa
wa changamoto:
kijana ni lazima aelewe changamoto mbalimbali na kujua jinsi ya
kijana ni lazima aelewe changamoto mbalimbali na kujua jinsi ya
kukabiliana nazo. Changamoto hizo ni
kama tatizo la ajira kwa vijana mtu utawaza kujiajiri au
kutafuta kazi halali itakayokuingizia
kipato.
Kujenga hoja
: umri mzuri wa kuwa na hoja zenye nguvu katika masuala mbalimbali.
: umri mzuri wa kuwa na hoja zenye nguvu katika masuala mbalimbali.
Unapokuwa
kijana ni lazima uwe mwepesi katika kushiriki masuala mbalimbali na kujenga
hoja
ambazo
zinanguvu na kufanya usikilizwe na jamii hata Taifa.
Ushawishi:
Kijana ni lazima uwe na ushawishi kuhusu jambo fulani,katika kushawishi ndipo
Kijana ni lazima uwe na ushawishi kuhusu jambo fulani,katika kushawishi ndipo
tunaona
nguvu ya kijana na kuanza kutengeneza Taifa imara. Vijana wengi wa sasa
tunajitahidi
sana
kuwa na nguvu ya ushawishi katika masuala tofautitofauti. Pia tunaona asasi
nyingi
zikiongozwa
na vijana wenyewe ili kuweza kushawishiana mambo yenye tija kwa maisha ya
kijana.
Hivisasa vijana kushawishi wenzao kushiriki uongozi, kupiga kura, kushiriki
huduma za
kijamii
na kitaifa.
KIJANA
ANAPASWA AFAHAMU MAMBO HAYA KUMHUSU
AJITAMBUE:
Kijana ni lazima ajitambue na kutambua fursa mbalimbali zinazowahusu vijana.
Kijana ni lazima ajitambue na kutambua fursa mbalimbali zinazowahusu vijana.
Siku
hizi kuna masuala mengi ambayo vijana wanashiriki hivyo kijana anaweza
kushiriki
uongozi,
ajira, ujasiriamali na mengine mengi. Unapojitambua ni lazima ujue thamani yako
na
kusudi
la uwepo wako ili uweze kufanya mambo mazuri sana kwa jamii na taifa kwa
ujumla.
AJIKUBALI:
kujikubali ni hali ya kuyapokea mambo yote yanayokuhusu, kijana anapaswa
kujikubali ni hali ya kuyapokea mambo yote yanayokuhusu, kijana anapaswa
kujikubali
vile alivyo hii itasaidia kusonga mbele zaidi.Hapa mfano mtu unatatizo fulani ambalo
linakufanya
tofauti na wengine unapaswa kujikubali
ili ujione kuwa ni wa thamani kama
walivyo
wengine. Unapojikubali unaweza kujiona kawaida na kufanya mambo makubwa kwa
familia,jamii
na Taifa na kufanya utambulike na uweze kuwa mfano wa kuigwa.
AWE
NA SHAUKU , NIA AU KIU:
kijana ni lazima uwe na shauku nia au kiu ya kufanya vitu
kijana ni lazima uwe na shauku nia au kiu ya kufanya vitu
vya
tofauti vyenye lengo la kuelimisha kuonya au kuasa jamii na pia kuishi maisha ya
kusaidia
wenginekatika
kujenga au kutikmiza kusudi, maono au matarajio yao.
AWE
MZALENDO:
Kijana anapaswa kuwa mzalendo sana. Hapa kama kijana inabidi ujiulize
Kijana anapaswa kuwa mzalendo sana. Hapa kama kijana inabidi ujiulize
na
ujue kusudi la kuzaliwa na kukwepo Tanzania. Ni lazima ujue kuwa unapaswa
kufanya
uzalendo
kwa nchi yako,ufanye yaliyo mazuri kwa jamii ya Kitanzania. Hivyobasi, kijana
na
vijana
tunapaswa kuelewa na kutambua nafasi yetu binafsi kwa familia zetu, jamii,
wilaya, mkoa
na
Taifa kwa ujumla ili tuweze kufanya mambo ya busara katika kuchochea maendeleo
ya nchi
yetu.
UJANA NI NINI?
·
Ujana
ni hatua ambayo mtu anapitia baada ya utoto.
·
Ujana
ni hali ya kuwa na tabia za umri wa ujana ambao ni miaka 18-35.
·
Ujana
ni kipindi cha makuzi ya mtu kabla ya utu uzima na hatimaye uzee.
·
Ujana
ni kipindi kati ya miaka 18-35 hivi ambapo mtu anakuwa amepevuka na ukomavu wa kiakili
na kimwili.
