Skip to main content

FALSAFA YA VIJANA NI TAIFA LA KESHO

TUMEWANYIMA NAFASI  YA UONGOZI VIJANA KUTOKANA NA FALSAFA POTOFU JUU YA VIJANA ISEMAYO’KIJANA NI TAIFA LA KESHO’ HUKU TUKISAHAU MCHANGO WAO
Mwandishi,Alfred mwahalende 
. Kutokutambua umuhimu wa kijana katika Taifa au jamii ni kushindwa kutambua mchango wa makundi yaliyopo katika jamii. Taifa lolote Duniani haliwezi kukua na kuwa imara kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na kijamii bila makundi yote ya jamii kushirikishwa kikamilifu katika mapambano dhidi ya  changamoto zinazolikibili taifa hilo kama njaa, vita, umaskini, maradhi, elimu duni na ugumu wa maisha.                                                                                    
Ni ukweli usiopingika na uliodhahiri kwamba maendeleo ya jamii zetu kwa asilimia kubwa  yanachangiwa na nguvu na maarifa ya vijana. Hivyo jamii isiyotambua umuhimu wa kijana imekufa na haiwezi kujikwamua kufikia mipango thabiti.vijana wanapaswa kushirikishwa katika harakati za kujikomboa kikamilifu na kutumia fursa zilizopo kutatua matatizo yanayoikabili jamii yao.                                                                                                                                           
 Hali kadhalika  katika ulimwengu huu wa sasa,asilimia kubwa ni vijana ambao kimsingi ndio wanaopaswa kuwa viongozi wa leo na kesho na nguvu yao inahitajika sana katika jamii zetu kutokana  na mchango wao mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo .Hivyo basi, vijana ni kundi kubwa na rasilimali muhimu katika kuleta mabadiliko.                                                           
 Falsafa ya “vijana Taifa la kesho” imekuwa ikisemwa mara nyingi ambayo  kwa matazamo wangu ni  upotoshaji mkubwa ukilinganisha na ukweli wa mambo,  licha ya kuwa kauli yenyewe sio ngeni katika masikio ya jamii, kwani imekuwa ikijirudia mara kwa mara katika misemo mbalimbali.  Kuna juhudi kadha wa kadha zimefanyika na wanaharakati mbalimbali wa masuala ya vijana katika kuipinga falsafa hiyo na kuonyesha falsafa mbadala katika kuweka mambo sawa na kupunguza malumbano yasiyo ya msingi.
 Dhana ya kijana ni”taifa la kesho”, imebaki kuwa ni imani, uelewa au maana inayotolewa na watu wanaomtazama kijana kama mtoto ambaye anahitaji malezi kwa kuwa umri wake ni mdogo. Katika matazamo huu kijana hawezi kupewa nafasi za uongozi , kushirikishwa katika harakati za maendeleo na majukumu mbalimbali kwa kuwa umri wake bado haujitoshelezi, katika dhana hii pia kijana anaonekana kuwa bado hajapevuka kimawazo na kusitaharabika hivyo anatakiwa kuvuta subira hadi pale anapofikia utu uzima.
  Leo nikushirikishe mahojiano niliyofanya kwa zaidi ya vijana hamsini (50) hapa nchini hasa kwa mkoa wa Dar es salaam na Mbeya wao kwa upeo wao wanajaribu kuiangalia  dhana hii kuwa ni potofu kwani inalenga kudidimiza Maendeleo ya taifa. Kwa mataifa makubwa kama marekani vijana wanashiriki kikamilifu katikja shughuli za ujenzi wa taifa kama siasa, uchumi na masuala ya jeshi kwa usalama wa taifa lao.
Michael Sostern toka mbeya anasema”kitendo cha kumuita kijana ni taifa la kesho kinazorotesha juhudi na jitihada zinazofanywa na wadau na mashirika mbalimbali ya kiserikali na watu binafsi yanayofanya kila namna kumkomboa kijana, hii ni kutokana na umuhimu wa kijana kwa kipindi hiki cha ushindani wakimataifa katika teknolojia.Anaendelea kusisitiza kwamba katika jamii yoyote ile kazi ya kijana ni kusimamia mipango na mikakati iliyoachwa na wazee ili kufikia kilele cha mafanikoa, ikiwa ni pamoja na kulinda rasilimali na maliasili zisiharibiwe na kubaki  tunu kwa jamii na taifa kwa ujumla.
                  Ikumbukwe kwamba vijana wanakabiliwa na changamoto mabalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira, umasikini,magonjwa, madawa ya kulevya, uhaba wa vitendea kazi na mitaji. Kwa hiyo kitendo cha kumuita kijana ni taifa la kesho kinaendelea kumnyanyasa kijana  kana kwamba hana nafasi katika jamii yake.vijana ni taifa la leo na siyo kesho,wao ndiyo walinzi wa jamii,watetezi wa haki na wapigania maendeleo ya taifa.
