Skip to main content

Posts

Showing posts from 2018

SAJILI NGO YAKO TANZANIA

SAJILI NGO YAKO TANZANIA Je, unahitaji ‘NGO’? Fahamu utaratibu wa kusajili NGO ni kifupi cha neno Non-Governmental Organization. Kwa Kiswahili neno hili humaanisha shirika lisilo la kiserikali. Kawaida Serikali huwa ina mashirika yake, kwa mfano Shirika  la Bima, Shirika la  Nyumba, Shirika  la Umeme, mashirika ya vyakula n.k.   Tunapozungumzia NGO maana yake ni kuwa ni mashirika ambayo kwa namna yoyote ile Serikali haihusiki na umiliki wake. Ni mashirika ambayo humilikiwa na watu binafsi.  Serikali huweza kushirikiana nayo tu, lakini si kuyamiliki. Taratibu za uanzishaji, usajili na uendeshaji huratibiwa bayana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002. 1. YAPI YAWE MALENGO YA KUANZISHA NGO Malengo makuu ya kuanzisha NGO yawe ni kusaidia makundi au kundi maalum katika jamii. NGO siyo shirika la biashara.  Siyo kampuni ambayo muanzishaji  wake hutarajia kutengeneza faida. NGO ni shirika la hisani. Ni shirika la kujitolea kusaidia makundi jamii. Usi

MARIAM KILYENYI

Tunapozungumzia waambaji wa nyimbo za injili wanaofanya vizuri sana Tanzania, tusisahau huyu Binti yetu @Mariam Kilyenyi ANAENDA KUFANYA UZINDUZI MKUBWA WA ALBAMU YAKE 02/12/2018 KKKT SINZA KUMEKUCHA #Malkiawamoyowaupendo #mamawahaki #BintiAmkaTanzania #Dirayakijanatanzania @MariamKilyenyi https://www.instagram.com/p/BqHqvUagooy/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=i5c6b2btxpc1

ENDELEA KULIPA GHARAMA ZA KUTIMIZA NDOTO ZAKO

ENDELEA KULIPA GHARAMA ZA KUTIMIZA NDOTO ZAKO Kila ukitazama ndoto ambazo umetimiza ni jambo gani linakujia katika tafakari yako? Najua yapo mambo mengi ambayo unakumbuka, jinsi ulivyopambana kuhakikisha unapata hicho ulichokipata. Kuna gharama ulilipa na kwa baadhi ya watu walikuona kana kwamba unacheza. Ndivyo ilivyo, unapojua kile unachokitaka usisubiri watu waseme kuwa ni wazo zuri bali wewe jiamini kuwa hiki ninachokifanya ni sahihi na nitapata matokeo chanya. Jambo lolote zuri kwenye maisha hupatikana kwa kupambana zaidi. Najua Januari 2018 ulijipangia malengo ya kutekeleza mwaka huu. Lakini kila ukiangalia kwenye daftari lako huoni chochote ambacho umefanya au umepambana lakini hakuna matokeo uliyotarajia kupata. Unapoona kuwa hujatimiza malengo yako, ni nini unafanya? Unakata tamaa? Hapana ni kujifunza tu mahali ulipokosea ili kuandika historia mpya kwenye maisha yako. 1. Usiichoke safari ya maisha yako 2. Endelea kujifunza kwani hakuna jambo linaloshindikana 3.

THAMANI YA CHANGAMOTO.

THAMANI YA CHANGAMOTO. NGUVU YA HISIA . Series 05. Saul Kalivubha. Hisia ni sehemu ya binadamu aliye kamili , na hisia ni sehemu ya AFYA , ...lakini kuna NGUVU YA AJABU SANA iliyomo ndani ya HISIA , nayo ni UWEZO WA KUFANYA UPOFU .  Unapoanza kusukumwa na HISIA ,utafanya maamuzi , mwisho wa siku maamuzi hayo yataleta MATOKEO ,....NGUVU iliyomo ndani ya HISIA NI KUKUFANYA KIPOFU , USIONE ATHARI ZA MATOKEO zitakazotokana na MAAMUZI YA HISIA. Hali hiyo ndio inafanya watu wengi wajutuie maamuzi ya HISIA  waliyoyafanya huku wakiamini ni sahihi kwa wakati ule ,lakini leo wanaishi MATOKEO yanayowaumiza. TIBA: HISIA hushawishi MAAMUZI, jitahidi  sana ufahamu athari za maamuzi kabla na HISIA isiwe ndio sababu ya kwanza KUKUFANYA UAMUE . http://kalivubha.blogspot.com/2018/02/mambo-matano-muhimu-kabla-ya-biashara.html?m=1 Facebook na instagram , tembelea kurasa zetu za FIKIA NDOTO ZAKO.      FIKIA NDOTO ZAKO.        0652 123707.

