TANZANIA YOUTH AND
CHILDREN DEVELOPMENT ORGANIZATION
UFUGAJI
BORA WA KUKU WA KIENYEJI
SEHEMU
YA KWANZA
UTANGULIZI
Napenda
kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa
mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana
nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Nimeamua kuuleta kwenu Wana group ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa
kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana
nazo.
A.KWA
NINI KUKU WA KIENYEJI?
1.
Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama
mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza.
2.
Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini.
3.
Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa
mazingira magumu kama ukame, baridi n.k
4.
Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU
WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE)
5.
Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni
muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda
mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha.
B.FAIDA
ZA KUKU WA KIENYEJI.
Faida
ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa
ni ngeni kwao.
-
Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji
linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
-
Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele
(shampoo)
-
Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga
kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo
ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
Zuia
viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua
mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga
kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula
mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato
unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku
C:
MAPUNGUFU
Yako
mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi.
MAGONJWA kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na
kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.
D:
KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuna maelezo ya kusisimua
sana kuhusu makabila ya kuku wa kienyeji, hata hivyo kuna ugumu kidogo kuweza
kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya
aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile
zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku.
Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi
ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
a.
Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
b.
Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
c.
Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
d.
Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
Mwingiliano
wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko.
Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi
au Kibutu.
Hivyo
kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa
kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.
(i)
KUCHI
Ni
kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache
mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa
uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm
45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na
Zanzibar.
(ii)
CHING'WEKWE
Kuku
hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana
sifa zifuatazo.
Majogoo
wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku
hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia
sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya
kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.
(iii)UMBO
LA KATI
Majogoo
wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa
wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa
kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya
ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu
- Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo
mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na
wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.
(iv)
SINGAMAGAZI
Ni
aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana
utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na
mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9,
mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.
(iiv)
MBEYA
Kuku
hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya
jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu
"Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49
(iiiv)
PEMBA
-Hupatikana
zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42
(xi)
UNGUJA.
Majogoo
Kg 1.6, mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana
sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.
SEHEMU YA PILI
1.
MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.
A.
MFUMO HURIA
Katika
mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji
na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi
lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.
FAIDA.
Mfumo
huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.
HASARA
Uwezekano
mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
Kuku
huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
Ni
rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
Utagaji
unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Uwekaji
kumbukumbu si nzuri.
Ni
vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.
UTUMIAJI
NZURI WA MFUMO HUU
Kuku
wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati
mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
Kuku
wapatiwe chakula cha ziada na maji.
Kuku
waandaliwe kwa viota vya kutagia.
Kuku
100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.
B.MFUMO
NUSU HURIA
Huu
ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/
wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza
kumpatia mfugaji faida haraka sana.
FAIDA
Sehemu
ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi
ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo
(Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na
mfumo huria.
C.
MFUMO WA NDANI
Kuku
hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye
mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za
mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.
FAIDA
Mfumo
huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto
litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa
na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.
HASARA
Uwezekano
wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda
UTUMIAJI
MZURI WA MFUMO HUU.
1.
Matandiko yageuzwe kila siku
2.
Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya
kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
4.
Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.
UTATUZI
WA KUKABILIANA NA VIKWAZO KATIKA UFUGAJI.
Mambo
ya kuzingatia:
Mabanda
bora - Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Sifa
za banda bora (Waone wataalam wa mifugo)
Kuchagua
kuku wa kuendeleza kizazi
Kuwa
makini na aina ya mitetea na majogoo unatakiwa kuchagua ili kuwa na kizazi
bora.
UTAGAJI WA MAYAI
Kwa
kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi
sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa
miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa
kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama
ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa
lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye
chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo
hicho.
Hakikisha
ya fuatayo.
Sehemu
iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi
sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai
yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.
UATAMIAJI
WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji
na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga
(Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja
Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia
kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji
na uanguaji wa asili
KUCHAGUA
MAYAI YA KUANGUA.
Hili
nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai
yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia
yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe
na uchafu yawe masafi
Yasiwe
na nyufa
Yatokane
na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe
madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe
mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe
yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe
yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.
KUMTAYARISHA
KUKU WA KUATAMIA
Pamoja
na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri
yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini
kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa
wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii
husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa
unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza
dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia
mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka
mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na
harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.
Ni
vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku.
Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.
PIA
JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI
Iwapo
una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na
kutotoa pamoja.
Unachotakiwa
kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
Unaweza
kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata
vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai
viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo
ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.
UTEKELEZAJI
WAKE
Kuku
anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku
anayotaga
Yanapofika
mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka
alama mayai yanayotagwa kila siku.
Mara
kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya
hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza
kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee
kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya
ukweli wakati wa usiku.
MUHIMU
Mayai
ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya
taa, manukato n.k.
JIFUNZE
PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji
anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba
baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa
maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii
itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au
kuyauza.
TAMBUA
VYAKULA NA UZALISHAJI WA KUKU - Sitalielezea hili naomba ufuatilie mwenyewe.