     Bwana Michael anaturudisha kwenye historia ya  utawala wa Rais wa Marekani Barack Obama ambaye alikuwa na ndoto kubwa sana akiwa mtoto mpaka kipindi cha ujana wake.Akiwa kijana mdogo kabisa wa darasa la tatu, rais wa marekani Barack Obama ambae sasa ni mtu mzima lakini sio mzee hata punde aliandika juu ya azma na nia yake ya kuja kuwa rais siku moja na leo hii ndiye rais wa mwafrika wa kwanza katika historia ya marekani. Kwa sasa anayaishi mawazo mengi ya kwake pamoja na ya watu kama yeye duniani kote. Aliweza na anaweza akiwa bado katika umri mdogo tu wa miaka ya arobaini, huyu sio malaika ni mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke.
              Ingawa hakujua ni nchi gani angekuja kuwa rais lakini lengo lake lilikuwa kuwa rais na kufanya maisha ya watu kuja kuwa ya furaha. Alikulia mazingira magumu ya ubaguzi wa rangi tofauti kabisa na nchi nyingi za Afrika na Tanzania ikiwemo. Kwa hiyo kama ni swala la kuishi mazingira magumu hata watu kama rais huyu waliishi maisha hayo. Sasa hapo utaona maamuzi mengi aliyafanya akiwa kijana na sasa anavuna matunda ya maamuzi hayo. Yupo katika hatua ya kuelekea uzeeni lakini ameacha historia ambayo kijana yoyote angetamani kuwa kama yeye.
  Batromeo H Mbogo anawaangalia vijana katika mitazamo mitatu tofauti; huku akizingatia zaidi umuhimu wao katika ujenzi  wa taifa moja, kijana ni taifa la leo kwa sababu ya uchapaji kazi wake. Pili kijana ni taifa la leo kwa sababu ya uongozi katika jamii. Jamii zilizoendelea kijana ndiye anayepewa nafasi  ya kusimamia  na kuratibu masuala mbalimbali ya kijamii.tatu anamweleza kijana katika kigezo cha umri,  kutokana na kuwa umri wao unaruhusu  wana nguvu na uwezo wa kuamua  na kufanya mipango ya sasa na badaye.
  Anaendelea kufafanua kwamba siku zote ninashangazwa sana na baadhi ya wanasiasa wanaosimamia mtazamo hafifu wa kumuona kijana  ni taifa la kesho hii inadhihirisha hali ya kutokujua mambo ya msingi na namna ya kumshirikisha kijana katika michakato ya ujenzi wa jamii endelevu.
Baada ya Zitto Kabwe kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi wa mwaka2015 wadau na wanasiasa walipinga hali hii hasa wale wa chama chake wakisema bado ni kijana mdogo hivyo awaachie wazee na yeye asubiri pale atakapofikia miaka yake kikatiba.
             Kama tutakuwa na nia nzuri ya kuwaita vijana ni taifa la kesho mbona hatuhoji historia ya uongozi wa mwalimu NYERERE  kwa mfano,alipokuwa na miaka 36 aliingia katika baraza la kikoloni na akachaguliwa kuwa waziri mkuu akiwa na miaka 38 na mwaka 1961 Tanganyika ikawa taifa huru na Nyerere akawa waziri mkuu wa kwanza akiwa kijana wa miaka 39 na mwaka ulofuata Tanganyika ilipokuwa jamhuri akawa rais wa kwanza. Na baada ya hapo yeye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa muungano ambao uliizaaa Tanzania ya leo?.
 Mbogo anaendelea kusema serikali isisipoliangalia suala hili tutaishia katika kutukuza wazee huku tukisahau umuhimu wa vijana na kuwanyima nafasi za msingi ili waweze kuleta mabadiliko na kufutilia mbali umaskini,uongozi mbaya, ajira na nafasi ya kazi, elimu duni, maisha duni na changamoto zinazowakabili vijana katikla kujikwamua kiamaisha. Jukumu la  kuwaandaa vijana kuwa wazalishaji mali liko mikononi mwa jamii nzima.
                Kwa upande wake Lukas  Nkoko Mwanafunzi wa chuo kiku Dar-es-salaam ansema”hatuna sababu ya kubeza misemo hii miwili ya kijana ni taifa la kesho au leo” hapa tujiulize maswali, kijana tunayemzungumzioa ni yupi? Mwenye miaka mingapi?, mwenye mchango gani katika jamii? anapewa kipaumbele gani katika ujenzi wa taifa? .
