Zig Ziglar aliwahi kusema kwamba Ukitaka kufanikiwa saidia wengine kufanikiwa na wewe utafanikiwa na mimi nakwambia kwamba Ukitaka kuangaza dunia nzima kuwa mshuma ambao unawasha mishumaa mingine sio kuizima ya wengine.Ukiwa na nafsi ya kutaka mshuma wako tu kuangaza dunia nzima hautafika sehemu yoyote itazima tu na wala hautakuwa na nguvu ya kuangaza mbali.Watu hawatasema kwamba huyu mtu alishawahi kuwasha mshumaa wake hata siku moja.
Naomba nikueleweshe kitu kuhusu huu mshumaa, mishumaa nimeivisha taswira ya MAARIFA YAKO, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI ZAKO ambao wanakuzunguka.
1. Mshumaa Ni watoto wako Kama hutaweza kuwapa maarifa ya dunia ambayo umeweza kuyaona na kuyatatua hata siku ukiwa haupo hawatatambua uwepo wako. Ila Kama utaweza kukaa chini na kuzungumza nao pindi usipokiwepo watajua kuwa baba au mama walitusaidia kwelii na watu watasema kwelii wale watoto ni wa flani. Watoto wanachohitaji ni zawadi ambayo unayo ndani yako kama ni maarifa basi hauna budi kuwapa pia.
Unapotumia mshumaa wako kuwasha ya wengine unaongeza nguvu ya dunia kuondokana na giza nene, na unazidi kuonesha kwamba kumbe peke yako hauwezi kuangaza dunia nzima bila kusaidia wengine kuwasha yao, mshumaa wako ukiwa chanzo cha mishumaa mingine kuwaka utatengeneza dhana ya kwamba bila kusaidia mwingine mshumaa wako sio kitu. Unaposaidia wengine unasaidia hata ambao huwajui kusaidia wasaidie wale ambao huwajui mishumaa yako kuwasha. Kumbuka kwamba hata ikizima bado ya wengine itasaidia kuwasha ya wenzao.
2. Mishumaa hii ni rafiki zako jinsi unavowasaidia kuwapa maarifa tofauti na kuweza kuwasaidia kimawazo. Unaposaidia marafiki zako ni sawa na kujisaidia mwenyewe ila usiposaidia marafiki haujajisaidia mwenyewe. Vipi mshumaa wako ukizima nani atauwasha ukiwa katika safari yako ya mafanikio wakati unaoongozana nao hukutaka kuwasha hata wa mmojawapo?? Kuwa makini.
Mpenzi msomaji wa makala hii katika mtandao wa YOPOCODE TANZANIA napenda kukwambia kwamba ukiweka MSHUMAA wako katika kilele utaangaza na utaleta maana yake ya kuangaza na kuweka kileleni maana taifa zima litanufaika, hapa namaanisha tuzidi kujinoa na kitu kionekane na kizidi kuleta manufaa katika jamii zetu.Ila unapoficha MSHUMAA wako chini ya uvungu wa kitanda haitakuwa na maana ya kuuwasha. hapa namaanisha kwamba unapoamua kufanya jambo la kusaidia jamii yako usilifiche kwa kuogopa watu, ila litoe limulike na wengine na kuwasha mishumaa ya wengine hapo utakuwa umeweka tafsiri maalumu ya mshumaa wako.
Kwa wewe ambae unahitaji kupata mwongozo katika shughuli zako za biashara maendeleo binafsi na mahusiano napenda kukukaribisha katika program ya AKILI YA USHINDI kupata maelezo ya kuwa mwanachana bonyeza https://akiliyaushindi.com/ nenda katika menu sehemu KUHUSU AKILI YA USHINDI.
Ulikuwa nami;
Coach Lazaro Samwel
0753616584/0653386586
Email; lazarosamweli41@gmail.com
NASHUKURU SANA MR LAZARO SAMWELI KWA MAKALA NZURI JUU YA KUWASHA MSHUMAA
ReplyDeleteKaribu sana kiongozi
Delete