Skip to main content

MAMBO YA YANAYOZUIA MABADILIKO

MAMBO YA YANAYOZUIA MABADILIKO

Kama wewe ni mzazi na una mtoto lakini kila mwaka mtoto wako hakui. Kila mwaka yupo vile vile, mzazi lazima achukue hatua ya kujiuliza kwa nini? Kama hajiulizi na kuchukua hatua basi ni wazi kwamba mtoto ataendelea kutokukua kabisa.

Ndivyo ilivyo katika ndoto za maisha yetu, inawezekana kila mwaka unapanga malengo lakini hakuna mabadiliko katika maisha yako. Kila mwaka upo pale pale, ni muhimu kuchukua hatua na kujua ukubwa wa tatizo na uamue kubadilika katika maisha yako.

Mambo yanayochangia kutokukua wa watu wengi ni kama ifuatavyo:

1. Kusikiliza maneno ya watu na sio kuamua hatima za maisha yao. Wapo watu wanasilikiza zaidi watu na sio kutengeneza hatima zao. Hata kama anapata wazo la biashara atajiuliza kwanza kwa watu kuhusu hiyo biashara akiambiwa tu hawezi basi anaishia hapo.

2. Hofu, watu wengi wanahofu ya mambo ambayo yanaweza kutokea kutokana na mabadiliko. Hivyo kutokana na hali hiyo watu wengi huamua kutokubadilika.

Unataka kutimiza ndoto za maisha yako, jifunze kwa watu waliobadilika na kuchukua hatua katika maisha yao. Usikubali kuwaachia watu maisha yako, lazima uongoze maisha yao. Wewe ni dereva wa maisha yako.

Karibu katika Badilika Kampeni tarehe 16.03.2019 kiingilio 10,000.00. Tel 255 652 067 614.

Badilika Sasa Initiative
Vareliano Ulrick Mtundu@2018

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana kama uta

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3.     Ujana ni hatua ambayo mtu anapi