KANUNI ZA KILIMO BORA
NA MWANDISHI WETU
Misingi na kanuni za kilimo bora.
Neno Msingi lina maana
ya mwanzo wa kufanya shughuli yeyote inayokusudiwa ili kuweza kufikia malengo.
kwa hiyo katika kilimo ipo misingi muhimu ifuatayo:
Kuwa na mipango
thabiti inayotekelezeka kabla ya kuanza kufanya kazi yeyote ya maendeleo ni vyema, kuweka mpango kazi ili iwe dira wakati wa utekelezaji. Hivyo wakulima
wanatakiwa waweke malengo yao ya kilimo kwa kuangalia Usalama wa chakula na
kipato
Mipango bora.
Ni mipango ambayo
inamsaidia mkulima kupata chakula cha kutosha na fedha ili kuondokana na umaskini.
Mipango inatakiwa iwe shirikishi kwa kuona kuwa wakulima wana shiriki katika
kupanga, kutekeleza, kufuatilia pamoja
na kutathmini.
Kuchagua eneo linalofaa kwa kilimo.
Kwa kuwa kilimo ni
kazi ya kisayansi, eneo linalofaa kwa kilimo liwe na rutuba, mteremko wa
wastani, liwe sehemu inayopitika ili kurahisisha usafirishaji wa mazao na
pembejeo wakati wa uzalishaji.
Uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu.
Ni muhimu mkulima
kujiwekea kumbukumbu za uzalishaji, mapato na faida ili kupima mafanikio ya
kazi yake.
Matumizi ya kanuni za kilimo bora.
Neno kanuni lina maana
ya utaratibu wa kisanyansi uliofanyiwa majaribio kwa muda mrefu na ambao
umekubalika utumike wakati wa uzalishaji wa mazao.
Kanuni za kilimo bora
Kutayarisha
shamba mapema Kwa kutifua.
Kupanda
mbegu bora kwa nafasi inayostahili.
Kupunguzia
miche na kubakiza inayoshauriwa
Palilia
mapema-si zaidi ya wiki mbili baada ya kuota mazao..Plazi ziwe mbili au zaidi.
Weka
mbolea ya kukuzia mara baada ya palizi.
Weka
dawa ya kuua wadudu wa mimea.
Linda
mazao yako na Wanyama waharibifu Vuna mazao yako baada ya kukomaa vizuri.
Sindika
mazao yako na kuyaweka kwenye mifuko inayoingiza hewa baada ya kuweka dawa.
Hifadhi
mazao mahali pazuri pasipo vuja au kufikiwa na wanyama waharibifu.( Panya)
Comments
Post a Comment