NJIA NGUMU; Kurasa 12 kitabu cha kwanza cha mwaka mpya HATUA kubwa 2018/19
Kitabu; WAR of SELF, The 7 Weapons of Self Mastery by Ramman Sheehan Turner ( Vita ya Binafsi, Silaha 7 za Ubobezi binafsi ) 60 ~ 72
SILAHA ya 3; Ona Ukweli katika udanganyifu na wewe ni sehemu ya Ulimwengu mzima ona mahusiano ya uwepo wako na watu na mazingira asilia yanayokuzunguka.
HATUA ya KUCHUKUA; Ona uhalisia ulivyo na kila mara jua u sehemu ya ulimwengu na acha kujidanganya mwenyewe.
Rafiki ukweli ni silaha yetu ya tatu ambayo itaondosha ugomvi ndani yako na kukuweka huru katika maisha yako. Pale unapoondoa ukweli basi unaangukia kujidanganya na ukijidanganya unajiweka katika kifungo. Je uko tayari kuishi maisha yako katika kifungo ikiwa waweza kuwa huru kwa kusema kweli au kujua kweli?. au ukweli wa mambo. Basi moja ya jambo ambalo watu wanajidanganya ni kujiona wao si sehemu katika ulimwengu, wanaona kuchukua au kutochukua hatua kwao hakuna athari katika Dunia. Si kweli kuwa athari yako haipo ipo ikiwa utaona kuwa u sehemu katika ulimwengu tunaoishi.
Dunia na mazingira yake yako katika mahusiano makubwa na mahusiano haya yanashuka hadi ngazi ya uwepo wa viumbe wake namna kuishi kwao kulivyo na mahusiano yanayoweza kutoa athari toka chini hadi juu kabisa ngazi ya mahusiano ya watu wa mataifa mbalimbali. Uwepo wa teknolojia hasa eneo la mawasiliano ndio umefanya eneo moja katika Dunia kuweza kufanya athari ionekane eneo lingine pia na hata ulimwengu mzima ( ona ilivyo Simu janja ujifunze kitu ) . Mfano katika habari moja ya eneo lingine yaweza kuathiri maeneo mengi ya Dunia sababu tu sehemu sasa ya umoja katika Dunia.
Je kitu gani huwa unakiona katika kila jambo unalolisikia katika taswira uonayo na jinsi uhalisia utakavyokuwa ukiingia kufanya hicho kitu au kikikupata ?. Kama unapuuza uhalisia wa mambo utakavyoenda kuwa basi utajitengenezea ugumu mwenyewe. Ili kupata amani na furaha katika kuishi kwako basi ni muhimu sana kuona mambo kama yalivyo katika maisha yako. Ona mambo kama yanavyotakwa kuonwa na uone jinsi ulivyo nawe ni sehemu ya jamii katika ulimwengu tunaoishi. Hatua hii ni silaha kwako ya kuondoa ukinzani ndani yako kila siku za kuishi kwako.
Endelea kufuatilia kurasa hizi 12 kila siku kuna hatua utavuka ya HATUA KUBWA kwa maisha yako ya kila siku.
Mchambuzi mwanafunzi eneo la Uhalisia wa Maisha
Mwanafunzi wa Kilingala
Mchambuzi wa vitabu
Mwandishi wa vitabu
Mfanyabiashara wa maarifa/taarifa ( INFOPRENEUR )
Malenga wa Ubena
© Raymond Nusura Mgeni 2018
+255 676 559 211 au +255 766 461 571
raymondpoet@yahoo.com
SAFARI ya V 450, 2023 Hatua moja huanzisha safari.
Mafanikio ni kujitoa na maisha ki uhalisia ni mchezo wa akili kubwa. Nimejitoa kulipia gharama kufikia HATUA KUBWA.

Comments
Post a Comment