Nikusihii kitu kimoja mpenzi msomaji wa makala hizi za YAPOCODE TANZANIA kwamba maisha ambayo unaishi muda mwingine jua ni kwasababu ya utumwa ambao umeujenga katika fikra zako.Huu utumwa ambao umeujenga katika akili zako ni utumwa ambao umekufunga kufikiri vizuri juu ya maisha yako,ni utumwa ambao umekufanya kujiona huna thamani mpaka mtu flani akufanyie kitu flani ndipo ujione kwamba unathamani katika maisha yako.Mpaka lini utaogopa kufanya unachotaka kukifanya kwasababu mtu flani kafanya kitu kama kacho ambacho unaogopa kukifanya,lini utaacha uwoga wa kuwa mtu mnyenyekevu hata kwenye sehemu ambazo zinahitajjuhudi zako kuwa zaidi ya unyenyekevu sehemu ambazo sio? lini utasema sasa najijenga mwenyewe na niweze kuwa zaidi ya leo nilipo?. Nakusihii usiache utumwa wako wa kifikra kuacha lulu iliyoko ndani yako kupotea,usiache utajiri ambao uko ndani yako kupotea.leo hii anza na jitahidi kufanya kile ambacho unaogopa kukifanya lakini unajua kabisa kwamba ni kitu chema katika maisha yako.
Nimeshakutana na watu wengi sana ambao wanakuwa watumwa wa kifikra katika maisha yao kwasababu wanaogopa watu flani watawaambia kitu gani ikiwa wataamua kuchukua hatua nzuri za maisha yao.Nasikitika sana kumwona Lionel Richie wa kitanzania anaishi kama kuku anayefugwa ikiwa anaweza kutumia sauti yake kuimba na akatikisa Dunia, nasikitika kumwona Warren Buffet wa kitanzania akiishi maisha kama ya mtu ambaye hana ramani yoyote ya maisha yake ikiwa ana akili na mwili ambavyo anaweza kuvitumia na kupata hela ya kuwekeza katika biashara,nasikitika kumwoma Mmbwana Sammata kutoka sehemu zingine za Tanzania ana smartphone nzuri lakini anakuwa ni mtu ambaye hajui alichokuwa nacho ikiwa anaweza kutumia YOUTUBE,FACEBOOK,INSTAGRAM kuweza kujitangaza kwa kipaji alichokuwa nacho na akapata nafasi za kusonga mbele kimataifa,nasikikita sana nikimwona Mrisho Mpoto katika sehemu zingine za Tanzania lakini anaogopa kuimba kwasababu watu watamcheka. Nazidi kuvuta picha kwa wadada na wanawake kwamba nasikitia nikimwoma Ophrah wa kitanzania akiogopa kutumia sauti yake na ujasiri wake kwasababu anaona tayari kuna watu bora zaidi yake, nasikitika nikimwona Mama Alaska mwingine wa Kitanzania katika maeneo mengine Tanzania anayeogopa kuthubutu kwasababu anaona Mama Alaska tayari yupo,nazidi kusikitika kumwona mwanamke mwenye kipaji cha uhubiri na kufundisha neno la Mungu zaidi kama Joyce Mayer lakini anaogopa kuomba nafasi kufundisha wenzake kanisani na hata kwenye mitandao ya kijamii.
Leo ni mwisho kwa ufungwa huu wa kutokutumia ulichokuwa nach,leo hii iwe ni siku ya kusema utumwa huu ambao unasababisha umasikini katika maisha yako sasa baasi.
Kama bado hujajiunga na program ya akili ya ushindi jitahidi sana kupata maelezo haya kwa kubonyeza http://www.akiliyaushindi.com/jiandikishe
Ulikuwa nami;
Kocha Lazaro Samwel
0753616584
EMAIL; lazarosamweli41@gmail.com
Comments
Post a Comment