KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA YAANZA
RASIMI JIJINI DAR ES SALAAM.
☑Yopocode kwa
kushirikina na Mabalozi wa kampeni ya Binti Amka Tanzania wameanza rasimi
kampeni katika shule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo katika Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam.
☑Akizungumza kwa
niaba ya shirika la vijana Tanzania la YOPOCODE, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu
Alfred Sostern Mwahalende amekuwa na haya ya kusema"kampeni ya Binti Amka
Tanzania inalenga kumsaidia mtoto wa kike nchini kufika ndoto yake na malengo yake kielimu,
kiuchumi na kiuongozi na katika hili pia tutalenga kupambana na masuala ya
mimba na ndoa za utotoni ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakichangia katika
kumkwamisha mtoto wa kike kufikia malengo
yake.Tumeanza na shule za misingi katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Jijini Dar Es Salaam huku tukifanya juhudi katika halmashauri zingine na
mikoa mingine ambayo tayari tumeanza maandalizi ya kuzindua kampeni yetu"
Katika kuhakikisha tunafikia lengo la
kampeni hii, tumependekeza kuwasilisha mada zifuatazo, Nafasi ya elimu kwa
mtoto wa kike,Mbinu za kutimiza malengo yako, Thamani ya mtoto wa kike katika
jamii, Kulijua Kusudi na Kutimiza Ndoto Yako,Nafasi ya mtoto wa kike katika
maendeleo, Binti na Uongozi Katika Karne hii,Fursa zilizopo kwa mabinti katika
nyanja za kimaisha,Athari ya mimba na ndoa za utotoni, Umuhimu wa kujua sera na
sheria kwa mtoto wa kike,Nguvu na thamani ya kipaji, Elimu ya afya ya uzazi na
maumbukizi ya ukimwi,Malengo endelevu ya dunia (SDGs).
Aidha kwa upande wake mkuu wa shule ya
msingi ya Mnazi Mmoja Mwalimu Abdulaziz amepongeza timu ya mabalozi na shirika
kuanzisha kampeni hii ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa watoto wa jinsia zote
ususani wa kike kujengewa uwezo wa kujitambua, kujiamini, kusimamia malengo
yao,kujithamini na kuweka mikakati ya kuzifika ndoto zao.Ikumbukwe kama iliyo
kwa watoto wa kiume pia watoto wa kike wana ndoto zao, hivyo ni jukumu la
mabalozi wa kampeni ya binti amka Tanzania kuhakikisha wanasimama kideta
kumkomboa mtoto wa kike.
Comments
Post a Comment