HOW TO BE A COMEDY WRITER

JAMII 100; Vichekesho na Ucheshi katika sura ya biashara ya kale iloanza kukua toka zamani na itazidi kukua kadri muda uendavyo. Mambo ya kuzingatia; Vichekesho ni fursa kubwa kibiashara na imetengeneza wafuasi wengi kwa maana kucheka ni moja ya tiba na kuipa akili utulivu. Kitabu; HOW TO BE A COMEDY WRITER, Secrets from the inside by Marc Blake ( Namna ya kuwa mwandishi wa vichekesho, siri kutoka ndani ) Vitimbi, Mizengwe, Futuhi, Joti Tv, Ze komedi, Cheka tu, Churchill show, Omondi, Mc Pilipili ni moja ya picha kubwa kwa namna gani vichekesho au ucheshi ulivyofanya maisha ya watu wengi wapende kufuatilia na kufurahi wasikiapo au wakitazama. Kucheka kuna raha yake na tunaona namna hata mwili huwa katika utulivu pale ambapo unakutana na kitu cha kukufanya ucheke. Je umewahi jiuliza kwanini watu hucheka ?, nini kinachowasukuma watu walipe na hata kuhudhuria majukwaa ya ucheshi. Inawezakana ikawa ni zoezi gumu kuelezea kwa maneno lakini ucheshi au vichekesho vinakufanya ujisikie vi

HII PIA NI SABABU

HII PIA NI SABABU Yapo mambo mengi yanayosababisha ndoto kutotimia kwa watu wengi. Lakini hii ya kutokujua unataka nini hasa ndiyo sababu inayopelekea watu wengi kufanya vitu vingi na kuviacha havijatimia. Tunapokaribia mwishoni mwaka, kipindi cha tathimini binafsi ya mwaka mzima unajikuta huna ulichotimiza ila una mengi ambayo januari mpaka novemba umeacha na kuishia njiani. Kujua nini unataka katika safari ya maisha yako utapelekea kupigania nakuhakikisha unatimiza adhima hiyo. Watu wengi hawajui nini wanataka hivyo hata wanapojiwekea malengo yao bado hawanauhakika kama ni kweli ndicho wanachokitaka. Mwanajeshi anapokosa shabaha vitani na kumimi tu risasi sehemu ambayo adui hayupo, humaliza risasi zake na huwa katika hatari ya kipigwa na adui. Nini tunajifunza hapa::: 1. Jua unataka nini kwenye maisha haya unayoishi 2. Chukua kitu kimoja kifanye kwa muda mrefu mpaka pale utakapo pata matokeo chanya. Endelea kung'ang'ania usiwe mwepesi kukata tamaa. 3. Pasipo maono

SAJILI NGO YAKO SASA.

Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/IqsKWrZF0GH9UIN9bhLAxV SAJILI NGO YAKO SASA. 🇹🇿Taratibu za uanzishaji, usajili na uendeshaji wa NGO huratibiwa bayana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002. 1. YAPI YAWE MALENGO YA KUANZISHA NGO Malengo makuu ya kuanzisha NGO yawe ni kusaidia makundi au kundi maalum katika jamii. NGO siyo shirika la biashara.  Siyo kampuni ambayo muanzishaji  wake hutarajia kutengeneza faida. NGO ni shirika la hisani. Ni shirika la kujitolea kusaidia makundi jamii. Usitarajie kuanzisha NGO kwa ajili ya kutengeneza faida ya fedha. 2. MGAWANYO WA USAJILI WA NGO Usajili wa NGO umegawanyika katika makundi makuu manne. Kwa mujibu wa sheria, mgawanyo huu umelenga maeneo ya kijiografia. Hata hivyo, ada za usajili na mambo mengine muhimu katika usajili hutegemea mgawanyo huu. Kwanza,  kuna mgawanyo wa usajili wa ngazi ya wilaya. Usajili wa aina hii huiwezesha NGO kufanya shughuli zake ndani ya mipaka ya wilaya

