KUHUSU KITABU CHA DIRA YA KIJANA TANZANIA
Ni kitabu pekee kilichobeba elimu stahiki ya stadi za maisha kwa vijana
na chenye ubora wa hali ya juu kinachochambua na kutoa dira ya safari ya maisha
ya kijana na miongozo inayotoa ramani ya kumsaidia kijana kujisimamia mwenyewe na kujiajiri kwa kutumia fursa mbalimbali za ujasiriamali zilizopo
kama vile uwekezaji katika sekta ya
viwanda, kilimo biashara, ufugaji wa kisasa, madini, biashara ndogo
ndogo, za kati na kubwa zilizopo katika jamii na kuweza kuendesha shughuli za
uzalishaji mali na maisha yao bila kutegemea usimamizi kutoka kwa mtu mwingine
( kuajiriwa).
Kitabu hiki ni chachu ya mabadiliko chanya kwa vijana na kinatoa hamasa
na kuwachochea vijana kushiriki katika
harakati za kuleta maendeleo katika jamii zao na kukubali mabadiliko ya kisera na kuacha
kukaa vijiweni kulia na kulalamika juu ya hali ngumu ya kimaisha (vyuma
vimekaza) na ukosefu wa ajira katika sekta za serikali na mashirika binafsi na
badala yake washiriki kikamilifu katika zoezi la
kuinua uchumi wao na uchumi
wa nchi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla Wake.
Dhima ya kitabu hiki ni kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uwezo wa
kujitambua, kujiamini, kujithamini, kuthubutu, kujitegemea kifkira na kutumia
rasilimali zinazo wazunguka na fursa mbalimbali zinazopatikana katika maeneo
yao kama ardhi, vyanzo vya nishati, mito, misitu, madini, nguvu kazi na elimu
kwa lengo la kuleta maendeleo yao binafsi na ya jamii zao.
Kutokutambua thamani ya kijana katika Taifa au jamii ni
kushindwa kutambua mchango wake katika mapambano dhidi
ya harakati za kuleta maendeleo chanya katika taifa. Taifa lolote duniani haliwezi kukua na kuwa imara kiuchumi,
kisiasa, kitamaduni na kijamii bila kuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa Dira
itakayotoa hamasa ya kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya
changamoto zinazolikibili taifa lao kama
njaa, vita, umaskini, maradhi, uhaba
wa ajira, uwekezaji duni, kukosekana kwa nguvu kazi, elimu duni na ugumu wa maisha. Kwa hiyo
kitabu hiki pekee ni nguzo imara ya dira ya kijana Tanzania.
KUHUSU WAANDISHI
Hiki ni kitabu cha kwanza kwa ubora duniani kilichoandikwa kwa ustadi wa
hali ya juu na waandishi vijana kutoka katika taaluma na fani mbalimbali
zinazokidhi Nyanja zote za maisha ya binadamu kama Sanaa na Utamaduni, elimu ya
ugunduzi wa vipaji na ubunifu, Sayansi ya Siasa, Biashara, Uchumi, Uongozi,
Dini, Uandisi katika Idara ya Sayansi ya Komputa, Uandishi wa habari,
utangazaji na mawasiliano, Ujasiriamali, Ualimu wa taaluma na Tehama na ustawi
na maendeleo ya jamii.
Waandishi washiriki wa kitabu cha dira ya kijana ni Alfred Mwahalende,
Adabert Chenche, Joas Yunus Buyungu (Jyb), Janerosa Mafwimbo, Hellen Mtui,
Gasper Chacha,Jacob Mushi, Lazaro Samwel, Filbert Nyoni, Innocent Laizer,
Angesta Nathanael, Deogratus Kessy,Mohammed Ismail Rwabukoba, Daniel Rwihula,
Subira Mlaga, Nabe Rodrick Na Daktari Raymond Mgeni
Nimefurahi kuona mmeshirikiana vijana wengi sana, hii inaashiria kupevuka kwa fikra za viajana wa kiafrika. Ushirikiano ukiwepo Afrika inaweza kuwa imara tena. Natarajia kazi nzuri kutoka kwenu makamanda.
ReplyDelete