UNGANA NA SHIRIKA LA VIJANA TANZANIA LA YOPOCODE, KATIKA KAMPENI YETU YA BINTI JITAMBUE TANZANIA, YENYE LENGO LA KUWASAIDIA WATOTO WA KIKE KUFIKIA MALENGO YAO KIELIMU NA KIUCHUMI
✅ Kwa mujibu wa shirika la watoto duniani la UNICEF k umekuwa na ongezeko la mimba mashuleni kutoka asilimia 23 hadi 26 yaani takribani watoto wa kike 8000 hapa Tanzania kila mwaka hukatisha masomo kwa ajili ya ujauzito na ndoa za utotoni amabazo kwa kiasi kikubwa huathiri ndoto za watoto wa kike kufikia malengo yao kielimu na kiuchumi.
✅ Vilevile idadi ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakimaliza elimu ya msingi lakini kutopewa nafasi ya kujiendeleza kielimu hata pale wanapokuwa wamechanguliwa kujiunga sekondari nayo pia imekuwa ikiongezeka na badala yake mabinti hawa wamekuwa wakilazimika kuingia katika ndoa KWA umri mdogo na hatimaye kushindwa kufikia malengo yao kielimu na kiuchumi.
✅ kushuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kingono kama ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kike na cha kusikitisha zaidi vitendo hivyo hufanywa na ndugu wa karibu sana wa watoto hawa wakiwemo wazazi, walezi, majirani na hata walimu huko mashuleni. Matukio haya yamekuwa hayaripotiwi katika Vyombo vya sheria kwani mengi huzungumzwa kifamilia na kuwaacha watuhumiwa wakiendelea na maisha yao.
➡
, Mimi na wewe tukae kimya na kuendelea kashangilia juu ya changamoto hii.
, Mimi na wewe tukae kimya na kuendelea kashangilia juu ya changamoto hii.
✅ Katika familia nyingi za kitanzania mtoto wa kike amekuwa akikosa fursa ya kupata elimu ukilinganisha na mtoto wa kiume na katika mazingira mengine wazazi wamediriki hata kuwaozesha watoto wao wa kike ili wapate pesa za kuwasomeshea watoto wa kiume. Ukiangalia pia suala Zima la elimu ni ukweli usiopingika kuwa idadi kubwa ya wasichana wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na tatizo hili.
BINTI JITAMBUE TANZANIA
Comments
Post a Comment