Barua Kutoka Gerezani Kuhusu Maisha Na Mafanikio

#TANO ZA JUMA #45 2018; Barua Kutoka Gerezani Kuhusu Maisha Na Mafanikio, Mteja Muhimu Ambaye Hupaswi Kumpoteza, Fedha Ni Zao La Hamasa Na Ijue Thamani Ya Muda. Rafiki yangu mpendwa, Juma jingine la mwaka huu 2018 linaelekea kutuacha, ni juma namba 45, juma ambalo nina hakika limekuwa bora sana kwako, kwa sababu umejifunza, umechukua hatua na umepata matokeo ambayo yamekufundisha zaidi au kukupa hamasa zaidi. Kumbuka kwenye maisha hakuna kushindwa mpaka pale unapoamua kukata tamaa mwenyewe. Haijalishi umekutana na magumu kiasi gani, kama bado upo tayari kuendelea, bado unayo nafasi ya kufanikiwa zaidi. Ni swala la muda tu na utapata kila unachotaka kupata. Muhimu ni wewe udhibiti kile unachoweza kudhibiti na kuachana na vile visivyo chini ya udhibiti wako. Na kitu cha kwanza unachoweza kudhibiti, ambacho unapaswa kukipa kipaumbele ni hatua unazochukua wewe mwenyewe. Pia kitu ambacho hakipo kwenye udhibiti wako ni matokeo unayopata, usiumizwe nayo sana, wewe kazana na hatua unaz

MAMBO YA YANAYOZUIA MABADILIKO

MAMBO YA YANAYOZUIA MABADILIKO Kama wewe ni mzazi na una mtoto lakini kila mwaka mtoto wako hakui. Kila mwaka yupo vile vile, mzazi lazima achukue hatua ya kujiuliza kwa nini? Kama hajiulizi na kuchukua hatua basi ni wazi kwamba mtoto ataendelea kutokukua kabisa. Ndivyo ilivyo katika ndoto za maisha yetu, inawezekana kila mwaka unapanga malengo lakini hakuna mabadiliko katika maisha yako. Kila mwaka upo pale pale, ni muhimu kuchukua hatua na kujua ukubwa wa tatizo na uamue kubadilika katika maisha yako. Mambo yanayochangia kutokukua wa watu wengi ni kama ifuatavyo: 1. Kusikiliza maneno ya watu na sio kuamua hatima za maisha yao. Wapo watu wanasilikiza zaidi watu na sio kutengeneza hatima zao. Hata kama anapata wazo la biashara atajiuliza kwanza kwa watu kuhusu hiyo biashara akiambiwa tu hawezi basi anaishia hapo. 2. Hofu, watu wengi wanahofu ya mambo ambayo yanaweza kutokea kutokana na mabadiliko. Hivyo kutokana na hali hiyo watu wengi huamua kutokubadilika. Unataka kutimiz

NDOTO YANGU

💪🏻NDOTO YANGU💪🏻 ©ENG JACKSON  MAN OF PURPOSE 12 NOVEMBER 2018 BAADA YA........😂💉 Mpendwa katika kipindi cha kuelekea ndoto yako, ipo misimamo kadhaa ambayo mtu hujiwekea ili asijikwae njiani, lakini.......💉 Misimamo yako itapimwa baada ya kushinda vikwazo vyooote vya njiani na wala sio maneno matupu ya awali ,kwani wengi hupanga vizuri sana kiasi Kwamba ukisikiliza mipango yake unaweza kutamani akupe, lakini cha Ajabu akikutana na kakishawishi kamoja tu chali 😂. "Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele" Mithali 10:25 👆🏻 Habari njema ni Kwamba kama huatabadilika njiani ukamtegemea Mungu tu Basi hata Pepo zivume vipi Bado utabaki kua imara tu oooooh hallelujah 💪🏻. Email: mssawajack@gmail.com Fb: Jackson Mssawa Page: Sindano za Yesu Insta: mssawajack WhatsApp: 0766991342 💪🏻MSIMAMO CHANYA UNAHESHIMISHA💪🏻

