NAMNA YA KUENDESHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI NA BIASHARA
Name; FILBERT NYONI
Phone no; 0656447888
email; nyonifilbert30@gmail.com
Vijana wenzangu popote mlipo Tanzania na duniani kote,poleni kwa mahangaiko ya kuendelea kutafuta ugali
kwani hata katika maandiko ya vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na
asile,na mwanaume atatafuta kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu,hii yote
ni kudhilisha kuwa ni lazima kila mtu afanye kazi kulingana na kipawa
alichojaaaliwa na mwenyezi mungu muumba wa mbingu na vyote vilivyopo katika uso wa duniani.
Najua kila kijana ananamna anavyotafuta RIDHIKI
ili mradi tu inakua halali, wapo
wanaofanya kazi mmoja mmoja,wapo walioajiriwa serikalina, taasisi
za serikali,
taasisi na mashirika binafsi, lakini wapo ambao
wameamua kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali za kijasiariamali, wapo wakulima, wafanyabiashara, mmoja na hata walioamua kuunda vikundi ili kuona
namna gani nguvu ya pamoja inaweza kuwafikisha pale wanapotaka kufika, yote kwa yote mkono unaingia kinywani. Leo ni fursa kwa wale ambao wameamua kuwa katika
vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na biashara, kuweka na kukopa n.k kwani watajifunza mengi kupitia makala
hii.
Maana ya neno kikudi…….
Kikundi ni mkusanyiko wa watu kadhaa wenye rika
tofauti au linalofanana, jinsia
moja au tofauti ambao walioamua
kufanya shughuli za kujiingizia kipato kwa mujibu wa sheria, pamoja na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu
maendeleo
yao .Leo nitaomba tujadili kuhusu
vikundi vya vijana wenye umri kati ya miaka 15-35,
hili ni rika ambalo
linachangamoto nyingi sana za kimaisha katika jamii yetu.
kikundi cha vijana cha sanaa cha DEGE LA JESHI katika halimashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
NAMNA
YA KUUNDA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI KWA VIJANA
Hatua
ya kwanza
ni lazima mtafute vijana kwanza ambao mnalengo la
kuunda kikundi chenu
yaani vijana mnaofahamiana kitabia, wenye nidhamu na heshima katika kazi, wenye
tabia njema kwa jamii inyowazunguka, vijana msio na tabia ya wizi, ubakaji,
ulevi na utumiaji madawa ya kulevya, vijana wenye uthubutu na bidii katika
kazi.
Kwa kukosa sifa
zinazoendane hapo ndipo vijana wengi
huwa tunashindwa na kujikuta baada ya miezi miwili kikundi kimekufa. Ni vizuri tukaanza kwa kutambuana kwanza, sisi wenyewe kuwa ni vijana wa aina gani,tunataka kujiunga kwa sababu gani,je sababu tu ni
kelele za viongozi kuwa tujiunge kwenye vikundi?.Eneo hili linahitaji
fikra na busara sana, mkishindwa
hapa huko mbele hakuna litakalofanyika.
kikundi cha vijana cha sanaa cha YOUTH TALENT DEVELOPMENT MKOANI MBEYA
Hatua
ya pili
Ni muhimu kikundi kikawa na malengo ya muda mafupi na malengo ya muda mrefu ambayo yamepangwa pamoja na wanakikundi wenyewe
siyo mtu mmoja apange kwa niaba ya watu wengine, malengo hayo yaweza kuwa ya miezi mitatu, miezi
sita, mwaka na hata miaka mitano kulingana na aina ya
shughuli mtakazokuwa mnafanya.
Malengo yakipangwa na wanakikundi wote inakua
raisi kutekelezeka kwani kila mtu anaona yeye ni familia ya kikundi kile, lakini mkishindwa kuwa na ushirikiano basi ni
vigumu kuyafikia malengo yenu.
Hatua
ya tatu
Ni muhimu kutafuta uongozi wa muda kwani hapa ndiyo mahali ambapo
uongozi wa muda unatafutwa ili uweze kuratibu na kusimamia shughuli za
kuimarisha kikundi,
najuwa mpaka kufikia hatua hii kikundi bado kinakuwa kinapitia changamoto nyingi sana wapo watakaoona
wanapoteza muda,
wapo watakaokua wanajaribu tu kama
mtaweza fika mbali n.k
Hatua
ya nne
Kuandaa mchakato wa utengenezaji wa katiba ya
kikundi,
hapa ndipo jina la kikundi
hupatikana,
malengo na shughuli zitakazofanywa
na kikundi hujadiliwa na kwa kina, majukumu
ya viongozi watakaochaguliwa yatakua ni yapi, adhabu na mafao ya mwanakikundi, kwa kifupi katiba ndiyo
mhimili wa kikundi,
ikikosewa hapa ndio dira na
muelekeo wa kikundi utakuwa
unaenda kombo.
Katiba ni lazima ijadiliwe na
wanakikundi wote.
Hatua
ya tano
Ni kusajili katiba ya kikundi, ni muhimu katiba ikasajiliwe katika halmashauri
husika ili kuweza kufanya shughuli kihalali.
NAMNA
YA KUENDESHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI
i) Kutengeneza katiba iliyobora.Kikundi ni lazima
kitengeneze katiba ambayo itatoa muongozo wa namna ya kujiendesha, majukumu ya viongozi na wajumbe wengine wa
kikundi.