              Kijana  ni mtu mwenye umri wa miaka 15-35 katika umri huu vijana wanawajibika katika kila hatua za ujenzi wa jamii zao, pia katika umri huu bado vijana wana nguvu na nafasi ya kushiriki katika mipango ya familia na jamii  Zao.
                 Hakuna jamii inayopinga au kukataa umuhimu wa kijana. Zipo sababu mbalimbali zinazowafanya vijana wasiaminike katika jamii ikiwa ni pamoja na  kujiingiza katika mapenzi na ngonon zembe, madawa ya kulevya, wizi, ubakaji, utapeli,uvivu, ulevi kupoindukia, vurugu,kukosa busara na mavazi.pia kianachofanya vijana wasiaminike kuwa wanaweza ni tama ya mafanikio m,akubwa pasipokufanya kazi kwa bidii, kudai masilahi makubwa zaidi ya kazi na kitendo cha kudai haki kwa kutumia mabavu badala ya amani.
                  Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania  hatuna budi kufanya mipango thabiti na mikakati bainifu kumkomboa kijana, kuweka misingi ya elimu yenye tija ili kumfanya  aendane soko la ushindani,hatuna budi kufungua milango ya kazi na ajira kwa vijana ili kuwaandalia maisha bora na siyo bora maisha.
              Kuhusu serikali bwana Lukasi  ansasema serikali iweke hazina kwa vijana ikikukmbukawazi mchango wa vijana katika kuinua uchumi  na kulinda ili kuihakikisha usalama miongoni mwa wanajamii.pia anaiasa serikali kujenga na kuimarisha secta zilizopo ili kukizi kiwango cha ajira kwa wahitimu kwa wote hawa ndiyo wahanga wa tatizo hili.tukome kuwaita vijan ni taifa la kesho.
                 Kadhalika Binedicto Furaha(UDSM) Soshiolojia anasema falsafsa ya kijana ni taifa la kesho haina mantiki yoyote na haisaidii  katika juhudi za ujenzi wa taifa jipya. Hatuna sababu ya msingi  kumuita kijana ni taifa la kesho. Madhara ya kupotosha wakati  wa vijana ndiyo kwa asilimia kubwa yamechangia kuzorota kwa jitihada za kuleta maendeleo ya jamii zetu.ukosefu wa ajira, utendaji mbaya, kungangania madaraka ni dalili za wazi za mitazamo mfu ya kumuita kijana ni ytaifa la kesho.
           Falsafa hii pia inakatisha tamaa na kuwafanya vijana wahisi kuwa wao ni watoto wadogo hivyo hawafai kushiriki katika shughuli kubwa kama kuwa viongozi wa ngazi za juu za kiserikali.Viongozi wengi wamekuwa wakisema mara kwa mara hasa wanapowapa nasaha utasikia wakisikika wakisema “Vijana ni Taifa la kesho fanyeni kazi kwa bidii na sio kuzurula ovyo, hampaswi kuishi lelemama na kuzubaa katika vijiwe huku mkipiga soga ambazo hazina umuhimu katika maisha yenu kwa manufaa katika kukabiliana na changamoto zao .
               Kadhalika naye Jidai Masanja mwanafunzi chuo kikuu UDSM  anasema “Napata tabu sana katika kufikiri ili nielewe katika tafsiri ya kijana taifa la kesho,sielewi mwanzilishi wa falsafa hiyo alikuwa anamaanisha nini na kwa maslahi ya nani? Endapo yupo basi nahitaji mjadala naye ili kuweka sawa hoja husika”. Mimi ninachojua kuhusu kijana ni kwamba ni mtu mwenye umri wa 18-45
    Katika karne hii ya 21 ambapo maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesambaa duniani kote vijana wanapaswa kushika madaraka mbalimbali katika taifa lao ili kuleta mabadiliko yatayolisaidia taifa kujikwamua na kufikia soko la dunia,ni jambo la aibu kumkuta  kijana anahangaika karibia miaka mitatu akizunguka huku na huko akiomba ajira au kazi huku mzee ambaye kimsingi anapaswa kustaafu bado yupo kazini, “huu ni ubinafsi,uchoyo na ulafi”.
    Vijana na jamii kwa sauti moja ya kusikika  tuseme ukweli dhidi ya kauli hii ya kijana ni taifa  la leo badala ya kusema ni taifa la kesho kimsingi wazee  wana watoto ambao wanawaendeleze kielimu hivyo basi zibuniwe na kuanzishwa secta nyingi zitakazo kidhi idadi ya wahitimu. Tulijenge taifa letu kwa kuwashirikisha vijana, tufungue milango na fursa zitakazowanufaisha vijna.tuwape nafasi kisiasa na kiutalawa ili tuone na kupima nguvu yao katika uzalishaji.



Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3. ...

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kuto...