Skip to main content

NAPENDA KUFUGA KUKU SEHUMU YA TANO

SEHUMU YA TANO

Habari Rafiki mfuatiliaji wa makala za Napenda Kufuga kuku karibu sana tuweze kujifunza pamoja mambo mazuri kuhusu ufugaji, lengo la makala hizi za napenda Kufuga kuku nikukupa Elimu sahihi kuhusu ufugaji wa kuku na faida na masoko ya mazao ya ufugaji karibu sana,

MBINU ZA MASOKO KWA WAFUGAJI 

Habari  Rafiki, Leo nimependa kuzungumzia swala la masoko ya mazao ya ufugaji kama unavyojuwa tunafuga na mwisho wa siku lazima tuingize mazao yetu sokoni, kumekuwa na changamoto kubwa kwa wafugaji wengi katika kupeleka mazao yao ya mifugo sokoni, wengi wananipigia simu wananiambia wanamazao ya mifugo lakini hawajuwi wapi watauza kuku wao wengine wananiambia wanamayai hawajuwi watawauzia wapi hii imekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi, Leo nimeona nije na mbinu au kanuni ambayo inanisaidia Mimi na huwa inawasaidia watu wengi pia katika kufanya biashara zao za kuku na mawayi na wamekuwa wanafurahi sana kwasababu soko ni kubwa na mafanikio ni makubwa, wewe ambaye umeingia katika uwekezaji huu wa kuku na umekuwa ukihangaika kupata Wateja wa mazao yako ya ufugaji karibu sana katika somo hili la Leo uweze kujifunza na kufurahia ufugaji wako

✍MASOKONI (vibanda Vya kuuza kuku)
Hii ni sehemu nzuri ya kuuza mazoa yako ya ufugaji kama vile kuku na mayai, hapa utakutana na wafanyabiashara wanaofanya biashara yakuuza kuku na Mayai hawa ni Wateja wazuri sana wa kuku na Mayai na huwa wanachukua idadi kubwa ya kuku na bei yao ni nzuri 

✍MIGHAHAWA MIKUBWA NA MIDOGO
Hii ni sehemu nzuri sana ambapo unaweza kufanya biashara yako ya mazao ya ufugaji (kuku na Mayai), hawa ni watu ambao wanauhitaji mkubwa wa kuku na Mayai kwaajiri ya chakula cha biashara katika biashara zao nimekuwa nikifanyanao biashara mala kwa mala sehemu hii na wamekuwa wateja wangu wakubwa na bei zao ni nzuri sana, wao mala nyingi wanapelekewa kuku na Mayai na madalali sasa wewe kama mfugaji ukitembelea sehemu hii utafanya biashara nzuri sana 

✍HOTERINI 
Hii ni moja ya sehemu ambayo wanahitaji sana mazao ya ufugaji, tembelea mwenyewe ujionee wamekuwa na uhitaji mkubwa sana wa mazao ya mifugo na watu wachache wameligundua hilo na kuchangamkia fulsa, ngoja nikuulize swali wewe unadhani wale wanaokuja kununua kuku wako bandani idadi kubwa wanawapeleka wapi? Ni huko nenda mwenyewe kashuhudie na uje unipe majibu maana nashangaa sana kuona ukilalamika hakuna soko wakati soko ni kubwa sana na wachache ambao siyo wafugaji wananufaika na wewe mfugaji unahadalaliwa na watu hao, amka rafiki huu ndio mda wako wakunufaika na ufugaji wako,

✍WAUZAJI WA SUPU
Hawa utawakuta maeneo mengi ya mijini hasa maeneo ya stand, baa, soko, Hospital, utawakuta wanauza supu hawa niwateja wazuri sana wa kuku Mimi mwenyewe nishahidi mzuri sana kwasababu hapa nilipo kuna watu wamenizunguka wanafanya biashara ya supu nashuhudia wakihangaika kutafuta kuku hadi wanaenda sokoni kutafuta kuku, sasa huoni wewe unahangaika bure wakati soko unalala nalo nyumbani sasa wewe endelea kulalamika sisi tunakuacha

✍WATU WENYE MASHEREHE 
Eeeh! Yani hadi hapa utaniambia soko hakuna Rafiki changamka ufugaji wako ni Pesa yako, ulizia wapi kunasherehe mwezi huu katika mtaa wako hata wilaya yako kawaambie Mimi nitawauzia kuku mkihitaji utashangaa watakavyochangamkia fulsa, nenda kaonane nao utaniambia nimekuwa nashuhudia watu wanaweka sherehe kuku wanapita kutafuta mitaani na kwenye vibanda Vya kuku ili wapate kuku kwanini wewe usiwarahisishie kazi kwa kuwaambia utawapelekea kuku, endelea kushangaa na kufa njaa wakati chakula unacho Mimi sipooo!

✍FUNGUA VIBANDA VYA KUUZA KUKU 
Nimekuwa nikishudia watu wengi wakihitaji kuku na hawajuwi wapi watapata wananiambilia sehemu zenye vibanda Vya kuuzia kuku ili kujipatia kuku, chakushangaza vibanda vingi havimilikiwi na wafugaji Bali vinamilikiwa na wafanyabiasha, sasa wewe unaonaje ufungue kibanda chuko na imukawa unauza kuku hapo, kiukweli sijuwi na wala siamini kama kunachangamoto katika soko la kuku kwamaana naliona pana sana.

✍MADUKA YA MATUMIZI YA NYUMBANI
Hapa nisehemu ambayo watu wengi huwa tunaenda kununua matumizi mbalimbali ya nyumbani sehemu nyingi huwa kunakuwa na Mayai wanauza wewe unadhani wanafuga wao wenyewee! Hapana wananunua sasa unaonaje kama wewe ukiwa mmoja ya watu wanaowapelekea Mayai. 
Sasa wewe kaa hivyo hivyo na kusema ufugaji hauna soko na ujihakikishie kufeli kwenye ufugaji Mimi sipo wewe baki ukilia peke yako Mimi masoko ninayo yakutoshaaa!

TUMIA KUNUNI HII ILI UNASE WATEJA WAKUTOSHA

Nenda stationary  katengeneza bisnescard ambayo utaandika taarifa zako muhimu na  mazao ambayo unayo nyumbani kama vile (kuku na Mayai) baada ya kutengeneza kadi yako ya biashara nenda maeneo ya kazi mfano: maofisini (bank, hospital, shuleni, nasehemu mbalimbali za ofisi) ukifika maeneo hayo zungumza nao kwa uchache kwasababu wapo maeneo ya kazi hawaweze kukaa kukusikiliza wewe hivyo unachotakiwa kufanya  wagawie kadi yako ya biashara na waambie wakutafute  nakuhakikishia utapokea Wateja hadi utashangaa, naomba nikwambie unadhani wafanyakazi wakiwa nashida na nyama au Mayai nani atakuwa wakwanza kutafutwa kama siyo wewe, sasa wewe shangaa watu tubebe wateja wako

✍Hizi ni baadhi tu ya masoko kuna mengi sijayazungumzia fanyia kazi hayo kama kunasehemu utafeli Karibu tuzungumze

Ni Mimi Rafiki yako 

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana...

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3. ...

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kuto...