Katiba ya kikundi ni lazima
ipendekezwe na wajumbe wengine ili kila kitu kilichomo kwenye katiba kieleweke
na kila mjumbe.
Sio vizuri na ni mbaya kunakili
katiba ya watu wengine na kuifanya iwe yenu kwani vikundi hutofautiana kwa aina
ya watu waliopo na shughuli wanazofanya.
ii) Kuwa na uongozi imara.Kikundi ni lazima kiwe na
uongozi imara katika kusimamia shughuli mbalimbali za uzalishaji na utawala.Ni
muhimu kuchagua viongozi wenye nia na lengo la kufanikisha kikundi kinasonga
mbele,usimchague mtu sababu/kiongozi sababu ni ndugu au rafiki yako au
mnafahamiana.
iii) Wanakikundi lazima waheshimiane wao wenyewe bila
ubaguzi wa aina yoyote ile wa rangi,jinsia,kitikadi,kiuchumi,kuwa na nidhamu ya
matumizi ya pesa na mali zingine za kikundi.
iv) Ni lazima maamuzi yanayofanywa ndani ya kikundi
yafuate sera,sheria na kanuni zilizowekwa na kupitishwa na wanakikundi wenyewe.Maamuzi
yasifanyike kwa kumkandamiza mtu au kikundi cha watu Fulani ndani ya kikundi.
v) Kikundi pia lazima kiwe na mikakati ya kubuni
miradi ya uzalishaji mali ambayo ina tija kwa wanachama wake,miradi hiyo yaweza
kubuniwa na wanachama wenyewe au kuomba msaada toka kwa wadau wengine wa
serikali na mashirika binafsi.Vile vile kikundi lazima kijenge utamaduni wa
kuaminiana baina ya viongozi na wanachama wenyewe,kwani hii huongeza mahusiano
mazuri baina ya wanachama na kupelekea kikundi kufanikiwa.
vi) Viongozi wa kikundi lazima muwe na utaratibu wa
kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya kikundi,ni muhimu kutafuta
taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya vijana na stadi mbalimbali za maisha
ili muweze kujiendesha kiuchumi na kijamii pia.Kila mwanakikundi awe kiongozi
na asiwe kiongozi ni lazima ayaweke maslai ya kikundi mbele kuliko maslai
binafsi,ni vibaya kutumia pesa na mali za kikundi kwa kujinufaisha mwenyewe.
vii) Viongozi wa kikundi wanajukumu la kuhakikisha
kunakuwa na mgawanyo mzuri wa majukumu kwa wanakikundi na
wafanyakazi walioajiriwa ili shughuli zote za kikundi ziweze kwenda kama
zilivyopangwa.
viii) Vilevile wanakikundi wanatakiwa kuwa na mtazamo wa
mbali na kuweka mawazo yao katika mpangilio mzuri wa kutekelezeka.
ix) Ni muhimu pia kuwa na vikao vya ndani vilivyowekwa
kwa mujibu wa sheria na katiba ya kikundi. Kutofanya vikao kunaweza kuibua maneno baina ya wanakikundi na
kukigawa kikundi.
Pamoja
na hayo yote,vikundi vingi vya ujasiriamali vya vijana vinakumbwa na changamoto
nyingi sana na hivyo kushindwa kuyafikia malengo kama ifuatavyo:
Vijana wengi waliopo kwenye vikundi vya
ujasiriamali wana haraka ya maendeleo ya ghafra na kwa muda mfupi, hivyo kushindwa kuendana sambamba na mifumo
mbalimbali ya kimaendeleo inayotolewa na serikali pamoja na wadau wengine.Vilevile
baadhi ya vikundi kushindwa kushiriki katika vikundi vya kuweka na kukopa
pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha.
Vikundi vingi vya vijana pia vimekosa taarifa juu
ya mifuko rasmi ya vijana ambayo ingeweza kusaidia kuwa chanzo cha fedha
kutunisha mifuko yao na hatimaye kuongeza mitaji waliyonayo, lakini pia hata wakizijua fursa hizo bado kuna
milolongo na vikwazo vingi vya kuwawezesha kupata fursa hizo. Lakini pia vikundi vingi vimekosa elimu ya namna
ya kusimamia shughuli za vikundi na hivyo kupelekea kupoteza dira ya maendeleo.
Tafadhali; Kabla ya kumaliza nitakua mchoyo wa fadhila kama sitozungumza
ili,vikundi vingi vya vijana vinavyojishughulisha na ujasiriamali huwa ni
vikundi vya mazoea,
huundwa kulingana na undugu wa
watu Fulani,
urafiki Fulani na hivyo kupelekea
mambo mengi kufanyika kwa mazoea. Lakini
pia vikundi vingi vya vijana vya ujasiriamali vinaanzishwa kwa lengo kuu la
kupata pesa au kuwezeshwa na mtu Fulani, na pale msaada unaposhindikana basi hufa mara moja. Hivyo basi ni vyema vijana tunapoamua kuwa pamoja, tunapoamua kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ni
vyema tukaepuka mambo haya, ni bora
mkawa wachache wenye lengo la kujikwamua kiuchumi kuliko kuwa wengi ambao hamna
faida yoyote.
Hongera sana ndugu mwandishi umetisha sana umenkfunza jambo nami pia ningependa kujiunga kwenye kikundi lakini sijapata fursa hiyo
ReplyDeleteAsante kwa kutufungulia njia kwa kutuelimisha kama vijana Wende future
ReplyDeleteGud lesson
ReplyDelete