#inawezekana

#inawezekana Mambo mawili ya kujilinda nayo unapokuwa katika wakati mgumu ni kile unachosema na kile unachoamua kukifanya kwa sababu hizo ndiyo silaha zinazoweza kukusaidia kutoka katika wakati mgumu au kukufanya uwe na wakati mgumu zaidi. Mambo mawili ya kujilinda nayo unapokuwa katika furaha ya mafanikio yako ni kile unachosema na kile unachoamua kukifanya kwa sababu kwa silaha hizo mbili unaweza kuongeza mafanikio yako au unaweza kukaribisha matatizo na kutowesha furaha yako. #lameckamos #2018more

NJIA NGUMU; Kurasa 12 kitabu cha kwanza cha mwaka mpya HATUA kubwa 2018/19

NJIA NGUMU; Kurasa 12 kitabu cha kwanza cha mwaka mpya HATUA kubwa 2018/19 Kitabu; WAR of SELF, The 7 Weapons of Self Mastery by Ramman Sheehan Turner ( Vita ya Binafsi, Silaha 7 za Ubobezi binafsi ) 60 ~ 72 SILAHA ya 3; Ona Ukweli katika udanganyifu na wewe ni sehemu ya Ulimwengu mzima ona mahusiano ya uwepo wako na watu na mazingira asilia yanayokuzunguka. HATUA ya KUCHUKUA; Ona uhalisia ulivyo na kila mara jua u sehemu ya ulimwengu na acha kujidanganya mwenyewe. Rafiki ukweli ni silaha yetu ya tatu ambayo itaondosha ugomvi ndani yako na kukuweka huru katika maisha yako. Pale unapoondoa ukweli basi unaangukia kujidanganya na ukijidanganya unajiweka katika kifungo. Je uko tayari kuishi maisha yako katika kifungo ikiwa waweza kuwa huru kwa kusema kweli au kujua kweli?. au ukweli wa mambo. Basi moja ya jambo ambalo watu wanajidanganya ni kujiona wao si sehemu katika ulimwengu, wanaona kuchukua au kutochukua hatua kwao hakuna athari katika Dunia. Si kweli kuwa athari yako haipo i

MAFANIKIO YANAHITAJI MABADILIKO.

MAFANIKIO YANAHITAJI MABADILIKO. Sijui unahitaji mabadiliko gani kwenye maisha yako ili kujiletea mafanikio? Inawezekana unahitaji kuwaacha marafiki zako waende. Inawezekana unahitaji maarifa mapya kwenye maisha yako. Inawezekana ni kuongeza juhudi katika kazi zako za kila siku. Inawezekana ni kupoteza kile ulichonacho ili kupata kitu kipya. Inawezekana ni kujitolea kwa mtu ili kupata ujuzi wa kutosha. Inawezekana ni kuajiriwa kwa mtu ili ujifunze na kisha kuanzisha biashara yako. Inawezekana ni kujua wapi unapaswa kwenda katika safari ya maisha yako. Inawezekana ni kujitolea na kuwapa watu wengine maarifa. "Gharama ya mafanikio ni kufanya kazi kwa juhudi, kuweka nia ya dhati ya kupata mafanikio na kuhakikisha unafanya kila kitu ambacho kitabadilisha maisha yako." Vince Lombardi. Mabadiliko chanya kwenye maisha yako yatategemea sana:- 1. Juhudi katika kazi zako 2.Kuweka nia ya dhati ya kubadilisha maisha yako. Hakuna mtu wenye jitihada na nia ya dh

WANAHITAJIKA MAWAKALA

WANAHITAJIKA MAWAKALA TanzaRice International inauza mchele mtamu wa Mbeya, uliochambuliwa, kusafishwa na kisha kufungwa vizuri katika mifuko standard ya kilo tano (5) inayouzwa kwa namna ya kibunifu inayowezesha walaji na wasambazaji kunufaika kifedha. Kampuni inatafuta mawakala 60 wa bidhaa zake katika viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam ili kusogeza Huduma karibu na wateja kote jijini. Sifa za Mwombaji 1. Awe na umri usiopungua miaka 18 2. Awe mtaji wa sh. 200,000/= na kuendelea 3. Awe na biashara au anataka kufanya biashara 4. Awe na simu/kompyuta yenye uwezo wa internet 5. Awe mwaminifu na mchapakazi. Wakala wa TanzaRice anapata faida ya sh. 1,000/= katika kila mfuko anaomuuzia mwanachama wetu na sh. 3,000/= katika kila mfuko anaomuuzia mteja wa kawaida. Pia kampuni inamlipa sh. 2,000/= kwa kumsajili mwanachama mlaji mpya. Zaidi ya yote,  wakala pia anapata kamisheni na bonus Kama wanachama wengine inayotokana na ulaji wa mchele wa TanzaRice. Iwapo una sifa

