Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2018

SAJILI NGO YAKO TANZANIA

SAJILI NGO YAKO TANZANIA Je, unahitaji ‘NGO’? Fahamu utaratibu wa kusajili NGO ni kifupi cha neno Non-Governmental Organization. Kwa Kiswahili neno hili humaanisha shirika lisilo la kiserikali. Kawaida Serikali huwa ina mashirika yake, kwa mfano Shirika  la Bima, Shirika la  Nyumba, Shirika  la Umeme, mashirika ya vyakula n.k.   Tunapozungumzia NGO maana yake ni kuwa ni mashirika ambayo kwa namna yoyote ile Serikali haihusiki na umiliki wake. Ni mashirika ambayo humilikiwa na watu binafsi.  Serikali huweza kushirikiana nayo tu, lakini si kuyamiliki. Taratibu za uanzishaji, usajili na uendeshaji huratibiwa bayana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002. 1. YAPI YAWE MALENGO YA KUANZISHA NGO Malengo makuu ya kuanzisha NGO yawe ni kusaidia makundi au kundi maalum katika jamii. NGO siyo shirika la biashara.  Siyo kampuni ambayo muanzishaji  wake hutarajia kutengeneza faida. NGO ni shirika la hisani. Ni shirika la kujitolea kusaidia makundi jamii. Usi