NI NINI CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI NA NANI ALAUMIWE?
NI, EMMY SUMUNI
1.WAZAZI/WALEZI: ninapo sema wazazi au walezi nina maanisha malezi anayopata binti huyu toka kwa wazazi/mzazi/walezi,hii inaweza kuwa pamoja na manyanyaso anayopata binti hadi kupelekea kukata tamaa na kuingia ktk vishawishi vibaya.hii ni kwa upande wa walezi wanaweza kuwa shangazi wajomba mama wa kambo n.k.
Pia kwa upande wa wazazi inaweza kuwa kumdekekeza mtoto kila anachotaka unampatia mtoto akifanya kosa hakemewi wala kuchapwa malezi haya yanaweza kumpelekea mtoto kujiona yeye ndio yeye maamuzi yoyote anaweza kufanya.
2.MARAFIKI/JAMII : hapa kuna vishawishi toka kwa marafiki wabaya pia jamii inayomzunguka mtoto ,hutegemea sana na mazingira anayokaaa watu anao kuwa nao muda mwingi akiwa nyumbani.
3.HALINGUMU YA UCHUMI; Kipato duni kwa wazazi/walezi hupelekea binti kukata tamaa na kushawishika na chips kuku n.k
4.UMBALI MREFU TOKA HOME HADI SHULENI: kutokuwepo na usafiri wa uhakika kwa mabinti zetu hasa vijijini hulazimika kutembea umbali mrefu hii hupelekea kuchoka na kushawishika kiurahisi na vijana wa bodaboda mwisho wa cku ni mimba za utotoni.
5.TAMAA MBAYA; Hupelekea binti kujiingiza ktk makundi mabaya ilimradi apate anachokita,kuiga tamaduni za kigeni bila kuzingatia mila na desturi yetu
POWERED BY YOPOCODE
Ni nani alaumiwe msichana au mvulana
ReplyDelete