ENDELEA KULIPA GHARAMA ZA KUTIMIZA NDOTO ZAKO
Kila ukitazama ndoto ambazo umetimiza ni jambo gani linakujia katika tafakari yako?
Najua yapo mambo mengi ambayo unakumbuka, jinsi ulivyopambana kuhakikisha unapata hicho ulichokipata. Kuna gharama ulilipa na kwa baadhi ya watu walikuona kana kwamba unacheza. Ndivyo ilivyo, unapojua kile unachokitaka usisubiri watu waseme kuwa ni wazo zuri bali wewe jiamini kuwa hiki ninachokifanya ni sahihi na nitapata matokeo chanya.
Jambo lolote zuri kwenye maisha hupatikana kwa kupambana zaidi.
Najua Januari 2018 ulijipangia malengo ya kutekeleza mwaka huu. Lakini kila ukiangalia kwenye daftari lako huoni chochote ambacho umefanya au umepambana lakini hakuna matokeo uliyotarajia kupata.
Unapoona kuwa hujatimiza malengo yako, ni nini unafanya? Unakata tamaa? Hapana ni kujifunza tu mahali ulipokosea ili kuandika historia mpya kwenye maisha yako.
1. Usiichoke safari ya maisha yako
2. Endelea kujifunza kwani hakuna jambo linaloshindikana
3.Endelea kulipa gharama, usikate tamaa.
4. Endelea kuamini kuwa ipo siku utapata unachohitaji kwenye maisha yako.
5. Usiache kuchukua hatua katika safari ya maisha yako.
Badilika Sasa Initiative
Vareliano Ulrick Mtundu@2018

Comments
Post a Comment