Skip to main content

NAPENDA KUFUGA KUKU* SEHEMU YA PILI

NAPENDA KUFUGA KUKU*
SEHEMU YA PILI
Habari za Asubuhi rafiki, Karibu sana katika kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ufugaji bora wa kuku, lengo KUU la makala haya kukupa Elimu iliyosahihi kuhusu ufugaji , Na mambo yote ninayoyaandika yanatoka kwenye uzoefu wangu mwenyewe katika ufugaji karibu sana.
MAMBO MUHIMU YAKUYAJUWA KABLA YA KUINGIA KWENYE UFUGAJI:
Moja ya changamoto kubwa kwa watu wengi tunajiwekea malengo makubwa kila mwaka kwamba nataka kufanya kile na kile ndani ya mwaka huu lakini kila siku bado unashindwa kuanza hii inatokana na changamoto mbalimbali za hapa na pale lakini sababu kubwa ni kokosa hamasa yandani juu ya kile tulichokiwekea malengo na hii inapelekea kila mwaka kuwa na malengo yaleyale bila kupiga hatua na kwenye upande wa ufugaji mambo ni hayo hayo kila siku natama kufuga natamani kufuga huku tukiendea kuimba wimbo usiokuwa na vitendo, nini ninachotaka kukwambia rafiki Asubuhi hii ya Leo  unahitaji kuchukua hatua chukua hatua sasa nasiyo kusubili subili utachelewa sana kufanikisha ndoto yako, huku siku zinaenda na majukumu yanazidi kuogezeka huku umri nao unakumbia, ninajambo Zuri ninalotaka kukwambia ni kuwa wakati mzuri wa wewe kuchukua hatua nisasa kipindi ambacho umepata wazo la ufugaji,
Unajuwa kwanini nakwambia nisasa kwasababu hakuna wati mwingine mzuri wa kuanza zaidi ya sasa, anza kufanya Na kuweka mipango yako mapema juu ya ufugaji wako, hapa chini nimekuandikia mambo ambayo unatakiwa kuyajuwa kwanza na kuyafanyia kazi unapotaka kufanya shughuri ya ufugaji za ufugaji ili uweze kufanikiwa katika ndoto yako ya ufugaji, najuwa unafahamu kuwa ufugaji kwasasa ni moja ya kazi yenye faida kubwa sana na somo lake ni pana sana (endelea kunifatilia nitakuja kukuonyesha  masoko mazuri ya mazao ya ufugaji yakiwemo Mayai, na kuku wenyewe bila kusahau samadi)
ELIMU NA MAARIFA SAHIHI KUHUSU UFUGAJI 
Hii imekuwa kama sehemu ya kujifichia kwa watu wengi wanaposhindwa kuanza jambo lalote hasa la ufugaji unakuta wanaibuka na sababu kuwa nashindwa kuanza kwasababu sina Elimu sahihi juu ya ufugaji sasa sijuwi unaaubili nini kuitafuta hiyo elimu na maarifa sahihi unajichelewesha rafiki, sasa nini unatakiwa ufanye
SULUHISHO:
Unapoweka malengo mfano Leo umeweka malengo nataka kufanya ufugaji, Leo hii hii tafuta taarifa sahihi zinazohusu ufugaji usisubili hadi mda ufike wawewe kufuga ndio uanze kutafuta taarifa nimuhimu sana kuwa Na elimu sahihi juu ya kile unachotaka kufanya, utapokuwa na taarifa na maarifa sahihi itakupa hamasa ya wewe kuchukua hatua mapema  katika kuyafanyia kazi katika ufugaji,
JUWA UNATAKA KUFUGA KUKU KWA MALENGO GANI: 
Nimuhimu kujuwa kwanini unataka kufuga kuku kwasababu ukijuwa kwanini unataka kufuga KUKU itakupa picha halisi juu ya kuku unaotaka kufuga ili uweze kutafuta taarifa sahihi juu ya ufugaji wako  kwasababu kuna aina nyingi za kuku na kila kuku anasifa zake na mahitaji yake hivyo ukijuwa malengo yako kuhusu ufugaji wako itakusaidia sana katika kufanya maamuzi na kutafuta taarifa sahihi kuhusu ufugaji wako
ENEO UNALOTAKA KUFUGIA 
Unapojuwa tayari malengo uliyonayo katika ufugaji na kujuwa aina ya kuku unaotaka kuwafuga sasa utakuwa na picha nzuri juu ya ufugaji wako, baada ya hapo unahitaji kujuwa ENEO GANI UNALOTAKA KUFANYIA UFUGAJI hii itakusaidia kujuwa malighafi ambayo itatumia katika banda lako, ni muhimu sana kuandaa eneo la kufugia mapema mala tu ya kuweka malengo yako ya ufugaji, juwa eneo lakufugia mifugo yako
GHARAMA ZINAZOHITAJIKA KATIKA KUFANYA UFUGAJI WAKO:  
