YOUTH
POTENTIALS FOR COMMUNITY DEVELOPMENT (YOPOCODE)
SIMU: +255-758 051641,+255-768 577408,0765300255,0653983001,
0768416619
KWA MADIWANI WOTE WILAYA YA
MBEYA VIJIJI/VIONGOZI
WA VIKUNDI/TIMU/BENDI NA MTU
MMOJA MMOJA
|
YAH: MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA NANENANE 2017
LITAKALOFANYIKA VIWANJA VYA ILEMBO MBEYA VIJIJINI.
Rejea kichwa cha habari hapo juu kama kinavyojieleza. Shirika la vijana Tanzania la “Youth Pontential for Community development( YOPOCODE)” linakuletea Tamasha La Nanenane 2017 litakalofanyika katika viwanjwa vya shule
ya msingi ya Ilembo Mbeya Vijiji kuanzia
01/08/2017 hadi 08/08/2017.Lengo la
tamasha hili ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo
ikiwemo kilimo ili kuinua maisha yao kiuchumi. Pia kuhamasisha vijana kujali na
kulinda afya zao kwa kushiriki michezo na burudani mbalimbali zenye tija na
kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana Tanzania.Ili kufanikisha tamasha hili
kwa ubora zaidi shirika limeaandaa utaratibu ufuatao na kuteua vipengelee
kadhaa ambavyo vitashirikishwa katika tamasha letu. Aidha tumeanishi vigezo
hapo chini:
Aina Ya Kipengele
|
Kiingilio
|
Zawadi Kwa Mshindi wa (kwanza,pili na tatu)
|
Ngoma Za Asili
|
10,000/=
|
(I)100,000/=,(II)50,000/= (III) 20,000/
|
Mpira Wa Miguuu
|
20,000/=
|
I)Ng’ombe Na Mpira (II) Mbuzi Na Mpira Iii)Mpira1
|
Muziki/injiri/bongo/dansi
|
10,000/=
|
(I)100,000/=,(II)50,000/= (III) 20,000/
|
Midahalo
|
10,000/=
|
(I)100,000/=,(II)50,000/= (III) 20,000/
|
Maonyesho Vya Kilimo
|
10,000/=
|
(I)100,000/=,(II)50,000/= (III) 20,000
|
ZINGATIA:
Kwa upande wa mpira wa miguu tuanze mapema tarehe 26/05/2017 ligi kwa ngazi ya kata kwa kila kata na mshindi wa
kwanza ndiye atayeingia fainali itakayofanyika Ilembo mbeya vijiji. Kupata fomu
ya ushiriki piga simu au fika ofisini Ilembo madukani.aidha kwa vikundi vya
ngoma, kwaya na wasanii wa kujitegemea tuanze maandalizi mapema sana ili tuweze
kujizolea zawadi kiabao.
Alfred Sostern Mwahalende
Mkurugenzi mtendaji
YOUTH POTENTIALS FOR COMMUNITY
DEVELOPMENT
Comments
Post a Comment