MAKALA HII MAALUMU KUHUSU UGONJWA HUU WA LUPUS.
MWANDAAJI NA MWANDISHI NI LOOKMAN ADAMLUPUS NI NINI?
Huu ni ugonjwa ambao hutokea pale ambapo seli hai zinapogeuka na kuanza kuushambulia mwili..Kazi kubwa ya seli ni kulinda mwili hasa kupambana na magonjwa..ila kwa Lupus seli hizi huanza kuushambulia mwili zenyewe...
Zipo dalili nyingi za LUPUS ila hizi ni zile ambazo hujitokeza karibu kwa wagonjwa wengi WA LUPUS
🔹 Uchovu
🔹Maumivu ya Misuli wakati mwingine viungo kushindwa kufanya Kazi
🔹Kifuwa kuwaka moto hasa wakati wa kupumua
🔹Midomo kukauka
🔹Ngozi kutoka vipele vyekundu
🔹Kunyonyoka nywele
🔹Mkojo kutoka ukiwa na damu
🔹Kutoka vipele usoni kama vijipu vidogo
🔹Kupungua uzito
🔹Kukosa hamu ya kula
🔹Kuwa na hasira(Mara chache hutokea)
Wakati mwingine LUPUS hufahamika kama SLE (SYSTEMIC LUPUS ERYTHIMATOSUS)
Kama nilivyo eleza awalu kuwa LUPUS hutokea pale tu ambapo seli hai zinapogeuka na kuanza kushambulia mwili zenyewe hii hufahamika kama AUTOIMMUNE DISEASES.Na hii Mara nyingi hutokea kwa wale ambao wamerithi vinasaba vya ugonjwa huu wa LUPUS toka kwa wazazi wao.(Hapa naomba nieleweke sio lazima awe baba na mama namaanisha kuwa alierithi toka kwenye kizazi kilichotangulia,yaweza kuwa baba na mama au bibi na babu au hata waliowatangulia.Kama vile ilivyo kwa magonjwa mengine ya kurithi mfano Asthma yaani pumu na Albinism yaani ualbino)Pamoja na hayo ili LUPUS ijitokeze lazima mgonjwa awe katika mazingira Rafiki kwa ugonjwa,na ndio sababu waweza kuwa na vinasaba vya ugonjwa na usijitokeze.
LUPUS ziko za aina nyingi takribani aina kumi na moja hivi (11)
Lupus inaweza sababisha kifo endapo hali itakuwa mbaya.Na hasa pale inaposhambulia mwili na viungo muhimu kama FIGO na endapo figo ikashindwa Fanya Kazi husababisha KIFO. Tafiti zinaonyesha LUPUS huuwa zaidi vijana(mabinti).kwani ugonjwa huu huwapata zaidi wanawake takribani kwa uwiano wa asilimia 90% kwa 10% kwa wanaume.
Pamoja na kusababisha KIFO ila asilimia 80_90 ya wanaoguwa LUPUS hutemewa kuishi umri wao wa kawaida kama asiye na LUPUS .
Inashauriwa kwa mgonjwa WA LUPUS kuepuka baadhi ya vyakula kwa mustakbali bora WA AFYA take navyo ni pwmoja na hivi
+ Chumvi nyingi
+ Mafuta mengi
+ Vyakula vilivyosindikwa kiwandani
+ Nyama nyekundu
LUPUS SIO KANSA KABISA.
Kansa ni hali ya ongezeko LA tishu zisizo za kawaida katika mwili WA mwanadamu na kusambaa kwa haraka katika mwili. Wakati LUPUS ni hali ya seli kugeuka na kuushambulia mwili zenyewe.
Vyakula muhimu kwa mgonjwa WA LUPUS NI:
Vitamin E
Vitamin A
Vitamin B
Zinc
LUPUS SIO UKIMWI /HIV
HIV ni hali ya kinga ya mwili kushuka na kuruhusu magonjwa nyemelezi kuushambulia mwili..wakati lupus ni seli zenyewe kugeuka na kuushambulia mwili...
LUPUS haiambukizwi kwa namna yoyote ile iwe kugusana ,kujamiiana,kuchangia Nguo,kula ,hata kukumbatiana..Kwa maana hiyo mgonjwa WA lupus anaweza olewa na asiambukize mumewe hats kwa kujiriki tendo la Ndoa..MGONJWA WA LUPUS HASTAHILI KUNYANYAPALIWA.
MATIBABU
Mpaka sasa ugonjwa huu wa LUPUS hauna kinga wala matibabu ya moja kwa moja .Za…
Mungu atunusuru na maradhi ya ajabu kama haya
ReplyDelete