#inawezekana

#inawezekana Ikiwa kuna mambo watu wanayasema kuhusu wewe na hata wewe unajua wanavyosema ndivyo ilivyo au ndivyo ulivyo basi jitahidi sana kubadilika ili ujenge palipobomoka badala ya kuanzisha vita ya kupambana na wanaokusema kitu kitakachofanya uovu wako ukomae na kuharakisha anguko lako. Kusemwa ni vizuri tu na utimilifu wa uzuri huo ni pale ndugu msemwaji anapoamua kuchukua hatua chanya juu ya ukweli uliomo kwenye kinachosemwa. #lameckamos #2018more

KUHUSU KITABU CHA DIRA YA KIJANA TANZANIA

KUHUSU KITABU CHA DIRA YA KIJANA TANZANIA Ni kitabu pekee kilichobeba elimu stahiki ya stadi za maisha kwa vijana na chenye ubora wa hali ya juu kinachochambua na kutoa dira ya safari ya maisha ya kijana na miongozo inayotoa ramani ya kumsaidia kijana kujisimamia  mwenyewe na kujiajiri  kwa kutumia fursa mbalimbali za ujasiriamali zilizopo kama vile uwekezaji katika sekta ya  viwanda, kilimo biashara, ufugaji wa kisasa, madini, biashara ndogo ndogo, za kati na kubwa zilizopo katika jamii na kuweza kuendesha shughuli za uzalishaji mali na maisha yao bila kutegemea usimamizi kutoka kwa mtu mwingine ( kuajiriwa). K itabu hiki ni chachu ya mabadiliko chanya kwa vijana na kinatoa hamasa na ku wachochea vijana kushiriki katika harakati za kuleta maendeleo katika jamii zao na kukubali mabadiliko ya kisera na kuacha kukaa vijiweni kulia na kulalamika juu ya hali ngumu ya kimaisha (vyuma vimekaza) na ukosefu wa ajira katika sekta za serikali na mashirika binafsi na badala yake wa shiriki

KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA YAANZA RASIMI JIJINI DAR ES SALAAM.

KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA YAANZA RASIMI JIJINI DAR ES SALAAM. ☑ Yopocode kwa kushirikina na Mabalozi wa kampeni ya Binti Amka Tanzania wameanza rasimi kampeni katika shule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam. ☑ Akizungumza kwa niaba ya shirika la vijana Tanzania la YOPOCODE, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Alfred Sostern Mwahalende amekuwa na haya ya kusema"kampeni ya Binti Amka Tanzania inalenga kumsaidia mtoto wa kike nchini  kufika ndoto yake na malengo yake kielimu, kiuchumi na kiuongozi na katika hili pia tutalenga kupambana na masuala ya mimba na ndoa za utotoni ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakichangia katika kumkwamisha mtoto wa kike kufikia malengo  yake.Tumeanza na shule za misingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam huku tukifanya juhudi katika halmashauri zingine na mikoa mingine ambayo tayari tumeanza maandalizi ya kuzindua kampeni yetu" Katika kuhakikisha tunafikia lengo la

Binti Amka Tanzania

YOPOCODE kwa kushirikikiana na Mabalozi Wa Kampeni Ya Binti Amka Tanzania kanda ya/Dar es salaam na Pwani wanafanya kampeni mahususi inayolenga kumsaidia mtoto wa kike kufikia malengo yake kielimu, kiuchumi na kiuongozi. Aidha kampeni inalenga kupambana na changamoto mbalimbali zinazomkwamisha mtoto wa kike kufikia ndoto zake ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, utoro wa masomo, mfumo dume katika jamii, kukosekana mahitaji na mifumo sawa kwa jinsia zote, kupata fursa sawa na vipaumbele sawa. Tumependekeza maeneo mbalimbali kuyafikia ikiwemo shule za misingi na sekondari ili kufanikisha kampeni yetu ya Binti Amka Tanzania. Binti Amka Tanzania Alfred Mwahalende Alfred Mwahalende YOPOCODE TANZANIA Youth Potentials for Community Development - Yopocode Yopocode-Singida Youth Potentials For Community Development