JIFUNZE
MBINU ZA KUZALISHA KUKU WENGI KWA MUDA MFUPI
Zoezi
hili linawezekana iwapo uleaji wa vifaranga kwa njia ya kubuni utatumika. Kuku
mmoja anaweza kutotoa zaidi ya mara saba kwa mwaka.
Hesabu
ya uzalishaji wa kuku wengi kwa mwaka kwa kutumia mtetea mmoja tu. Mpaka mwisho
wa mwaka unaweza kuwa na idadi ya vifaranga 252 kwa kadirio la vifaranga 8 kila
mzao. Hivyo kama una kuku 10 wanaotunzwa vizuri utakuwa umezalisha jumla ya
vifaranga 2520.
ULEAJI
WA VIFARANGA
NJIA
YA KUBUNI
NJIA
YA ASILI
Kuku anapo angua ,chukua vifaranga Kisha
tafuta box au jenga kibanda kidogo Kisha weka vifaranga ndani na weka TAA ya
aina yoyote kwalengo la kuwapatia joto.
Baada
ya kumnyang'anya mama vifaranga atarudi kutaga tena Baada ya siku chache .Lisha
vyakula kama Pumba ambayo ni maalum kwa vifaranga na watakuwa bila Shaka.
Kwa
kufanya hivo itasaidia vifaranga wasiliwe na mwewe au wadudu wengne
Pia
hawatashambuliwa na magonjwa sana
MAGONJWA
NA WADUDU WANAOSHAMBULIA KUKU WA KIENYEJI NA JINSI YA KUKINGA.
A.
MAGONJWA.
Ugonjwa
hatari - Mdondo/ Kideri (Newcastle desease) Hapo nyuma dawa ya kukinga ugonjwa
huu ilikuwepo lakini ilikuwa inahitaji kuhifadhiwa kwenye hali ya ubaridi
(Friji) Hali hiyo ilisababisha iwe ngumu kutumika vijijini kwa dawa hiyo. Hivi
sasa kumepatikana chanjoa ambayo inastahimili joto ambayo inaweza kutumika hata
vijijini.
Pamoja
na mdondo yapo pia magonjwa yanayoshambulia kuku hapa nchini
Ndui
ya kuku(Fowl pox)
Mafua
ya kuku(Infectious coryza)
Homa
ya matumbo (Cocciodiosis)
Minyoo
na wadudu kama viroboto, chawa, utitiri na kupe wa kuku.
DALILI
ZA KUKU MGONJWA.
Huzubaa
Hali
chakula/maji vizuri
Hujitenga
na wenzake
Hujikunyata
au kuinama
Hutetemeka
Hutembea
kwa shida
Utagaji
wa mayai hupungua au hukoma kabisa
MAGONJWA
YA KUKU HUSABABISHWA NA NINI?
Yako
mambo mengi yanayosababisha lakini matunzo hafifu pia huchangia.
MATIBABU
KIDERI
- Sifahamu tiba ya kitaalam ya ugonjwa huu kama kuna ambaye anafahamu tunaomba
atufahamishe lakini ziko dawa za asili na za kitaalam ambazo zinafaa zaidi kwa
chanjo.
Ugonjwa
huu unaweza kuukinga kwa kuwapa kuku chanjo ya Mdondo. Pia usichanganye kuku
wako na kuku ambao huna taarifa zao za chanjo.
KUMBUKA
Mdondo
au kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kuua kuku wote
Mdondo
ukitokea vifo huwa vingi pia kuku hupumua kwa taabu, hupooza na wengine
huzunguka na huzungusha vichwa.
Mdondo
unaweza kuzuilika kwa chanjo kila baada ya miezi 3
NDUI
YA KUKU
HOMA
YA MATUMBO (Fowly typhoid)
MAFUA
YA KUKU(Infectious coryzya)
KUHARISHA
DAMU(Coccidiosis)
Minyoo
na wadudu wanaoshambulia kuku kama viroboto n.k
Kwa
magonjwa na wadudu tuliowataja hapo juu please wasiliana na mtaalamu wa mifugo
aliye karibu nawe Kwani siwezi kueleza kila kitu hapa wataalamu tunao naamini
watatusaidia.
TIBA
ZA ASILI
Kuna
madawa ya asili ambayo hutokana na mimea ambayo hukinga kuku.
BAADHI
YA MIMEA INAYOTIBU NA KUKINGA MARADHI YA KUKU.
MWAROBAINI
- Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda
ALOEVERA
- Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda,ngozi na Cholera. Tutaelekezana
zaidi namna ya kuandaa dawa hii.
Hapa
nataka niorodheshe baadhi ya madawa ya asili ambayo yanasaidia kutibu na
kukinga kuku.
Mwarobaini,
Aloevera, Mtakalang'onyo(Euphorbia),Mbarika, mlonge,
Ndulele/dungurusi/tura/ndura, Majani ya mpapai, Mwembe, Minyaa na Pilipili
kichaa
Comments
Post a Comment