Skip to main content

NAPENDA KUFUGA KUKU* SEHEMU YA TATU

*NAPENDA KUFUGA KUKU*
SEHEMU YA TATU
Habari rafiki na mfuatiliaji wa makala hizi za *napenda kufuga KUKU* karibu sana tujifunze zaidi Yale mambo mahimu yatakayotusaida katika ufugaji bora wa KUKU,
AINA ZA KUKU NA FAIDA ZAKE
Kuna AINA mbalimbali za KUKU ambazo mfugaji anaweza kufuga na kila AINA inategemeana na malengo ya mtu husika anayetaka kufanya shuughuri hii ya ufugaji, hivyo Leo nimekuletea  makundi makuu manne ya KUKU ambayo tunayafuga hapa Tanzania
KUKU WA NYAMA 
hii ni moja ya kundi la KUKU ambalo linafugwa sana hapa nchini na kuku hawa wanafugwa kwa malengo ya kuzalisha nyama tu, 
Uzalishaji wa KUKU hawa wanachukuliwa KUKU wazazi kutoka nje ya nchi na kuhifadhiwa sehemu maalumu kwaajiri ya kuzalisha Mayai na Mayai yanatotoreshwa na kupata Vifaranga kwaajiri ya nyama ,
FAIDA YA KUKU HAWA
Faida ambayo utaipata kama mfugaji nikuwa KUKU hawa hufugwa kwa mda mchacheche mda wa miezi miwili au mitatu na kuuzwa kwaajiri ya matumizi ya nyama, hivyo nisehemu nzuri yakujipatia kipato na kunufaika na ufugaji wako kwa mda mfupi
ZINGATIA: gharama za kuwalea kuku hawa ni kubwa kidogo hivyo unapoamua kufanya ufugaji kwaajiri yakupata tija katika kukuza kipato chako nimuhimu ukafuga kuku wengi kwa wakati mmoja hii itakufanya upate faida nzuri kuliko kufuga kuku wachache na ukapata hasara na kuona ufugaji haulipi kumbe wewe mwenyewe haukuwa na taarifa kamili kuhusu ufugaji wako, 
*MUHIMU* Nimuhimu sana kutunza kumbukumbu za gharama za matumizi katika mradi wako wakuku ili pale utakapo uza uweze kujifanyia tathmini nakujuwa umepata faida au hasara katika mradi wako.
KUKU WA MAYAI 
Hawa ni aina ya kuku ambao hufugwa kwa malengo maalumu ili kuzalisha mayai, kuku hawa wanataga kwa wingi sana Mayai na wanataga bila jogoo, kuku hawa wamendaliwa vizuri kwaajiri ya kutaga tu hivyo kama utaamua kuwawekea jogoo wataga lakini Vifaranga wake watakuwa hawana ubora ule unaotakiwa.
FAIDA YA KUKU HAWA
Kwakuwa kuku hawa ni watagaji wazuri wamayai basi wanampatia mfugaji uhakika wa kipato kwa kila siku hadi pale atakapofikia mwisho wa mladi wake, (miaka miwili),
ZINGATIA 
Ili kupata faida iliyokusudiwa katika mradi wako huu wakuku unatakiwa uwape chakula bora na cha kutosha pia  uzingatie cha chanjo na tiba kwa magonjwa pale unapoona dalili ya magojwa, (endelea kunifatilia nitakuja kueleza chanjo na tiba kwa magonjwa yote yakuku kwa ujumla katika makala za huko Mbele)
*Muhimu* ufugaji wakuku ni moja ya aina ya miladi yenye faida nzuri iwapo tu mfugaji atazingatia kanuni bora za ufugaji,
Ufugaji huu ili ukuletee tija ni Muhimu ukafuga kuku wengi angalau miatatu na kuendelea hapo utaiona faida yake nzuri,
KUKU CHOTARA
Hawa ni aina ya kuku ambao wamechanganya aina Fulani ya kuku na aina nyingine ya kuku na kupata aina moja ya kuku, mfano: amechukuliwa jogoo  wakienyeji akachanganywa na tetea wa kisasa na  Vifaranga vitakavyotoka vitakuwa chotara kwamaana watakuwa na sifa baadhi za kienyeji na sifa baadhi zakisasa 
Kuku hawa kwahapa nchini wapo wengi na kuna makundi mbalimbali ya kuku kulingana na Asili na mahali walipo tokea, mfano: MALAWI, KENBRO, SASO, KROILA, N.K, hawa wanatofautiana sifa Na Asili 
FAIDA YA KUKU CHOTARA
Hapa nitataja kwa ujumla faida zote ila wakati mwingine nitachambua aina moja moja ya kuku chotara,
>wanakuwa kwa haraka na wanakuwa na maumbo makubwa tofauti na kuku wakienyeji (hivyo niwazuri sana kwa nyama)
>ni watagaji wazuri sana tofauti na kuku wakienyeji (kuku hawa ukuwahudumi vizuri wanataga Mayai kati ya (180-300)kwa mwaka hivyo niwazuri sana kwa Mayai
>wanaishi kwenye mazingira yeyote Yale kwamaana wanaweza kuishi vizuri wakiachiwa kujitafutia chakula 
>wanastahimili sana magonjwa (chanjo ni Muhimu kuwapa) tofauti na kuku wa nyama au wamayai
>nyama yao ni nzuri sana haina tofauti na kuku wakienyeji
>wanauzito  Mkubwa kuku mmoja anafika hadi kilo sita
>soko lake nikubwa
KUKU WAKIENYEJI
Hawa ni kuku ambao Asili yake ni hapa hapa Tanzania na tunao katika maeneo mengi ya nchi yetu, kuku hawa wanakuwa wanamaumbo madogo kulinganisha na kuku chotara, pia kuku hawa  hawakuwi kwa haraka ukilinganisha na kuku chotara,  aina hii ya kuku hutaga Mayai machache sana kwa mwaka na wanataga Mayai kati ya 40-120,
FAIDA YA KUKU HAWA
>kuku hawa wanafugika katika mazingira yeyote Yale kwasabu niwazuri kujitafutia chakula, ili upate faida nzuri ya mradi wako wa kuku huo unashauriwa kuwapa chakula cha ziada ili waweze kukua kwa haraka na kuwa Na uzito nzuri,
>kuku hawa hawana gharama hivyo nashauri kama una eneo nzuri ni Muhimu ukaanza ufugaji wa kuku hawa kwasababu hawana shida katika ufugaji wake
> kuu hawa wanapendwa sana hapa nchini kwasababu ya nyama na Mayai yake kuwa mazuri sana na nikuku wa Asili hivyo tunaamini hawana makemikali na hii nikweli kabisa,
Hizi ni aina mbalimbali za kuku katika nchi yetu na jambo la Muhimu kuangalia malengo yako na uhitaji ya jamii husika jambo nzuri na lakuvutia nikwamba aina hizi za kuku zinafugika katika maeneo yetu yote ya nchini hivyo angilia mazingira yako na anza kufanya ufugaji.
Nimimi rafiki yako 
Frank Mapunda
0758918243/0656918243
Karibu kwa mahitaji ya Vifaranga chotara aina ya KROILA, 
Pia Mayai kwaajiri ya kutotoresha na kula yanapatikana aina ya KROILA
Pia kwa mahitaji ya mashine kwaajiri ya kutotoresha zinapatikana 
Karibu sana rafiki


Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana kama uta

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3.     Ujana ni hatua ambayo mtu anapi