HAKUNA
LISILOWEZEKANA KWA MUNGU.
MWALIMU SUBIRA MLAGA
💦Kuna mambo kwa
akili za kinadamu yanashindikana, akili ya kibinadamu inafika mwisho. Pale
akili yako inapofika mwisho hapo ndio mwanzo wa akili za Mungu. "Maana
mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa
maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi
juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."ISAYA
55:8_9.
💎Yamkini kuna
hali,majaribu na mapito mbalimbali unapitia sasa,watu wako wa karibu
wamekukatisha tamaa kuwa hilo jaribu/pito/shida yako haiwezekani tena.Labda ni
dokta kutokana na vipimo akakuvunja moyo kuwa hutapona tena,hautazaa tena na
n.k.
Leo nakumbia habari za Mungu mwenye uweza wa mambo yote hakuna jambo lolote
la kumshinda yeye.Ukimwamini sasa atafanya yasiyowezekana katika macho ya wanadamu
kuwezekana na kuwashangaza
waliokubeza.
Haikuwa rahisi kwa ajuza Sara kuamini katika umri wa miaka tisini
matiti yake yangenyonyesha mtoto wa kumza.
Lakini tunaona Mungu akimtokea Sara
na kumpa mtoto katika umri mkubwa ambapo wanasayansi akili zao zinagoma katika
umri mkubwa vile mwanamke kuzaa mtoto.
"Ndipo Ibrahim akaanguka kifudifudi
akacheka,akasema moyoni,
Je!Mtu wa umri wa miaka mia,kwake atazaliwa mtoto?Naye
Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?"MWANZO 17:17,"BWANA
akamwambia Ibrahimu,Mbona Sara amecheka akisema,Mimi kweli nitazaa mwana,nami
ni mzee?Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?..."MWANZO
18:13_14.
Hakika hakuna la kumshinda Bwana.Hata kama Ibrahimu na Sara
walishajikatia tamaa tunaona kwa majira yaliyokubarika Isaka anazaliwa.
💎Unaona mambo magumu
hayawezekani kwa sababu haujampa Mungu nafasi ya kudhihirisha uweza wake katika
maisha yako.
"Tazama mimibni BWANA,Mungu wa wote wenye mwili;je !Kuna neno
gumu lolote nisiloliweza?YEREMIA 32:27.Mungu anatushanga kuwa hatumtegemei na
kumwamimi kwa 💯🐥%kuwa yeye
anaweza.Anza leo kuwamwani Mungu yeye anaweza na hakuna la kumshinda.
💎Katika mapango na
malengo yako uliyonayo nakusihi usiwaze na hofu kuwa itakuwaje?Ni kweli siku
zimeenda na miezi imesogea labda haujapata kazi,mke,mume n.k. Namutia moyo hata
hayo usipoyaona kwako haina maana kuwa Mungu hawezi tena kukutendea kwa sababu
yeye ni Mungu wa wote wenye mwili hivyo na la kwako analiweza pia."Kwa
kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu"LUKA 1:37
KWA
MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.
Amina,,barikiwa Sanaa mtumishi
ReplyDelete