JE, VIJANA NI TAIFA LA KESHO???
Mwandishi,Alfred
mwahalende
. Kutokutambua umuhimu wa
kijana katika Taifa au jamii ni kushindwa kutambua mchango wa makundi yaliyopo
katika jamii. Taifa lolote Duniani haliwezi kukua na kuwa imara kiuchumi,
kisiasa, kitamaduni na kijamii bila makundi yote ya jamii kushirikishwa
kikamilifu katika mapambano dhidi ya changamoto zinazolikibili taifa hilo kama njaa, vita, umaskini, maradhi, elimu duni na ugumu wa
maisha.
Ni ukweli usiopingika na
uliodhahiri kwamba maendeleo ya jamii zetu kwa asilimia kubwa
yanachangiwa na nguvu na maarifa ya vijana. Hivyo jamii isiyotambua umuhimu wa
kijana imekufa na haiwezi kujikwamua kufikia mipango thabiti.vijana wanapaswa
kushirikishwa katika harakati za kujikomboa kikamilifu na kutumia fursa zilizopo kutatua
matatizo yanayoikabili jamii
yao.
Hali kadhalika
katika ulimwengu huu wa sasa,asilimia kubwa ni vijana ambao kimsingi ndio
wanaopaswa kuwa viongozi wa leo na kesho na nguvu yao inahitajika sana katika
jamii zetu kutokana na mchango wao mkubwa katika kusukuma gurudumu la
maendeleo .Hivyo basi, vijana ni kundi kubwa na rasilimali muhimu katika kuleta
mabadiliko.
Falsafa ya “vijana Taifa la kesho” imekuwa
ikisemwa mara nyingi ambayo kwa matazamo wangu ni upotoshaji mkubwa
ukilinganisha na ukweli wa mambo, licha ya kuwa kauli yenyewe sio ngeni
katika masikio ya jamii, kwani imekuwa ikijirudia mara kwa mara katika misemo
mbalimbali. Kuna juhudi kadha wa kadha zimefanyika na wanaharakati
mbalimbali wa masuala ya vijana katika kuipinga falsafa hiyo na kuonyesha
falsafa mbadala katika kuweka mambo sawa na kupunguza malumbano yasiyo ya
msingi.
Dhana ya kijana
ni”taifa la kesho”, imebaki kuwa ni imani, uelewa au maana inayotolewa na watu
wanaomtazama kijana kama mtoto ambaye anahitaji malezi kwa kuwa umri wake
ni mdogo. Katika matazamo huu kijana hawezi kupewa nafasi za uongozi ,
kushirikishwa katika harakati za maendeleo na majukumu mbalimbali kwa kuwa umri
wake bado haujitoshelezi, katika dhana hii pia kijana anaonekana kuwa bado
hajapevuka kimawazo na kusitaharabika hivyo anatakiwa kuvuta subira hadi pale
anapofikia utu uzima.
Leo
nikushirikishe mahojiano niliyofanya kwa zaidi ya vijana hamsini (50) hapa
nchini hasa kwa mkoa wa Dar es salaam na Mbeya wao kwa upeo wao wanajaribu kuiangalia dhana hii
kuwa ni potofu kwani inalenga kudidimiza Maendeleo ya taifa. Kwa mataifa
makubwa kama marekani vijana wanashiriki kikamilifu katikja shughuli za ujenzi
wa taifa kama siasa, uchumi na masuala ya jeshi kwa usalama wa taifa lao.
Michael Sostern toka mbeya
anasema”kitendo cha kumuita kijana ni taifa la kesho kinazorotesha juhudi na
jitihada zinazofanywa na wadau na mashirika mbalimbali ya kiserikali na watu
binafsi yanayofanya kila namna kumkomboa kijana, hii ni kutokana na umuhimu wa
kijana kwa kipindi hiki cha ushindani wakimataifa katika teknolojia.Anaendelea kusisitiza
kwamba katika jamii yoyote ile kazi ya kijana ni kusimamia mipango na mikakati
iliyoachwa na wazee ili kufikia kilele cha mafanikoa, ikiwa ni pamoja na
kulinda rasilimali na maliasili zisiharibiwe na kubaki tunu kwa jamii na
taifa kwa ujumla.
Ikumbukwe kwamba vijana wanakabiliwa na changamoto mabalimbali ikiwemo ukosefu
wa ajira, umasikini,magonjwa, madawa ya kulevya, uhaba wa vitendea kazi na
mitaji. Kwa hiyo kitendo cha kumuita kijana ni taifa la kesho kinaendelea
kumnyanyasa kijana kana kwamba hana nafasi katika jamii yake.vijana ni
taifa la leo na siyo kesho,wao ndiyo walinzi wa jamii,watetezi wa haki na
wapigania maendeleo ya taifa.