Hali
ya ujana huanza baada ya maumbile ya mtu kubadilika na kuanza kuwa na hisia za
kimwili na kutamani kuwa na uhuru wake katika maamuzi. Hiki ni kipindi chenye changamoto nyingi sana
kwa kijana, sababu anakuwa amekumbana na hali mpya ya mabadiliko ya mwili na
anajiona yupo tofauti na aliyokuwa mwanzo.
Katika
ujana kuna vichocheo, hisia na mabadilio mbalimbali ya kimwili na tabia kwa
ujumla.
Mabadiliko
ya kimwili ni yale yanayoambatana na ukuaji wa mtu toka utoto kuelekea ujanani.
Mabadiliko
hayo huambatana na vichocheo vya mwili pamoja na hisia kali sana za
kimaumbile,katika kipindi cha ujana ndipo hutokea mihemko na matamanio mengi
hasa ya kukaa au kuwa na urafiki na mtu wa jinsia nyingine.
Mahusiano
baina ya kijana wa kike na wa kiume ndipo huanza, utovu wa
nidhamu,ujeuri,kiburi,na kujisikia au kujiona bora kwa kijana.
MAISHA YA UJANA YANAAMBATANA NA TABIA HIZI;
·
Kuwa
mbichi,mwenye nguvu, na kuchangamka.
·
Kutokuwa
na ukomavu wa kutosha sababu bado upo
kwenye ukuaji.
·
Kuwa
na nguvu nyingi kimwili na kiakili.
·
Kuwa
na majukumu machache na uhuru mwingi.
·
Kuwa
na muda wa kutosha kufanya mambo mengi.
·
Kuwa
na shauku ya kufanya mambo mazuri katika maisha yako.
·
Kuwa
na muda wa kushirikiana na vijana wengine katika masuala ya maendeleo.
MAMBO YA KUFANYA
KATIKA MAISHA YA UJANA
·
Nidhamu: Ujana ni lazima uambatane na nidhamu ya hali ya
juu ili uweze kuvuka vikwazo mbalimbali.
·
Heshima: Heshima utakayoionesha wakati wa ujana ndiyo
itakayokusaidia uzeeni,utaheshimika kama ulivyoheshimu wengine.
·
Uwajibikaji: Jifunze kuwajibika katika majukumu mbalimblai ili
ufanikiwe.
·
Msingi wa maisha yako: Ni lazima kufahamu namna ya
kujiandalia maisha ya baadaye.
·
Chagua marafiki wema na sahihi: Jua kuchagua marafiki wanaofaa katika
shida na raha
·
Uhusiano: Tengeneza uhusiano wenye matokeo chanya,fahamu
uhusiano wenye mafanikio na kuchagua watu wema kwenye mahusiano.
MATOKEO YA
KUUTUMIA UJANA VIBAYA
Majuto na malalamiko:
Ukitumia vibaya ujana wako ni lazima ujute na kulalamika uzeeni.
Ukitumia vibaya ujana wako ni lazima ujute na kulalamika uzeeni.
Kulaani watu au kulaaniwa:
Kuwalaani watu ambao unahisi walifanya ushindwe au watu kukulaani kutokana na mwenendo wako.
Kuwalaani watu ambao unahisi walifanya ushindwe au watu kukulaani kutokana na mwenendo wako.
Kushindwa au kutofaulu katika maisha:
Usipojifunza na kuwajibika basi kuna hatari ya kushindwa au kutofaulu malengo ya maisha yako.
Usipojifunza na kuwajibika basi kuna hatari ya kushindwa au kutofaulu malengo ya maisha yako.
Kuchanganyikiwa:
Ukiutumia vibaya ujana kwa mambo yasiyofaa kama vile bangi, madawa ya kulevya, sigara na pombe yanaweza kukufanya uchanganyikiwe.
Ukiutumia vibaya ujana kwa mambo yasiyofaa kama vile bangi, madawa ya kulevya, sigara na pombe yanaweza kukufanya uchanganyikiwe.
MAMBO YA KUFANYA KATIKA MAISHA YA UJANA, (nyongeza)
ReplyDeleteTENGENEZA MAZINGIRA YA KUAMINIKA NA KUAMINI WENGINE.
Kumwamini mtu na gharama sana na kuaminka ni kazi kubwa ,lakin kwa upande mwingine ni jambo rahisi kutengeneza mazingira ya kuaminika endapo kama unayo nia ya dhati ya kufanikiwa katika kile unacho kifanya ni lazima uwe muungwana, mwenye hekima na busara pia uvumilivu na maamuzi yasiyo ya kukurupuka yatakusaidia kujenga uaminifu katika jamii na muhimu zaidi acha tamaa na majungu.
Nimependa sana jinsi ""Kijana" alivyochambuliwa katika makala hii.
ReplyDeleteNimependa sana
ReplyDeleteWaoooo nimependa hii nimekuwa nikitafuta sana makala hii Mimi kama msimamizi wa vijana
ReplyDelete0689188156
DeleteNzurii sana
ReplyDelete