Skip to main content

*NAPENDA KUFUGA KUKU*

*NAPENDA KUFUGA KUKU*                                       
Habari rafiki, karibu katika makala ya siku hii ya Leo makala ambayo itakuwa inakufikia mala kwa mala kwalengo la kukupa elimu bora ya ufugaji wa kuku kutoka hatua yakwanza hadi ya mwisho karibu sana
        KWANINI UFUGAJI WA KUKU.                      
        
Ufugaji wa kuku ni secta ambayo inakuwa kwa kasi sana hapa nchini nasasa imekuwa ni sehemu ya ajira kwa watu wengi, ufugaji kwasasa umekuwa ukifanya vizuri sana kwakuwa na soko nzuri kwa ndani ya nchi yetu na hata nje ya nchi, Ufugaji umekuwa sehemu nzuri ya ajira kwa watu wengi na imekuwa kazi rasmi kwa watu wengi, Ufugaji umekuwa ni sehemu nzuri ya uwekezaji unaompatia MTU kipato makumtimizia malengo yake katika maiaha, Ufugaji umekuwa ni rahisi kufanya Na unafanyika katika maeneo yeyote mjini au vijijini, licha yakuwa Ufugaji wa KUKU kuwa Na faida nyingi pia Ufugaji wa kuku umekuwa na changamoto zake ambazo zinawafanya wafugaji wengi kukata tamaa katika Ufugaji huu wa kuku, Jambo lililokuwa nzuri nikwamba changamoto nyingi zilizopo kwenye Ufugaji ni aina changamoto ambazo inawezekana kabisa kuzipunguza iliwa tu tukiwa makini na kupata Elimu bora na sahihi katika secta hii ya Ufugaji wa kuku, changamoto hizi zinatokana na  wafugaji wengi wanaingia kwenye Ufugaji bila kuwa na Elimu sahihi ambayo itawapa mwongozo bora katika kufikia malengo waliyojiwekea katika ufugaji, kwakukosa huko kujuwa mambo muhimu yanayohusu Ufugaji inawapelekea kupata hasara kubwa na kushindwa kutimiza malengo ambayo walikuwa wamejiwekea katika maisha yao, Mimi kwakuliona hili nimeona bora nikuletee Elimu hii ili uweze kuwa Na elimu sahahi katika uwekezaji wako katika secta hii ya ufugaji

CHANGAMOTO KUBWA ZA UFUGAJI WA KUKU
MAGONJWA.
Magonjwa yamekuwa nichangamoto kubwa kwa wafugaji wengi hasa wanaoanza kuingia katika secta hii ya Ufugaji na hii inasababisha wafugaji wengi wakate tamaa ya kufuga nakuona kufuga hakuna faida yeyote kwasababu inawapa hasara kubwa ya kupoteza mifugo yao kwa vifo vinavyotokana na magojwa (jambo lakuvutia nikuwa katika mfululizo huu wa makala zangu nitaeleza mbinu ambazo kama utatumia utaweza kupunguza kwakiasi kikubwa cha magonjwa ya kuku kwakifupi nimekuja na majibu juu ya changamoto hii)
GHARAMA KUWA KUBWA ZA CHAKULA
Hii nimoja yachangamoto kubwa kwa wafugaji wengi wa sasa kwasababu wanapenda kufuga lakini wanajikuta wanashindwa kwasababu yakukosa mitaji ambayo itaweza kuwasaidia katika kuwapa chakula mifugo kutokana na changamoto kuwa kubwa kwa upande wa chakula watu wengi wameshindwa kuendelea na ufugaji wa kuku kwa wingi na wamekuwa wakifuga kwa idadi ndogo sana au kuacha kabisa kwasababu yakushindwa kukidhi mahitaji Muhimu ya chakula (endelea kunifatilia nimekuja na majibu ya changamoto hii kwakiasi kikubwa sana naamini nitaweza kukusaidia kupunguza gharama jadi kwa 50%)
WIZI 
hii ni moja ya changamoto ambayo zinawakuta wafugaji wengi wakuku hasa maanea ya mijini, wezi wamekuwa wakibomoa mabanda na kuingia kuiba kuku wengi nakupelekea Hasala kubwa kwa wafugaji (jibu la changamoto hii kama unafuga kuku wengi nibora ukaweka mlinzi anaweza akawa mbwa au milinzi kwa maana ya binadamu)
WAFANYA KAZI KUKOSA UAMINIFU
Hii pia ni moja ya changamoto kwa wafugaji hasa wanaofuga kuku wengi wamekuwa wakipata hasara ya kuibia baadhi ya mazao yamifugo kama vile mayai hata kuku wenyewe (suluhisho tafuta mfanyakazi mwadilifu/ funga kamela ili iweze kubaini udanganyifu)
Kwa Leo naomba niishie hapa tutaendelea siku nyingine kwa Elimu bora ya Ufugaji wakuku.
Endelea kunifatilia.......
Kwamahitaji ya vifaranga bora kabisa kwaajiri ya Ufugaji karibu sana vinapatikana, 
pia kwamahitaji ya MASHINE  bora za kutotoleshea vifaranga zinapatikana
Bila kusahau mayai kwaajiri ya kutotoresha, kula yanapatika kwa bei nafuu sana yanasafirishwa popote pale, 
Mayai na vifaranga vinavyopatikana ni yakuku chotara aina ya kroila
Karibu sana wote mnakaribishwa
Kwa mawasiliano zaidi 
0758918243/0656918243
Nimimi rafiki yako 
FRANK MAPUNDA 
KARIBU KATIKA UFUGAJI BORA WAKUKU TUKUZE UCHUMI 


Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3. ...

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kuto...