Bwana Michael anaturudisha kwenye historia ya utawala wa Rais wa Marekani
Barack Obama ambaye alikuwa na ndoto kubwa sana akiwa mtoto mpaka kipindi cha
ujana wake.Akiwa kijana mdogo kabisa wa darasa la tatu, rais wa marekani Barack
Obama ambae sasa ni mtu mzima lakini sio mzee hata punde aliandika juu ya azma
na nia yake ya kuja kuwa rais siku moja na leo hii ndiye rais wa mwafrika wa
kwanza katika historia ya marekani. Kwa sasa anayaishi mawazo
mengi ya kwake pamoja na ya watu kama yeye duniani kote. Aliweza na anaweza
akiwa bado katika umri mdogo tu wa miaka ya arobaini, huyu sio malaika ni
mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke.
Ingawa hakujua ni nchi gani angekuja kuwa rais lakini lengo lake lilikuwa kuwa
rais na kufanya maisha ya watu kuja kuwa ya furaha. Alikulia mazingira magumu
ya ubaguzi wa rangi tofauti kabisa na nchi nyingi za Afrika na Tanzania
ikiwemo. Kwa hiyo kama ni swala la kuishi mazingira magumu hata watu kama rais
huyu waliishi maisha hayo. Sasa hapo utaona maamuzi mengi aliyafanya akiwa
kijana na sasa anavuna matunda ya maamuzi hayo. Yupo katika hatua ya kuelekea
uzeeni lakini ameacha historia ambayo kijana yoyote angetamani kuwa kama yeye.
Batromeo
H Mbogo anawaangalia vijana katika mitazamo mitatu tofauti; huku
akizingatia zaidi umuhimu wao katika ujenzi wa taifa moja, kijana ni
taifa la leo kwa sababu ya uchapaji kazi wake. Pili kijana ni taifa la leo kwa
sababu ya uongozi katika jamii. Jamii zilizoendelea kijana ndiye anayepewa
nafasi ya kusimamia na kuratibu masuala mbalimbali ya kijamii.tatu
anamweleza kijana katika kigezo cha umri, kutokana na kuwa umri wao
unaruhusu wana nguvu na uwezo wa kuamua na kufanya mipango ya sasa
na badaye.
Anaendelea kufafanua kwamba siku zote ninashangazwa sana na baadhi ya wanasiasa
wanaosimamia mtazamo hafifu wa kumuona kijana ni taifa la kesho hii
inadhihirisha hali ya kutokujua mambo ya msingi na namna ya kumshirikisha
kijana katika michakato ya ujenzi wa jamii endelevu.
Baada ya Zitto
Kabwe kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi wa mwaka2015
wadau na wanasiasa walipinga hali hii hasa wale wa chama chake wakisema bado ni
kijana mdogo hivyo awaachie wazee na yeye asubiri pale atakapofikia miaka yake
kikatiba.
Kama tutakuwa na nia nzuri ya kuwaita vijana ni taifa la kesho mbona hatuhoji
historia ya uongozi wa mwalimu NYERERE kwa mfano,alipokuwa na miaka 36
aliingia katika baraza la kikoloni na akachaguliwa kuwa waziri mkuu akiwa na
miaka 38 na mwaka 1961 Tanganyika ikawa taifa huru na Nyerere akawa waziri mkuu
wa kwanza akiwa kijana wa miaka 39 na mwaka ulofuata Tanganyika ilipokuwa
jamhuri akawa rais wa kwanza. Na baada ya hapo yeye alikuwa mmoja wa
waanzilishi wa muungano ambao uliizaaa Tanzania ya leo?.
Mbogo
anaendelea kusema serikali isisipoliangalia suala hili tutaishia katika
kutukuza wazee huku tukisahau umuhimu wa vijana na kuwanyima nafasi za msingi
ili waweze kuleta mabadiliko na kufutilia mbali umaskini,uongozi mbaya, ajira
na nafasi ya kazi, elimu duni, maisha duni na changamoto zinazowakabili vijana
katikla kujikwamua kiamaisha. Jukumu la kuwaandaa vijana kuwa wazalishaji
mali liko mikononi mwa jamii nzima.
Kwa upande wake Lukas Nkoko Mwanafunzi wa chuo kiku Dar-es-salaam
ansema”hatuna sababu ya kubeza misemo hii miwili ya kijana ni taifa la kesho au
leo” hapa tujiulize maswali, kijana tunayemzungumzioa ni yupi? Mwenye miaka
mingapi?, mwenye mchango gani katika jamii? anapewa kipaumbele gani katika
ujenzi wa taifa? .
