Skip to main content

Posts

HATUA ZA MSINGI ZA KUKUSAIDIA KATIKA KUPANGA AU KUWEKA MALENGO YAKO

HATUA ZA MSINGI ZA KUKUSAIDIA KATIKA KUPANGA AU KUWEKA MALENGO YAKO; ü         Fanya maamuzi ya dhati kutoka moyoni mwako katika jambo au kile unachotaka kitokee kwako au kwa taasisi yako. ü         Andika Malengo yako na uyapangilie vizuri ü         Weka muda wa kuyafikia malengo yako ü         Vijue vikwazo au changamoto zinazoweza kukuzuia kuyafikia malengo yako ü         weka mikakati bayana kuyafikia malengo yako ü         Bainisha watu unaweza kuwashirikisha katika malengo yako na siyo kila mtu wengine wanaweza kukukatisha tamaa. ü         Panga ratiba yako vizuri na anza kufanya hatua kwa hatua ni kupima Malengo yako. ü         Weka vipaumbele ü       ...

UMUHIMU WA KUWA NA MALENGO KATIKA MAISHA YAKO;

UMUHIMU WA KUWA NA MALENGO KATIKA MAISHA YAKO;     ✅ Malengo huchochea ari ya kupenda kufanya kazi. ✅ Malengo huleta nidhamu katika matumizi ✅ Malengo ni daraja la mafanikio ✅ Malengo huongeza ufanisi katika kazi. ✅ Malengo hupunguza uzemba   ✅ Malengo huongeza nidhamu katika matumizi ya muda uliojiwekea. ✅ Malengo mazuri huvutia wahisani na marafiki wanaopenda kuona mafanikio: ✅ Malengo humfanya mtu asikate tamaa katika kazi au biashara zake. ✅ Malengo hujibu changamoto zinazoweza kukukwamisha. ✅ Malengo hutoa mwongozo na kipaumbele yaani kipi ufanye Leo, kipi Kesho na kipa Kesho kutwa.. ✅ Malengo hufungua mlango wa fikra chanya.

MADHARA YA KUISHI BILA MALENGO

MADHARA YA  KUISHI BILA MALENGO; ✍ Mtu asiyekuwa na malengo kamwe hawezi kufanikiwa katika maisha yake kwa sababu atatumia kila alichonacho hovyo hovyo. ✍ Mtu asiyekuwa na malengo hutumia vibaya muda wake na huishi bila ratiba ✍ Mtu asiye na malengo hukosa uthubutu yaani hawezi kujaribu kufanya chochote. ✍ Mtu asiye na malengo hawezi kuzifikia ndoto zake na badala yake ataishia kutamani tu. ✍ Mtu asiye na malengo hawezi kulijua kusudi la kuwepo duniani. ✍ Mtu asiye na malengo hawezi kuzungumzia kazi na mipango badala yake atazungumzia watu  na siyo kazi.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU.

HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU. MWALIMU SUBIRA MLAGA 💦 Kuna mambo kwa akili za kinadamu yanashindikana, akili ya kibinadamu inafika mwisho. Pale akili yako inapofika mwisho hapo ndio mwanzo wa akili za Mungu. "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."ISAYA 55:8_9. 💎 Yamkini kuna hali,majaribu na mapito mbalimbali unapitia sasa,watu wako wa karibu wamekukatisha tamaa kuwa hilo jaribu/pito/shida yako haiwezekani tena.Labda ni dokta kutokana na vipimo akakuvunja moyo kuwa hutapona tena,hautazaa tena na n.k. Leo nakumbia habari za Mungu mwenye uweza wa mambo yote hakuna jambo lolote la kumshinda yeye.Ukimwamini sasa atafanya yasiyowezekana katika macho ya wanadamu kuwezekana  na kuwashangaza waliokubeza. Haikuwa rahisi kwa ajuza Sara kuamini katika umri wa miaka tisini matiti yake yange...

NENO LA SIKU

NENO LA SIKU "Mamaye ajawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia , fanyeni."MATHAYO 2:5 Mariamu alijua ukuu na uweza wa Yesu,hakupata shida ya kuamini kuhusu utendaji kazi wake Yesu,Ndio maana alijua neno lolote atakalowaambia watumishi litakuwa.Leo watumiashi wa Mungu wamekuambia mambo mangapi kuhusu Mungu?? Na Mungu mwenyewe aliposema na wewe ulikuwa tayari kufanya sawasawa na alivyokuagiza??Leo usikubali Mungu akupite, tii na fuata maagizo yake anayokuagiza kupitia watumishi wake. LOLOTE MUNGU ATALALOKUAMBIA LIFANYE.

MAMBO YA KUFANYA ILI MUDA WAKO UKULETEE MAFANIKIO

MAMBO YA KUFANYA ILI MUDA UKULETEE MAFANIKIO. Mwalimu Subira Mlaga 1 . Chagua kitu cha kufanya :Haijarishi una mipango mingi kiasi gani.Toa vipaumbele katika mipango yako uliyojipangia.Pasipo kuwa na vipaumbele unaweza tamani kufanya kila kitu ndani ya muda mmoja.Unapoweka vipaumbele vinakusaidia kujua kitu gani uanze nacho na kitu gani kimalizie. Na kwa muda gani uwe umekamilisha na kuanza jambo lingine.Unapochagua ufanye nini na nini usifanye itakusaidia kukomboa muda. 2 . Tenda jambo sahihi kwa muda sahihi: Kila jambo lina muda wake.Ili ufanikiwe zaidi ni muhimu kufanya kila jambo kwa muda  sahihi.Mfano wewe unauza duka,muda wa kuwahudumia wateja wewe upo busy whatsup,instergram,fb unachati,mara kidogo unasuka nywele dukani ukweli ni kwamba unawapa wakati mgumu wateja wako hata kama hawatakuambia.Sasa wateja wakikuama utaanza lalamika,kuwa duka la jirani mchawi kahamisha wateja wako.Kumbe mchawi ni wewe mwenyewe umeshindwa kufanya jambo sahihi kwa muda sahihi.Ukiwa dukani...

KULIJUA KUSUDI

NA MWANDISHI, SUBIRA MLAGA KULIJUA KUSUDI. Hakuja jambo linalofanyika kwa bahati mbaya, kila jambo linalofanyika kuna sababu inayosababisha lifanyike kwa jinsi unavyoliona. KUSUDI:Ni sababu inayofanya mtu,au kitu kuwepo pale kilipo. Mfano kisu unapokuwa nacho kinalitumikia kusudi la kutengenezwa kwake.Kisu utakitumia kurahisisha shughuli zako mbalimbali.Pale kisu kinapokupa urahisi wa kazi yako hapo kinatimiza kusudi la kutengezwa kwake. 💎 Binadamu Mungu alipomuumba alimwekea kusudi ndani yake.Haijarishi unajua au haujui kusudi la kuumba kwako aina maana kuwa Mungu alikuumba bila ya kusudi.Katika kitabu cha mwanzo wakati Mungu akimuumba mwanadamu aliweka sababu kwa nini anamuumba."Mungu akasema,Na tumfanye mtu kwa mfano wetu ,kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani,na wanyama,na nchi yote pia,na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."MWANZO 1:26. Hapa inaonekana sababu ya kuumbwa mwanadamu kuwa atawale vitu vyote Mungu alivyo viumba....