NA MWANDISHI, SUBIRA MLAGA
KULIJUA KUSUDI.
KULIJUA KUSUDI.
Hakuja
jambo linalofanyika kwa bahati mbaya, kila jambo linalofanyika kuna sababu
inayosababisha lifanyike kwa jinsi unavyoliona.
KUSUDI:Ni
sababu inayofanya mtu,au kitu kuwepo pale kilipo. Mfano kisu unapokuwa nacho
kinalitumikia kusudi la kutengenezwa kwake.Kisu utakitumia kurahisisha shughuli
zako mbalimbali.Pale kisu kinapokupa urahisi wa kazi yako hapo kinatimiza
kusudi la kutengezwa kwake.
💎Binadamu
Mungu alipomuumba alimwekea kusudi ndani yake.Haijarishi unajua au haujui
kusudi la kuumba kwako aina maana kuwa Mungu alikuumba bila ya kusudi.Katika
kitabu cha mwanzo wakati Mungu akimuumba mwanadamu aliweka sababu kwa nini
anamuumba."Mungu akasema,Na tumfanye mtu kwa mfano wetu ,kwa sura yetu;
wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani,na wanyama,na nchi yote pia,na
kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."MWANZO 1:26. Hapa inaonekana
sababu ya kuumbwa mwanadamu kuwa atawale vitu vyote Mungu alivyo viumba.Jiulize
swali na mimi pale ulipo wewe ni mtawala au mtawaliwa??Kama unatawaliwa huo
siyo mpango wa Mungu utawaliwe bali utawale.
AINA
ZA KUSUDI.
kuna
aina kuu 2 za kusudi katika maisha ya mwanadamu.
1. KUSUDI KUU/GENERAL PURPOSE.
Mungu
alipokuumba alikusudia uwe mtawala wa vile alivyoviumba.Mungu anafurahi akiona
una mamlaka .Kuwa na mamlaka hakuishi tu Kuwa na cheo kazi hata kuwa na mamlaka
na kazi za shetani,shetani hasikutawale kwa sababu ukiibwa utawale.
"Lakini nasema ya kuwa mrithi,wakati wote awapo mtoto,hana tofauti na
mtumwa,angawa ni bwana wa yote"GALATIA 4:1.Hata na wewe kama haujui haki
zako utaendelea kutawaliwa kila mahali.
2. KUSUDI MAALUMU/SPECIFIC PURPOSE.
Kuna
kusudi maalum kwa kila mtu mahali popote alipo.Makusudi haya yametofautiana
kutoka mtu moja hadi mwingine:
I)Kusudi
la wito:Wewe mtumishi unayemtumikia Mungu katika huduma yoyote je unajua sababu
ya wewe kuwa mbele za Mungu??Mungu hajakuita tuu ana sababu na wewe katika
ualimu wako,uchungaji wako,uimbaji wako n.k.Kusudi la Mungu kukuita katika wito
uliona ni ili umuwakilishe yeye na siyo kujionyesha wewe."Mtu na atuhesabu
hivi,kuwa tu watumishi wa Kristo,na mawakili wa siri za Mungu". 1KORINTO
4:1
II)Kusudi
katika ndoa/familia:Katika familia uliyopo Mungu ana kusudi na wewe,na Katika
ndoa uliyofunga Mungu anakusudi nayo.Yamkini kutokana na mapito na taabu
ukaanza kumlamu Mungu Kwann mume Wang hivi,watoto n.k pamoja na hayo Mungu bado anakusudi
anakusudiapo weweo.Ukilijua kusudi la wewe kuwa katika familia hiyo hautapata shida. hautapataII)Kwanasumbua
FAIDA
ZA KULIJUA KUSUDI.
1. Utafanya bidii ufikie ndoto/Hatima
yako.Unapolijua kusudi la kuubwa kwako hiyo ni dira inayoonyesha uelekeo wa
ukuu wako.
2. kilijua kusudi hautaambatana na
kila mtu. Unapolijua kusudi ni sawa na mama mjamzito ambaye anajichunga baadhi
ya mambo
asifanye ili mtoto aliyembeba awe salama.Na wewe unapolijua kusudi
hautaambatana na kila mtu ili ufike kwenye kiilele chako.Kuna watu ukiambatana
nao wanaua na kupoteza muda wako.Angalia sana nani unaambatana nae.
3. Ukilijua kusudi la kuumbwa kwako
utafurahia
maisha.Furaha ya kweli katika maisha ya mtu inapatikana kwenye kusudi.Ili
ufirahie maisha haina haja ya kuumiza kichwa muombe Mungu akupe kulijua kusudi
la kuumbwa kwako.Usimtegemee mtu akufurahishe,tumikia kusudi la kuubwa kwako
ufurahie maisha.
4. Hautafanya
kila kitu.Ukilijua kusudi litakuongoza ufanye nini na utajizuia usifanye kile
kilicho kinyume cha kusudi lako.
5. Kusudi litakutofautisha na
wengine.Kuna watu ni ngumu
kuwatofautisha kwa sababu wana copy na kupaste vya watu.Watu hawajawahi kuishi maisha yao.Hata bidhaa utofautiana
kutokana na matumizi.Tafuta kujua kusudi.
Comments
Post a Comment