Skip to main content

SAJILI NGO YAKO TANZANIA

SAJILI NGO YAKO TANZANIA


Je, unahitaji ‘NGO’? Fahamu utaratibu wa kusajili


NGO ni kifupi cha neno Non-Governmental Organization. Kwa Kiswahili neno hili humaanisha shirika lisilo la kiserikali. Kawaida Serikali huwa ina mashirika yake, kwa mfano Shirika  la Bima, Shirika la  Nyumba, Shirika  la Umeme, mashirika ya vyakula n.k.  
Tunapozungumzia NGO maana yake ni kuwa ni mashirika ambayo kwa namna yoyote ile Serikali haihusiki na umiliki wake. Ni mashirika ambayo humilikiwa na watu binafsi.  Serikali huweza kushirikiana nayo tu, lakini si kuyamiliki.
Taratibu za uanzishaji, usajili na uendeshaji huratibiwa bayana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002.

1. YAPI YAWE MALENGO YA KUANZISHA NGO
Malengo makuu ya kuanzisha NGO yawe ni kusaidia makundi au kundi maalum katika jamii. NGO siyo shirika la biashara.  Siyo kampuni ambayo muanzishaji  wake hutarajia kutengeneza faida. NGO ni shirika la hisani. Ni shirika la kujitolea kusaidia makundi jamii. Usitarajie kuanzisha NGO kwa ajili ya kutengeneza faida ya fedha. 

2. MGAWANYO WA USAJILI WA NGO
Usajili wa NGO umegawanyika katika makundi makuu manne. Kwa mujibu wa sheria, mgawanyo huu umelenga maeneo ya kijiografia. Hata hivyo, ada za usajili na mambo mengine muhimu katika usajili hutegemea mgawanyo huu.
Kwanza,  kuna mgawanyo wa usajili wa ngazi ya wilaya. Usajili wa aina hii huiwezesha NGO kufanya shughuli zake ndani ya mipaka ya wilaya.  Husajiliwa hapo hapo wilayani na hufanya kazi zake ndani ya mipaka hiyo.
Pili, usajili ngazi ya mkoa. Huu huhusisha usajili ngazi ya mkoa na mipaka ya kazi itakuwa ni ndani ya mkoa husika. 
Tatu, usajili ngazi ya Taifa ambao hufanyika makao makuu na mipaka ya kazi ni Taifa zima. 
Nne, ni usajili ngazi ya kimataifa ambao huiwezesha NGO kufanya kazi zake katika taifa zaidi ya moja.

3. WAPI UKASAJILI NGO
Kwa ngazi ya wilaya nenda makao makuu ya wilaya yako, na ulizia afisa maendeleo ya jamii.  Hawa ndiyo wanaohusika na usajili. Hali kadhalika, ngazi ya mkoa utaenda makao makuu ya mkoa wako ndipo usajili utakapofanyika.
Aidha, kwa ngazi ya Taifa usajili hufanyika makao makuu ya wizara kwa msajili wa NGO. Kwa sasa wizara husika ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Wasajili wa ngazi zote hupata mamlaka ya kusajili kutoka kifungu cha 22(1) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

4. VITU GANI VINATAKIWA KATIKA USAJILI
(a) Katiba ya NGO. Hizi hutakiwa nakala tatu zilizojaladiwa (binding).
(b) Maelezo binafsi ya viongozi watatu wa NGO. Mwenyekiti, Katibu na Mhazini.  Maelezo binafsi ni wasifu (CV) pamoja na picha mbili za kila mmoja.
(c) Muhtasari wa kikao cha kuanzishwa kwa NGO ukienda sambamba na majina na sahihi za waanzilishi.
(d) Fomu ya maombi ya usajili iliyojazwa (NGO Form No. 1). Hii hupatikana kwa msajili. Itatakiwa kubandikwa ushuru wa stempu wa Sh 1,500.
(e) Barua ya utambulisho kutoka kwa afisa maendeleo ya jamii wa wilaya, mkoa husika.
(f) Taarifa nyingine yoyote ambayo msajili anaweza kuomba kutoka kwako.

https://yopocodetanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3. ...

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kuto...