MAMBO
YA KUFANYA ILI MUDA UKULETEE MAFANIKIO.
Mwalimu Subira
Mlaga
1.
Chagua kitu cha kufanya:Haijarishi
una mipango mingi kiasi gani.Toa vipaumbele katika mipango yako
uliyojipangia.Pasipo kuwa na vipaumbele unaweza tamani kufanya kila kitu ndani
ya muda mmoja.Unapoweka vipaumbele vinakusaidia kujua kitu gani uanze nacho na kitu
gani kimalizie. Na kwa muda gani uwe umekamilisha na kuanza jambo
lingine.Unapochagua ufanye nini na nini usifanye itakusaidia kukomboa muda.
2.
Tenda jambo sahihi kwa muda
sahihi:Kila
jambo lina muda wake.Ili ufanikiwe zaidi ni muhimu kufanya kila jambo kwa
muda sahihi.Mfano wewe unauza duka,muda
wa kuwahudumia wateja wewe upo busy whatsup,instergram,fb unachati,mara kidogo
unasuka nywele dukani ukweli ni kwamba unawapa wakati mgumu wateja wako hata
kama hawatakuambia.Sasa wateja wakikuama utaanza lalamika,kuwa duka la jirani
mchawi kahamisha wateja wako.Kumbe mchawi ni wewe mwenyewe umeshindwa kufanya
jambo sahihi kwa muda sahihi.Ukiwa dukani mteja anategemea akukute upo tayari kumuhudumia
kwa muda sahihi,sasa kama wewe hautajali muda wateja watakuhama.Na watakwenda
huko ambapo muda wao utathaminiwa.Kama haujali muda,mafanikio utaishia
kuyasikia kwa jirani.
3.
Tenga muda wa kutosha katika jambo unalotaka kulifanya:Kuna wakati umefanya uchaguzi
sahihi wa nini kifanyike,ukafanya jambo hilo kwa usahihi lakini umeshindwa
kufanikiwa kwa sababu haukutenga muda wa kutosha.Mafanikio ya kudumu
yanahitaji muda wa kutosha.Na hilo jambo lako lipe muda wa kutosha,usikurupuke
wala usiingilie mipango mingine kabla ya kukamilisha mipango ya
awali.Mfano umeanza kufuga kuku wa mayai
mtaji wa kutosha unao mpaka chenji ina baki.Lakini ufugaji huo usipoupa muda wa
kutosha hautaona mafanikio yoyote.Unapokuwa na muda wa kutosha inakusaidia
kujua vyema lile jambo unalotaka kulifanya,hautalifanya kwa kubahatisha bali
utafanya kwa uhakika.Hata changamoto zijapo utakuwa ngangari na tayari kusonga
mbele.Kila jambo ulifanyalo lipe muda wa kutosha.
4. Yawezekeza muda wako kwenye
ndoto zako:Watu wengi leo hawajafanikiwa na uenda wasifanikiwe kabisa kwa
sababu wamewekeza muda wao kwenye ndoto za wengine na wamesahau
kuziishi,ndoto zao.Mfano wewe ni mwalimu kama mimi una ndoto ya kuwa na chuo
chako,au shule yako.Unapaswa kuweka mipango madhubuti ya kufikia ndoto yako.Ni
kweli umeajiriwa lakini usiterekeze ndoto zako.Tenga muda kwaajili ya ndoto
zako
5.
Kaa mahali sahihi:
Ukifanya
jambo sahihi mahali pasipo sahihi si rahisi kufanikiwa.Ukiwa mahali sahihi kwa
muda usio sahihi hautafanikiwa.Haijalishi umejitoa kwa kiasi gani.Hata kama
wewe ni time keeper kama haupo eneo sahihi utaendelea kupoteza muda.Tafuta eneo
sahihi la wewe kuwepo.Mfano unafanya kazi kama mwalimu,kumbe wewe ulipaswa kuwa
mkandarasi.Unapoendeleakuwa mwalimu hautafanikiwa kwa sababu siyo eneo
lako.Unapokuwa eneo sahihi ni rahisi kufanikiwa.Tafuta na ulijue eneo la
mafanikio yako lipo wapi?Siku utakapolijua hautapishana tena na mafanikio yako.
6.
Jitahidi kubalance muda wako:Natambua
umuhimu wa kuwajibika,pamoja na kuwajibika huko jitahidi kupangalia mambo yako
vizuri na muda wa kutosha wa kuyatekeleza.Ukishajua vipaumbele vyako ni vipi
jitahidi kuvipa muda wa kutosha.Mfano wewe ni mwanamke na una
familia,mfanyakazi,mjasiriamali,na mengine unayafanya ili ufanikiwe unapaswa
kubance muda wako.Muda wa familia usiingiliwe na biashara,muda wa kazi uwe muda
wa kazi.Ukifanya hivyo utafanikiwa kwa sababu kila jambo umelipa muda wake.
Comments
Post a Comment