NENO
LA MWAKA
² "Basi
imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo
yasiyoonekana."EBRANIA 11:1.
² Unapokuwa
na imani ina maana unao uhakika wa mambo yote unayoyatarajia yatoke katika
maisha yako.
² Imani
ina sababisha mambo kutokea katika maisha yako, ukiwa na imani haba utapokea
haba katika matarajio yako.
² Ukiondoa
imani ndani ya moyo wako utakaribisha hofu, mashaka na wasiwasi ambayo uvuruga
mipango ya Mungu kwako.Watu wengi wameshindwa kufanikiwa katika mipango yao kwa
sababu ya kukosa imani.
² Kukosa
imani kunamfanya mtu akate tamaa kuyaendea mafaniko yake.
² Mtu
asiye na IMANI katika moyo wake huendeshwa na mitazamo na kilele za watu
wanamzunguka, hujiuliza maswali ya kushindwa na kukatisha tamaa kabla
hajajaribu kufanya jambo.
² Endelea
kumwamini Mungu juu ya ahadi zake maishaini mwako nae atafanya mambo makubwa na
utamshangaa mungu anavyoonekana katika mipango yake kwake.
² Nataka
niseme na wewe unayemwamini MUNGU kuwa ndiyo kimbilio lako ya kwamba huna
sababu ya kuogopa kitu kwa kuwa ahadi ya Mungu kwako ni kukufanikisha kwa kila
jambo.
² UKIWA
NA IMANI UNA UHAKIKA WA KILA JAMBO LA BAADAE.
Comments
Post a Comment