Vijana Tanzania
Na Alfred Mwahalende
Na Alfred Mwahalende
Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania
Janerosa Mafwimbo anasema “Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa
likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani.
Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno
kijana kama ifuatavyo:
1.
Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya
umoja wa Mataifa.
2.
Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka
18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea
ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996
na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia
miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa
miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na
kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi.”
JE,
UJANA NI NINI?
3. Ujana ni hatua ambayo mtu anapitia baada ya
utoto.
4.
Ujana
ni hali ya kuwa na tabia za umri wa ujana ambao ni miaka 18-35.
5.
Ujana
ni kipindi cha makuzi ya mtu kabla ya utu uzima na hatimaye uzee.
6. Ujana ni kipindi kati ya miaka 18-35 hivi
ambapo mtu anakuwa amepevuka na ukomavu wa kiakili na kimwili.
NIKUKUMBESHE MAMBO KUMI NA MBILI (12) MUHIMU UNAYOTAKIWA
KUYAFANYA KATIKA KIPINDI HIKI CHA UJANA WAKO;
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unajijenga kielimu,
imarisha misingi kwenye taaluma mbalimbali yaani elimu ya msingi ya darasani na
elimu ya stadi za maisha ya mtaani. Jijengee Maarifa makubwa yatakayokusaidia kuhamisha
milima yaani changamoto. Pia katika elimu usisahau elimu ya dini, elimu ya
afya, biashara, ujasiriamali na mahusiano.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unapata ardhi au kiwanja
chako na uanze kuweka malengo ya kujenga.
✳ wekeza kwenye chochote unachohisi au unachoona kinaweza
kukuingizia kipato chako, usiogope kuwekeza kwenye fursa ndogo ndogo zinazoweza
kukuingizia kipato.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unaingia kwenye
mahusiano ya kweli na ndoa. Unapofikia ujana hakikisha unajijengea mahusiano
mazuri, unitumie silaha ya ujana kujiingiza katika mahusiano na kila inayemuona
mbele yako.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unakwepa kujiingiza
kwenye starehe zisizokuwa za lazima, achana na tabia za ulevi, matumizi mabaya
ya muda na pesa, kumbuka wakati wa ujana ni wakati wa kukusanya utakachokula
uzeeni.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unafungua akaunti ya
pesa ili uweze kuanza kuweka akiba kwa matumizi ya baadaye.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unajenga uaminifu kwa
kila mtu yaani uaminifu katika ahadi na matendo yako.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unakuwa na marafiki
wenye tija, pia marafiki wanakujenga kiakili na kukusaidia kutimiza kusudi
lako, achana na marafiki wanafiki, wafitini na wenye wivu wa kijinga. Pia
angalia marafiki wanaokutia moyo na kukukosoa pale unapokosea.
✳ katika kipindi hiki cha ujana hakikisha unaanza kufanya mambo
yako kwa malengo. Usifanya mambo bora yaenda, Fanya mipango kwa utuluvi mkubwa
usikurupuke, weka mikakati makini inayoweza kukutoa katika maisha yako.









Edgr
ReplyDeleteNice nitafanyia kaz
ReplyDeleteNice thakyour for adivice
ReplyDelete