Skip to main content

HOW TO BE A COMEDY WRITER

JAMII 100; Vichekesho na Ucheshi katika sura ya biashara ya kale iloanza kukua toka zamani na itazidi kukua kadri muda uendavyo.

Mambo ya kuzingatia; Vichekesho ni fursa kubwa kibiashara na imetengeneza wafuasi wengi kwa maana kucheka ni moja ya tiba na kuipa akili utulivu.

Kitabu; HOW TO BE A COMEDY WRITER, Secrets from the inside by Marc Blake ( Namna ya kuwa mwandishi wa vichekesho, siri kutoka ndani )

Vitimbi, Mizengwe, Futuhi, Joti Tv, Ze komedi, Cheka tu, Churchill show, Omondi, Mc Pilipili ni moja ya picha kubwa kwa namna gani vichekesho au ucheshi ulivyofanya maisha ya watu wengi wapende kufuatilia na kufurahi wasikiapo au wakitazama. Kucheka kuna raha yake na tunaona namna hata mwili huwa katika utulivu pale ambapo unakutana na kitu cha kukufanya ucheke. Je umewahi jiuliza kwanini watu hucheka ?, nini kinachowasukuma watu walipe na hata kuhudhuria majukwaa ya ucheshi. Inawezakana ikawa ni zoezi gumu kuelezea kwa maneno lakini ucheshi au vichekesho vinakufanya ujisikie vizuri hata kama hukuwa vizuri. Katika vichekesho unaona hamasa mpya tena na unapata nguvu katika maisha. Nini mwandishi Marc Blake anataka kusema katika hiki kitabu ?. Twende pamoja kujifunza msingi wa uandishi wa vichekesho.

Kama ambavyo tumeona toka kale huko kale ya Ugiriki ucheshi ulianza na umeandikwa katika kazi nyingi za fasihi. Tunaona ilivyo Duniani kote namna vichekesho vilisaidia sana kurejeza matumaini ya watu ambao walipatwa matukio ya kusikitisha katika maisha yao. Tunaona namna Charlie Chaplain moja ya waliowahi kuwepo Duniani bingwa wa uchekeshaji wa vichekesho vya matendo bila sauti alivyorejeza watu furaha baada ya matukio makubwa ya vita ya pili ya dunia iloishia mwaka 1945. Kumekuwa na mwendelezo wa watu wanaozaliwa na wana ucheshi ndani walivyoendelea kuikuza fani ya uchekeshaji kama kazi na biashara na ikawapa utajiri mkubwa kama mchekeshaji Mr Bean. Huu ni uchache wa namna ucheshi ambavyo ni biashara kubwa kwa karne zote ambapo hitaji la kuwa na furaha au kucheka ni hitaji muhimu kwa maisha ya kila siku.

Je wajua kuwa wewe ni kiumbe pekee mwenye uwezo wa kucheka na hali ya kucheka ilianza zamani toka siku ulipokuja Duniani. Ona jinsi ambavyo maisha ya watu yanavyopendeza sababu ya vicheko vyao. Na hata utakuwa umewahi kusikia kucheka ni tiba na cheka uongeze siku za kuishi. Kauli hii ina ukweli kwa mlengo huu kuwa maisha ya uchungu, huzuni yanapelekea magonjwa na hii ikasababisha kufupisha maisha yako. Cheka mara kwa mara kila upatapo nafasi hiyo maana ni tiba nafuu ya maisha yenye akili tulivu.

Kama kuna kipaji ndani yako cha kuchekesha basi hiki kitabu usiache kukisoma au kufuatilia kurasa zake ili ujinoe zaidi na zaidi. Watu wakati mwingine wanakosa kunoa fani hii ya kuchekesha sababu ya kukosa baadhi ya maarifa ambayo yataweka msingi bora wa kuwa mchekeshaji hodari na ikawa kazi yako na ukaongeza thamani kwa maisha ya watu wanaokuzunguka. Twendelee kuwa pamoja ukiwa unafuatilia nini kimeandikwa katika kitabu hiki kikitoa mwongozo wa uandishi wa vichekesho.

Mchambuzi mwanafunzi eneo la Uhalisia wa Maisha
Mwanafunzi wa Kilingala 
Mchambuzi wa vitabu
Mwandishi wa vitabu
Mfanyabiashara wa maarifa/taarifa ( INFOPRENEUR )
Malenga wa Ubena
© Raymond Nusura Mgeni 2018
+255 676 559 211 au +255 766 461 571
raymondpoet@yahoo.com

SAFARI ya V 450, 2023 Hatua moja huanzisha safari.

Mafanikio ni kujitoa na maisha ki uhalisia ni mchezo wa akili kubwa. Nimejitoa kulipia gharama kufikia HATUA KUBWA.

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3. ...

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kuto...