² MAMBO 13
YANAYOWAFANYA WATU WANABAKI MASKINI.
NA, SUBIRA MLAGA
Sababu
zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli:-
² Kushindwa
kuamua haraka fursa zinapojitokeza kwao,Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni
uongo na utapeli wa mjini
² Kung'ang'ania
kuajiriwa hata kama ajira hiyo hailipi
² Kudhania
unajua sana hivyo huoni jipya la kujifunza
² Kukosa
ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi huu au mwaka huu ntafanya hili au lile.
Lakini mwaka unaisha hujaanza!!!
² Kutokuwa
na ndoto ya kiasi cha pesa unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka. Unataka
shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi? Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi
yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi?
² Kununua
vitu vya bei kubwa sana na visivyo na tija yoyote katika kuongeza kipato chako.
² Kuwaza
kwamba maendeleo yanapatikana uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya
pesa mpaka uwe mzee kama Reginald Mengi vile.
² Kufikiri
eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi.
Ujinga.
² Kuwa na
wategemezi kibao nyumbani kwako wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu
kwa mwezi. Hatari!!
² Kusubiri
siku utakayopata pesa nyingi sana eti ndipo utafanya biashara hii au ile!
Utasubiri sana.
² Kutokuweka
akiba yoyote kwa malengo ya maendeleo ya watoto na wajukuu zao.
² Kufikiria
kuwa kuna siku utapata msaada kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au
washikaji zako. Utangoja sana.
² Kubadilisha
mshahara wako au kipato chako kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo
wenu anakuomba pesa na wewe unampatia.
Comments
Post a Comment