MAMBO 5 YANAYOWEZA KUKUSAIDIA KUTIMIZA MALENGO YAKO KWA WAKATI.
1.
Anza mapema utekelezaji wa malengo
yako,”Wahenga wanasema mambo mazuri hayahitaji haraka” lakini napenda
kukushauri kwamba unapopata wazo zuri katika malengo yako usisubiri sana, ukikaa na wazo muda mrefu sana bila kulifanyia kazi utasahangaa uzito wa wazo lako unapungua siku hadi siku.
"wazo/lengo siyo lako mpaka uanze kulifanyia kazi ndiyo litakuwa lako" waweza kuwa na malengo mazuri na makubwa tena makubwa ya kuleta mapinduzi makubwa, lakini kama hujaanza kuyawekea utekelezaji mapemayatabaki kuwa mawazo. jitahidi kuanza mapema kutekeleza juu ya malengo yako.
2.
Usitumie muda mwingi kuwaza na kusimulia watu
juu ya Malengo, usimushirikishe kila mtu katika Malengo yako Bali angalia watu
wanaofanya kile ulicholenga kukifanya, kwa mfano kama lengo lako ni kufungua
biashara, angalia watu wanaofanya biashara inayofanana jaribu kuwashirikisha
upate undani wa biashara yenyewe'
Dada Amina Wa Sanga anasema "Usimuamini kila mtu, usimuweke karibu kila mtu. Kuna vitu kaa navyo mwenyewe mpaka vitokee, wengine wangeshakua wamefanya vitu vikubwa, wengine wangekua wameandika vitabu vingi, hawachukui hatua kwasababu wanataka kueleweka. Usilazimishe watu wakuelewe, sio lazima. WE PAMBANA, You're the captain of your own ship.
Dada Amina Wa Sanga anasema "Usimuamini kila mtu, usimuweke karibu kila mtu. Kuna vitu kaa navyo mwenyewe mpaka vitokee, wengine wangeshakua wamefanya vitu vikubwa, wengine wangekua wameandika vitabu vingi, hawachukui hatua kwasababu wanataka kueleweka. Usilazimishe watu wakuelewe, sio lazima. WE PAMBANA, You're the captain of your own ship.
3.
Usiogope kufanya kazi Kwa bidii kutumiza lengo lako yaani
usijionea huruma, unapoweka Malengo yako usijionee huruma, piga kazi usiku na
mchana mpaka uone njia ya kukufanikisha kufikia malengo yako.
4.
Ongeza ufahamu wako (maarifa) kuhusu Malengo
yako, Jitahidi kutafuta Maarifa ya nyongeza kuhusu Malengo yako, hapa soma vitabu na taarifa mbalimbali zinazohusu malengo yako. Tafuta taarifa sahihi kuhusu wazo lako, hakikisha unakuwa mwalimu wa malengo yako kwa utajiri wa taarifa na maarifa uliyonayo.
5.
Weka usimamizi mzuri wa Malengo yako
na ujenga nidhamu ya pesa na matumizi ya muda wako. Ukitaka kufanya vizuri katika kuelekea malengo yako, jitahidi kuweka usisimamizu mzuri, pangilia vizuri ratiba zako na ujenge nidhamu ya kutosha katika kuzifikia ndoto zako.
@alfredmwahalende
@yopocode
@nanenanefestival2018
https://yopocodetanzania.blogspot.comhttps://yopocodetanzania.blogspot.com
nimejifunza kitu muhimu sanaaaaaa
ReplyDeletenimejifunza
ReplyDelete