MAMBO MUHIMU KILA KIJANA KUYAKAFAHAMU KUHUSU YEYE (KIJANA):
1.
Ni lazima ujitambue, upate ufahamu sahihi juu ya maisha yako pamoja na mambo
yote na jamii inayokuzunguka
2.
Ni muhimu ujue wajibu ulionao kwako wewe mwenyewe kama mtu binafsi juu ya
maisha yako
3.
Kuna haja ya kujua kuwa wewe ni sehemu ya familia yako na lazima ujue wajibu
wako kwa wazazi na familia kwa ujumla
4.
Ni lazima ujifunze kuwa mzalendo wa taifa lako sawa na jinsi ambavyo Mungu
anataka, fahamu kuwa umeunganishwa na ardhi ya Tanzania kwa mafanikio yako,
Mungu akikwambia nenda nje ya nchi nenda lakini usifikiri mafanikio hayako
Tanzania
5.
Kijana anatakiwa ajitambue, ajielewe yeye ni nani na ana kusudi gani katika
maisha yake
6.
Unatakiwa kupata uelewa wa kutosha juu ya kipindi cha ujana na umuhimu wake
ukiwa bado Kijana ili ujue namna ya kuzingatia na kujipanga kwa hapo baadae
7.
Kuelewa changamoto zilizopo katika kipindi cha ujana na namna ya kuzishinda
kuna uhusiano na namna unavyojitambua ukiwa bado kijana
8.
Kujenga shauku, nia na kiu kwa kijana ili aweze kuishi maisha yenye mwelekeo na
aweze kutimiza maono yake akiwasaidia na wengine kumjua Mungu na maisha yake
kwa ujumla wake
9.
Kuwekeza uthamani na nguvu ya kipindi cha ujana kwa mtazamo wa Ufalme wa Mungu
UELEWA
JUU YA UJANA NA KIJANA
1. Ujana ni hatua ambayo
mtu anaipitia baada ya utoto au ni kipindi cha kati cha makuzi ya mtu kabla ya
utu uzima na hatimae uzee
2.Ujana huanza mara
baada ya mtu kubadilika kimaubile na huanzia miaka kumi na mbili wengine hadi
kumi na tano ambapo mtu huanza kuwa na hisia za kimwili na kutamani sana kuwa
na uhuru wake katika maamuzi. Mabadiliko haya huchochea au qhupelekea hisia mbalimbali za kimwili na mabadiliko ya jumla
ya tabia
3.Ujana ni majira
yanayopita katika makuzi ya mwanadu, ukifanikiwa kuwa mzee ni lazima ulipita
katika kipindi hiki au daraja hili la ujana, kwa hiyo kama bado uko katika dara
hili ni muhimu kujipanga ili usije ukajilaumu mbele ya safari
ZINGATIA
HII
“Huwezi
kuyajali maisha yako kama hujui thamani yake, huwezi kujua thamani ya maisha
yako kama hujajitambua kwa Neno la Mungu, huwezi kuwa na maisha ya mafanikio
kama maamuzi yako hayatengenezi mafanikio, ufahamu sahihi juu ya maisha yako
ndio msingi wa kujitambua kwako, yaani kuijua Kweli ili hiyo Kweli ikuweke huru
na ndipo utakapokuwa huru kweli kweli, kumbuka hata usipoamua maisha yako
yataendelea kama kawaida. Zaidi ya hayo kama hujui wewe ni nani huwezi kujua
thamani yako, kama hujui thamani yako lazima utaishi chini ya kiwango cha
maisha unayotakiwa kuishi”
UTAIJUAJE
NAFASI YAKO KAMA KIJANA
Nafasi
yako kama Kijana ni wajibu wako, umuhimu ulionao kwako na kwa jamii kwa ujumla
wake pamoja na familia yako. Lazima ujue Nafasi yako katika maeneo yafuatayo:
•
Kwako binafsi,
•
Kwa familia yako,
•
Kwa kanisa lako,
•
Kwa jamii yako
•
kwa mkoa wako,
•
kwa taifa lako na
•
kwa Ufalme wa Mungu. Safari ya kujua
Nafasi
yako katika maeno yak ohayo yote inaanzia katika neon moja tu: KUJITAMBUA.
Jenga
Ufahamu Hapa
1.
Kujitambua ni hatua ya muhimu katika maisha ya mtu yoyote duniani kama anataka kuishi
kwa Furaha na matumaini na kufikia malengo yake
2.
Kujitambua ni matokeo ya kupata ufahamu sahihi juu eneo fulani utakaokusaidia
kufanya maamuzi sahihi katika eneo husika ili uweze kufanikiwa
3.
Ufahamu au maarifa unapatikana kwa kutafuta, kuchunguza na kudadisi taarifa
mbalimbali kwani si kila namna ya kujitambua ni sahihi kwa kijana
4.
Matokeo ya ufahamu ulionao yatafanana na ubora wa maisha unayoishi kwa kiwango
cha kuathiri maamuzi yako ya kila siku
5.
Kiwango cha matokeo ya kujitambua kitafanana na ubora wa taarifa ulizozipata
6.
Udhihirisho wa maisha ya kujitambau ni hatua ya juu kabisa ya kuthibitisha
kwamba kweli umejitambua
Comments
Post a Comment