Baada yakujuwa malengo eneo unalotaka kufanyia shughuri zako za ufugaji nimuhimu sana kuchanganua gharama zitakozotumika katika kuanza ufugaji gharama hizo ni pamoja na banda, chakula, chanjo na tiba, hii itakusaidia kuweka mipango yako sasa ili uweze kufanya ufugaji wako kwa ufanisi mzuri
ANZA NA ULICHONACHO: 
Hii ni jambo la muhumi sana katika kutimiza malengo ya aina yeyote, nimuhimu kuanza na kile ulichonacho usiabili hadi uweze kujipanga vizuri sana kwasababu unapoanza inakupa hamasa ya kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhusu ufugaji,
Ninapozungumzia Anza na ulichunacho nataka unielewe ninachomaanisha kwakuwa wewe malengo yako ni kufanya ufugaji unatakiwa uangalie nini ulichonacho unachoweza kuanza nacho mfano: malengo yako ni kufuga KUKU wa kienyeji 1000 na ukiangalia gharama zote za kufanya ufugaji ni million kumi (hii ni banda, chakula na madawa) na wewe mkononi unashilingi laki tano tu, Hauna haya yakuendelea kukaa na Pesa na kushindwa kuanza eti kwasababu pesa hazijatimia, unachotakiwa ni kuangalia nikwanamna gani unaweza kuanza na idadi ndogo ya mifugo huku ikiendelea na harakati zako zakuhakikisha unafikia lengo la kufuga KUKU 1000, 
Rafiki ninachopenda nikwambie kuwa unapoanza kufanyia kazi malengo yako utapata hamasa kubwa ya kuendelelea kuweka bidii na juhudi katika kufikia malengo yako
napenda nikwambie jambo moja rafiki ili ufanikiwe kwenye ufugaji hauhitaji hadi uwe na mtaji mkubwaa hapana kinachotakiwa ni kuanza kukifanyia kazi kile kidogo ulichonacho, ngoja nikwambie jambo furani ambalo naamini litakusaidia na wewe
Ikiwa unamtaji mdogo kabisa na unaeneo dogo na unataka kufanya ufugaji unachotakiwa kufanya ni kununua kuku wachache wanaweza kuwa watano labda wakubwa wanaokaribia kutaga hivi katika kuku hao matete manne na jogoo mmoja baada ya miezi mitatu naamini wataanza kutaga na tuchukulie kila mmoja ametaga Mayai kumi na kuangua Mayai matano hivyo kwa hesabu ya haraka utakuja kupata Vifaranga 20, nakatika hivyo (tutaelekezana mbinu ya kulea Vifaranga wengi kwa wakati mmja na  kupunguza hatari ya nagonjwa yatakayosabaisha vifo kwa vifaranga, endelea kunifatilia somo lipo Mbele litakuja) Vifaranga vikakuwa 12 naamini kama utawalea vizuri wakifika mieze sita watanza kutaga tena na huku hawa wakubwa watakuwa wametaga na kutotoa zaidi ya mala mbili kwa hesabu ya haraka utakuwa na kuku wakubwa wasiopungua 17= 12(wale Vifaranga)+5(wale wazazi) bado pia tutakuwa na Vifaranga visivyopungua 12 wamiezi mitatu na 12 wa wiki ukijumlisha wote hukosi 40, hapo ni kwa miezi tisa pekee sasa hapo huja zungumzia baada ya mwaka kwasababu wale kumi na mbili watakuwa wanataga sawasawa na wale wazazi, utaona kwa mtiririko huu baada ya miaka miwili unatimiza lengo la kufuga kuku 1000 kwa mtaji wa laki moja ulioanza nao 
Hii ndio nguvu ya kuanza na ulichonacho, haijalishi wewe unakiona kidogo kiasi gani ukikipeleka kwenye matendo kinakuwa kikubwa sana. 
Naomba niishie hapa kwa Leo,
Endelea kunifatitia ninamegi mazuri yakukwambia kuhusu ufugaji naamini yatakusaidia sana
Ni Mimi rafiki yako katika ufugaji
Frank Mapunda 
0758918243/0656918243
Karibu sana 
Pia kwamahitaji ya Vifaranga chotara (kloila)  karibu wanapatikikana,
Pia Mayai kwaajiri ya kutotoleshea/kula  yanapatiaka aina ya kloila 
Mwisho kwa mahitaji ya MASHINE ya kutotoleshea Vifaranga zinapatikana kwa bei rahisi sana MASHINE zenye ubora wa hali ya juu sana.
KARIBU SANA


Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana kama uta

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3.     Ujana ni hatua ambayo mtu anapi