MHUTASARI KUHUSU MRADI
Katika uzinduzi wa
kampeni hii ya Binti Jitambue ni moja ya utekelezaji wa malengo 17 ya malengo
ya milenia ambayo yaliafikiwa na wanachama 189 wa umoja wa Mataifa mwaka 2015,
ambapo lengo namba 3 linazungumzia haki sawa kwa wote na
kumwezesha mwanamke (Promote Gender Equality and Empower Women). Ukiachilia mbali malengo ya milenia hata shiriki
letu la YOPOCODE malengo yake yako bayana juu ya kumsaidia kijana kujitambua Na
hii inaenda sambamba kabisa na kampeni yetu ya “ BINTI JITAMBUE”.Hivyo
tunaamini kampeni hii itakuwa ni chachu ya maendeleo kwa vijana wa kike. Na kwa
mwaka 2017/2018 tutaanza na kata 18 za Halmashauri ya Mbeya vijijini na baadaye kampeni yetu kusambaa
mkoa mzima na taifa kwa ujumla wake.
VIASHIRIA
Kuna
viashiria mbalimbali ambavyo vimepelekea kuanzisha kampeni hii ya binti
jitambua
1.
Kuwepo
kwa wasichana ambao wanaacha shule kwa sababu ya kujiingiza kwenye mahusiano ya
kimapenzi ,hii inatokana na wasichana wengi kukosa elimu ya kujitambua na
kufanya maamuzi sahihi hasa pale anapokutana na vishawishi
2. Kuongezeka kwa
idadi ya wasichana wanaopata mimba wakiwa shule .
3.
Wasichana
kukosa elimu ya ujinsia kabla na baada ya kuvunja ungo.
MALENGO YA MRADI
Malengo mahususi ya mradi huu ni kuwafikia mabinti
900 katika Halmashauri ya Mbeya vijijini KUWAJENGEA UWEZO KUHUSU ELIMU YA KUJITAMBUA.
MALENGO YA JUMLA
Malengo ya kampeni hii ya “Binti Jitambue” yanatokana na changamoto mbalimbali ambazo mabinti wengi wanapitia
katika kipindi cha ukuaji na mabadiliko ya miili yao ambayo hutokea baada ya
kuvunja ungo.
Hivyo malengo yafuatayo yataweza kumwezesha binti
kutambua na kuchukua hatua kufanya maamuzi sahihi.
1. Kuwa na
taarifa sahihi za mabadiliko yanayotokea katika mwili wake. Hii itamwezesha
binti kujua ni wakati upi na ni nini cha kufanya anapoona mabadiliko fulani
katika mwili wake. Kwa sababu atakuwa na taarifa sahihi hivyo, ataweza kuchukua
hatua impasayo na kwa wakati sahihi.
2. Kutoa elimu ya kujitambua na kujiepusha na
vishawishi kutoka kwa wanaume
Wasichana wengi hukumbana na vishawishi kutoka kwa
wanaume ambavyo husababisha kushindwa kuendelea na masomo kwa kupata mimba, pia
kuingia kwenye ngono zembe ambayo huwafanya kutumia muda mwingi kujihusisha na
mapenzi badala ya kusoma. Hivyo tunaamini kampeni utawapa uwelewa wa kutosha
kuhusu njia mbalimbali za kuwaepuka mafataki huko mitaani
3. Kujumuika
na makundi rika
Elimu kuhusu makundi rika itawawezesha
vijana/mabinti kutambua nafasi yake katika kufanya maamuzi kwani wengi wao
hufuata mkumbo kutoka kwenye makundi rika elimu hii itawaongezea uwezo wa
kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.
4. Kuchagua
marafiki
Tunatambua kwamba kila msichana huwa na rafiki yake
ambaye anamwamini na kumweleza mambo yake yote, elimu ya kumwezesha binti
kuchagua rafiki mwema. Hii itawafanya
mabinti kuwa na marafiki watakaowaongoza kufikia malengo yao.
5. Kuwawezesha wasichana kuwa na malengo.
Wahenga walisema huwezi kupotea kama hujui
unapokwenda, kama wasichana watapatiwa elimu ya namna gani ya kupanga malengo
na kuyafikia malengo ambayo ameyapanga.
6. Kuongozwa
ili ajenge haiba.
Elimu kuhusu haiba itawawezesha mabinti kuwa
nadhifu katika mavazi na miili yao pia. Kwani kumekuwa na kasumba hasa kwa
mabinti kuvaa nguo za ajabu(nusu uchi) na hivyo kuongeza ushawishi kwa wanaume
hasa mafataki au wanaume wasio na hofu ya Mungu. Kwa mabinti wadogo wenye umri
sawa na watoto wao.
UHAI WA MRADI:
YOPOCODE kwa
mara kadhaa tumeshiriki katika kampeni za kijamii na kwa uzoefu tulio nao
miongoni mwetu viongozi inatupa imani na nguvu kuwa mradi huu pekee utadumu na
kuwanufaisha walengwa kwa kiasi kikubwa. Mwaka 2016 miongoni wa viongozi wetu
walishiriki katika kampeni ya LISHE YA MAMA NA MTOTO iliyokuwa inafanyika mkoa
wa Lindi chini ya shiriki la maendeleo ya wanawake ROWODO na kudhaminiwa na shirika la kimataifa la SAVE THE CHILDREN..
WADAU WAKUU WA KAMPENI/MRADI
Ili kampeni hii ya BINTI
JITAMBUE iweze kuwafikia wasichana wengi zaidi na jamii kwa ujumla wake, tumependekeza wafutao kuwa
wadau wa kampeni hii na mchango wao unahitajika sana kufanikisha mradi wetu;
a) Mkuu wa mkoa wa Mbeya
b) Wakuu wa wilaya ( kwa
sasa mkuu wa wilaya ya mbeya)
c) Maafisa elimu wa mkoa na
wilya
d) Maafisa maendeleo mkoa
na wilaya
e) Maafisa ustawi mkoa na
wilaya
f) Viongozi wa dini na
siasa
g) Wakuu wa shule za
misingi na sekondari
h) Wanafunzi wa kike kwa
shule ya msingi kuanzia Darasa la tano hadi la saba
i)
Wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha
kwanza hadi cha sita.
NAMNA YA KUFIKISHA UJUMBE WA KAMPENI
BINTI JITAMBUE ni
kampeni iliyoandaliwa mahususi kuwasaidia watoto wa kike/ binti kukuza uelewa
na kujitambua na hatimaye kufikia malengo kielimu na kimaisha kwa maslahi ya
maisha yao na jamii nzima. Kwa hiyo ili kuhakikisha ujumbe wa kampeni unaifikia
jamii ya Tanzania na walengwa yaani wanawake ( binti) tutatumia vyombo vya
habari kama ifuatavyo;
a) Mitandao ya kijamii kama
facebook, whatsapp na blogs
b) Radio naTelevision kwa
matangazo na mahojiano
c) Vipeperushi na mabango
d) Magazeti na majarida
e) Mbao za matangazo za
mashuleni
i) Aidha tutaanzisha
klabu za wasichana mashuleni zenye lengo la kuwafanya wapate mwamko wa kujadili
kwa pamoja changamoto zao kupitia midahalo na mijadala yao.
ii) mashindano ya mpira
wa pete na miguu kwa timu za wanawake.
iii) michezo na burudani
zitakazowafanya wakutane na kujenga urafiki miongoni mwao.
Comments
Post a Comment