UKITAKA MAMBO YAKO YAENDE
VIZURI KATIKA MALENGO ULIYOJIWEKEA FANYA MAMBO YAFUATAYO ;
A) Imarisha na kujenga mawasiliona mazuri na mahusiano mazuri pia kati yako na watu wanaokuzunguka. Kama ni malengo ya kibiashara jitahidi kuwa na mawasiliona mazuri na wateja wako. Ili kukuza mawasiliona jitengenezee kitu kinaitwa “business cards" yenye mawasiliona yako yote muhimu yaani namba ya simu, email na hata website kama ipo.
B) Jijengee tabia ya kwenda na wakati kwa lugha nyepesi unaweza kusema zingatia sana muda wako na ikiwezekana panga ratiba yako mapema. Usipoteze muda wako kwa vitu visivyokuwa vya msingi wowote katika maisha yako. Kila kukicha jiulize nitafanya nini Leo? Na nitaanza na nini?? Na kumalizia nini???
C) Jiamini na kujidai mbele ya maadui zako, hapa namaanisha usiogope changamoto zilizopo katika kile unachotaka kukifanya. Kumbuka Uoga ni adui wa mafanikio yako. Pia Uoga ni udhaifu na ni dhambi kwa watu wanao Amini. Mtu asiyejiamini ni ngumu sana kufanikiwa katika maisha yake.
D) Uwe na nidhamu na heshima kwa watu wote bila kujali umri, hadhi au madaraka au muonekano. Usimdharau mtu yeyote. Mtu mwenye nidhamu na heshima ni mtu mwenye heshima ana hekima pia. Mtu mwenye hekima kichwa chake hujaa Maarifa na utayari wa kujifunza mambo mengi kuhusu maisha na kazi.
E) Uwe mwaminifu na mkweli, ukitaka kufanikiwa katika maisha yako jijengee tabia ya uaminifu na kuwa mkweli, hapa pia jifunze kuwa na siri na kutimiza ahadi zako. Kwa mfano kikao ni saa kumi jioni wewe unakuja saa moja jioni, umekosa uaminifu na hujawa mkweli na umeshindwa kutimiza ahadi yako.
F) Uwe na lugha ya ushawishi kwa shughuli au malengo yako. Unaweza kuwa na jambo zuri lenye kuleta tija kwako na kwa Jamii nzima lakini ukakosa nguvu ya ushawishi. Mtu mwenye lugha ya ushawishi kwa biashara au huduma yake atapata wateja na walaji wa bidha au huduma yake.
G) Jifunze kuwa mtu wa kutoa maamuzi usipende kila kitu kiamliwe na watu wengine. Jijengea tabia ya kuamua juu ya hatima ya maisha yako.
Comments
Post a Comment