Kijana ni mtu mwenye umri wa miaka 15-35 katika umri huu vijana
wanawajibika katika kila hatua za ujenzi wa jamii zao, pia katika umri huu bado
vijana wana nguvu na nafasi ya kushiriki katika mipango ya familia na
jamii Zao.
Hakuna jamii inayopinga au kukataa
umuhimu wa kijana. Zipo sababu mbalimbali zinazowafanya vijana wasiaminike
katika jamii ikiwa ni pamoja na kujiingiza katika mapenzi na ngonon
zembe, madawa ya kulevya, wizi, ubakaji, utapeli,uvivu, ulevi kupoindukia,
vurugu,kukosa busara na mavazi.pia kianachofanya vijana wasiaminike kuwa
wanaweza ni tama ya mafanikio m,akubwa pasipokufanya kazi kwa bidii, kudai
masilahi makubwa zaidi ya kazi na kitendo cha kudai haki kwa kutumia mabavu
badala ya amani.
Katika nchi zinazoendelea kama
Tanzania hatuna budi kufanya mipango thabiti na mikakati bainifu
kumkomboa kijana, kuweka misingi ya elimu yenye tija ili kumfanya aendane
soko la ushindani,hatuna budi kufungua milango ya kazi na ajira kwa vijana ili
kuwaandalia maisha bora na siyo bora maisha.
Kuhusu serikali bwana Lukasi ansasema serikali iweke hazina kwa vijana
ikikukmbukawazi mchango wa vijana katika kuinua uchumi na kulinda ili
kuihakikisha usalama miongoni mwa wanajamii.pia anaiasa serikali kujenga na
kuimarisha secta zilizopo ili kukizi kiwango cha ajira kwa wahitimu kwa wote
hawa ndiyo wahanga wa tatizo hili.tukome kuwaita vijan ni taifa la kesho.
Kadhalika Binedicto Furaha(UDSM) Soshiolojia anasema falsafsa ya kijana ni
taifa la kesho haina mantiki yoyote na haisaidii katika juhudi za ujenzi
wa taifa jipya. Hatuna sababu ya msingi kumuita kijana ni taifa la kesho.
Madhara ya kupotosha wakati wa vijana ndiyo kwa asilimia kubwa
yamechangia kuzorota kwa jitihada za kuleta maendeleo ya jamii zetu.ukosefu wa
ajira, utendaji mbaya, kungangania madaraka ni dalili za wazi za mitazamo mfu
ya kumuita kijana ni ytaifa la kesho.
Falsafa hii pia inakatisha tamaa na kuwafanya vijana wahisi kuwa wao ni watoto
wadogo hivyo hawafai kushiriki katika shughuli kubwa kama kuwa viongozi wa
ngazi za juu za kiserikali.Viongozi wengi wamekuwa wakisema mara kwa mara hasa
wanapowapa nasaha utasikia wakisikika wakisema “Vijana ni Taifa la kesho
fanyeni kazi kwa bidii na sio kuzurula ovyo, hampaswi kuishi lelemama na
kuzubaa katika vijiwe huku mkipiga soga ambazo hazina umuhimu katika maisha
yenu kwa manufaa katika kukabiliana na changamoto zao .
Kadhalika naye Jidai Masanja mwanafunzi chuo kikuu UDSM anasema “Napata
tabu sana katika kufikiri ili nielewe katika tafsiri ya kijana taifa la
kesho,sielewi mwanzilishi wa falsafa hiyo alikuwa anamaanisha nini na kwa
maslahi ya nani? Endapo yupo basi nahitaji mjadala naye ili kuweka sawa hoja
husika”. Mimi ninachojua kuhusu kijana ni kwamba ni mtu mwenye umri wa 18-45
Katika
karne hii ya 21 ambapo maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesambaa duniani
kote vijana wanapaswa kushika madaraka mbalimbali katika taifa lao ili kuleta
mabadiliko yatayolisaidia taifa kujikwamua na kufikia soko la dunia,ni jambo la
aibu kumkuta kijana anahangaika karibia miaka mitatu akizunguka huku na
huko akiomba ajira au kazi huku mzee ambaye kimsingi anapaswa kustaafu bado
yupo kazini, “huu ni ubinafsi,uchoyo na ulafi”.
Vijana na jamii kwa sauti moja ya
kusikika tuseme ukweli dhidi ya kauli hii ya kijana ni taifa la leo
badala ya kusema ni taifa la kesho kimsingi wazee wana watoto ambao
wanawaendeleze kielimu hivyo basi zibuniwe na kuanzishwa secta nyingi zitakazo
kidhi idadi ya wahitimu. Tulijenge taifa letu kwa kuwashirikisha vijana,
tufungue milango na fursa zitakazowanufaisha vijna.tuwape nafasi kisiasa na
kiutalawa ili tuone na kupima nguvu yao katika uzalishaji.
Comments
Post a Comment