DIRA YA MAISHA YA KIJANA
Kijana ni nani?
Ø Neno
kijana linatafsiriwa katika tafsiri tofauti katika kila jamii, Mathalan nchini
Tanzania kijana ni mtu mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35, yaani baada ya
balehe. Mabadiliko makubwa ya kimaumbile hutokea sambamba na kukomaa kwa mawazo.
Ø Aidha
Kwa mujibu wa sera ya
Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007,
kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15 hadi 24.
Ø Hali kadhalika
Kwa tafsiri ya umoja wa mataifa, Kijana ni mwanamke au mwanamme aliye na umri
kati ya miaka 15 hadi 24. Tafsiri hii hutofatiana kutoka nchi moja hadi nchi
nyingine. Nchi au maeneo mengine ya dunia huwa na tafsiri tofauti kulingana na
mahitaji ya mazingira na maeneo yao, na pengine kwa mujibu wa mifumo ya
kijamii,kisiasa na kisheria katika nchi hizo.
Ø Ni
kipindi cha mpito kutoka utoto kuelekea uzee.Ni kipindi chenye heka heka nyingi
kwa vijana kutokana na mabadiliko ya kimaumbile, kwani kijana hutaka
kujionyesha kwamba yeye ni nani katika jamii.
Kwa kweli na hapa ndiyo msingi wa maisha ya uzeeni.Na pia ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Kwa kweli na hapa ndiyo msingi wa maisha ya uzeeni.Na pia ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Ø Katika taifa lolote lile, vijana ni nguzo
muhimu katika shughuli na masuala mbalimbali, iwe ni shughuli za ujenzi, vita,
siasa, uchumi, utawala n.k. Vijana wana hamu, shauku, ndoto na matumaini
makubwa ya maendeleo, huku wakiwa na nguvu nyingi na akili zao zikiwa
zinachemka.
NAFASI YA VIAJANA KATIKA UJENZI WA JAMII NATAIFA
1.
Vijana
wanapaswa kuwa na fikra yakinifu. Ufikiri yakinifu ni suala muhimu sana kwa
vijana. Ufikiri yakinifu ndio hupelekea uvumbuzi na ubunifu wa vitu na mambo
mbalimbali. Kama ambavyo John F. Kennedy, Rais wa Marekani miaka ya 1961 -
1963, aliposema "usifikirie kuwa nchi yako itakufanyia nini, ila fikiria
utaifanyia nini nchi yako".Hii inamaanisha kuwa vijana wanatakiwa kuja na
mawazo mapya yenye maendeleo chanya kwa taifa. Vijana watakuwa wadau wazuri na
viongozi bora wa taifa, endapo watakuwa wanajua mambo mengi hususani
yanayohusiana na maendeleo, jambo ambalo linahitaji kujifunza kupitia kujisomea
kwa kila siku.
2.
Vijana
wanapaswa kuwa wabunifu. Gurudumu la maendeleo la taifa lolote, hutegemea sana
ubunifu na uzalishaji wa vijana wa taifa hilo. Hii inamaanisha kwamba, taifa
ambalo vijana wake hawafikiri, si wabunifu na ni wavivu katika uzalishaji mali,
taifa hilo kamwe haliwezi kuendelea. Kila kona ya nchi kwa sasa, vijana wengi
wanalia na tatizo la ajira, jambo ambalo nakubaliana nalo kwa asilimia mia
moja. Lakini kwa upande mwingine vijana wanapaswa wakumbuke kanuni ya kwanza ya
mwendokasi ya Isaack Newton inasema, "hakuna kitu kinachoweza kujongea
kutoka sehemu moja kwenda nyingine, pasipo kutumika nguvu". Tafsiri ya
kanuni hii, inaweza kuwa inakatisha tamaa hasa kwa wale wanasubiri kuajiriwa.
Lakini huo ndio ukweli. Huu ni muda wa vitendo. Ni muda muafaka wa vijana
kupanua wigo wa kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa taifa, kwa kufanya
ujasiriamali, kilimo, au ufudi stadi. Vijana hawapaswi kusubiri hadi wawe na
mtaji mkubwa ili kuanzisha biashara. Wanaweza kuanza biashara kwa mtaji mdogo
wa fedha, ambapo kutokea hapo wanaweza kukuza mitaji yao na hatimaye kuzifikia
ndoto zao. Kuwekeza na kufanya biashara katika sekta zinazoajiri na kuleta
faida kubwa kama sekta za kilimo, viwanda, usafirishaji na mawasiliano.
3.
Vijana
wanapaswa kuwa chachu ya mabadiliko. Vijana ni lazima wawe chachu ya
mabadiliko. Na mabadiliko hayo hayana budi kuanzia kwao. Ni lazima watumie
uwezo wao kuisaidia serikali katika kutekeleza sera zake, lakini pia lazima
wapinge kwa nguvu zote aina zote za unyonyaji unaofanywa na mtu au kundi la
watu dhidi ya umma, na pia hata unyonyaji unaofanywa na kundi kubwa dhidi ya
kundi dogo au mtu mmoja.
4. Vijana wanapaswa kuonyesha mfano mzuri wa
aina ya uongozi yenye tija kwa kizazi cha sasa na kijacho. Vijana ni lazima
washiriki katika kufanya maamuzi kwa kujiunga na kushiriki katika siasa. Kada
ya uongozi ilikuwa imetawaliwa kwa kiasi kikubwa na wazee ambao walidhani kuwa
suala la kujenga na kulitumikia taifa, ni jukumu lao na si la vijana, kwa madai
kuwa vijana ni taifa la kesho. Lakini hiyo kesho mara nyingi ilikuwa haifiki.
