ZAO LA MUHOGO
UTANGULIZI
Zao la mihogo ni
muhimu . Hata hivyo wakulima
wengi bado wanatumia mbegu za asili ambazo hutoa mavuno kidogo. Jitihada zinafanywa
za kusisitiza matumizi ya aina ya kisasa hususan Kiroba ambayo inaukinzani na ugonjwa wa mihogo uitwao batobato. Faida ya zao hili ni
kwamba hustahmili ukame, mizizi, miti na majani hutumika kwa chakula mbegu na
mboga, pia huweza kukaa ardhini kwa muda mrefu bila kuharibika
AINA ZA MIHOGO
Zipo aina mbali mbali
za mihogo za asili lakini kwa sasa inashauriwa kutumia aina za kisasa ambazo
ni: Kiroba na Msitu Zanzibari kwa sababu hukomaa haraka na kutoa mazao mengi.
Pia Kiroba inaukinzani na ugonjwa wa batobato wa mihogo.
UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba la mihogo ni
vema litayarishwe mapema kwa kukata miti, vichaka kisha tifua vizuri kiasi ya
sm 15 hadi 30. Aidha shamba linaweza kutayarishwa kwa kutumia matuta.
UPANDAJI NA NAFASI ZA
KUPANDIA
Mihogo hupandwa pingili
zilizochaguliwa kutoka katika mimea iliyokomaa vizuri na isiyo na ugonjwa.
Pingili hukatwa kwa kisu kwa urefu wa sm 30 hadi 45 tayari kwa kupelekwa shamba
ili zipandwe. Mihogo
hupandwa kwa nafasi ya sm 120x90 kwenye shamba la sesa na sm 150x75 kwenye shamba
la matuta.
Sio muhimu kutumia
mbolea za kupandia za viwandani isipokuwa iwapo shamba halina rutuba
inashauriwa kutuima samadi kiasi cha tani 4 hadi 5 kwa eka.
PALIZI
Palizi huanza baada ya
wiki mbili toka kupandwa na jembe la mkono hutumika na kurudia mara kwa mara
mpaka mihogo inapokomaa. Hakuna haja ya kupunguza miche kwa sababu hupndwa pingili
moja kwa shina.
MBOLEA ZA KUKUZIA
Mbolea za viwandani
sio muhimu kwa zao la muhogo.
DHIBITI YA WADUDU
Wadudu wanaothiri
mihogo ni mchwa, vidugamba na inashauriwa kutumia dawa aina ya Karate au Decis
kiasi cha cc125 kwa lita 20 za maji.
MAGONJWA
Mihogo huathiriwa
zaidi na ugonjwa wa bato bato kali kwenye majani pamoja na ule wa kuoza mizizi.
Magonjwa haya hukingwa kwa kuanda mbegu ambazo hazina ugonjwa au kutumia aina
ya mihogo yenye ukinzani ambayo ni Kiroba. Pia inshauriwa kutumia kanuni za
kilimo bora ilikupunguza athari ya magonjwa haya.
UKOMAAJI NA UVUNAJI
Mihogo hukomaa baada
ya miezi 12 had 18 kutegemea na aina ya mihogo, hali ya hewa pamoja na
utunzaji. Mihogo iliyokomaa ivunwe kwa kungoa mashina na eka moja iliyotunzwa
vizuri hutoa tani 4
hadi 10.
HIFADHI NA UUZAJI
Mihogo iliyovunwa
humenywa na kukaushwa juan ili ikauke vizuri. Mihogo iliyokaushwa husagwa unga
na kuuzwa au huhifadhiwa kama makopa kwa matumizi ya baadae
Comments
Post a Comment