Kauli na misemo kama hii imewafanya vijana wakae pembeni na kuacha kushiriki
pamoja na kutimiza majukumu yao wakidhani kuwa muda wao wa kutimiza majukumu
kwa taifa bado. Taifa lenye vijana wanaojitambua, ni taifa litakaloendelea, na
taifa lenye vijana wasiojitambua ni taifa lenye safari ndefu ya maendeleo.
Vijana wengi wamedhihirisha kuwa wanaweza kuwa viongozi wazuri au kuwa na
mchango mkubwa katika taifa, ili hali wana umri mdogo. Mfano Mwl. Nyerere,
alianza kuongoza harakati za kudai Uhuru akiwa na miaka 30, na akaanza kuhudumu
nafasi ya Urais wananchi akiwa na miaka 39. Salim Ahmed Salim alihudumu kama
balozi wa Tanzznia nchini Misri akiwa na miaka 22. John Samuel Malechela alihudumu
kama balozi wa Tanzania kuwakilisha Umoja wa Mataifa akiwa na miaka 28, huku
Jenerali Mrisho Sarakikya alikuwa Mkuu wa Majeshi akiwa na miaka 30. Bila
kumsahau Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa
vipindi viwili tofauti. Vijana hawa wote walihudumu nafasi zao kwa weledi na
uwezo mkubwa.
5. Vijana wanapaswa kuwa
na uzalendo kwa taifa lao. Kwa sasa, uzalendo ambayo ni tunu muhimu sana,
imepotea miongoni mwa vijana wengi. Ili taifa liweze kustawi, ni lazima watu
wake wakiwemo vijana, wawe na mapenzi ya dhati na yasiyo na mipaka kwa taifa
lao.
Maovu yote yanayofanyika katika taifa hili, kama vile rushwa ufisadi,
ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, na mengine mengi, ni matokeo ya kukosekana
kwa uzalendo.
Kama vijana wa kitanzania, uzalendo ni lazima uonekane katika
maisha yao ya kila siku. Uzalendo unapojengeka ndani ya mioyo na akili za
vijana wa kitanzania, itawafanya vijana hao waone kuwa Tanzania ni mali yao, na
hivyo ni jukumu lao kuilinda.
Watatumia nguvu zao, akili zao na ujuzi wao
kulijenga taifa lao kwa maslahi ya kizazi chaleo na kesho. Kama vijana watakuwa
wazalendo, wataweza kupinga rushwa na aina zote za uhujumu uchumi, na hata siku
wakipewa dhamana katika ofisi za serikali au taasisi binafsi, wat aendelea
kuyapinga maovu.
6. Vijana wanapaswa
kufanya kazi Kwa bidii. Vijana ni kama injini ya gari.Bila injini, gari
haliwezi kutembea.Vivyo hivyo, taifa bila vijana, haliwezi kuendelea. Kundi la
vijana ni uti wa mgongo wa taifa. Vijana ni injini ya uzalishaji na maendeleo,
kwa kuwa ndiyo nguvukazi katika uzalishaji wa mazao, bidhaa au huduma. Hivyo wanapaswa kuwa wepesi wa kujifunza, kufanya kazi
katika mazingira magumu na yenye presha, na kuleta mafanikio makubwa katika
taasisi au taifa.
7. Vijana wanapaswa kuwa
mabalozi wa kusambaza habari mbalimbali zinazohusu maendeleo. Ni lazima kuwe na
taasisi za vijana ambazo ni kubwa na zenye nguvu, ambazo zitakuwa ni majukwaa
ya vijana kujihusisha na shughuli za ujenzi wa Taifa ikiwa ni pamoja na
kuelimisha jamii kuhusu maendeleo ya taifa lao na Tanzania ya lwo na kesho.
Lakini kwa upande
mwingine pia, serikali na jamii kwa ujumla pia haipaswi kukaa nyuma katika
kuwajengea vijana katika kuchangia kuleta maendeleo maendelevu. Vijana
wanatakiwa kufundishwa maarifa na ujuzi unaoakisi maendeleo ya taifa husika.
Pia vijana wanapaswa kujua kusoma, kuandika, kufikiri, kuchambua na kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu taifa hilo. Baba wa taifa la Afrika Kusini,
Hayati Nelson Rolihlahla Mandela (Madiba), alipata kusema kuwa "hakuna
taifa linaloweza kuendelea, pasipo na kuelimika kwa watu wake".
Nguvu na upeo wa akili za
vijana, ni kama tochi inayomulika maendeleo ya Taifa. Katika dunia ya leo,
maarifa na ujuzi ndio vimekuwa sarafu (fedha) ya dunia nzima. Lakini hakuna
benki kuu ya sarafu hii, bali ni viongozi na jamii ndio hupanga jinsi ya
kuzalisha sarafu hii, na jinsi ya kuitumia. Taifa linaweza kuwa na utajiri wa
rasilimali kama gesi asili, madini au mafuta, lakini rasilimali hizi zinaweza
kuwa hazina maana endapo faida inayotokana na rasilimali hizo, hazitawekezwa
katika sekta muhimu kama elimu ambayo ndio shamba la fikra mpya.
Pia ni lazima taasisi
zetu za elimu, hususani vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na vyuo vikuu, viwaandae
wahitimu wao kuwa watengeneza ajira na siyo kuwa wanasubiri kuajiriwa. Kijana
anapoanza masomo ya chuo, anapaswa kujua kuwa atakapohitimu hapaswi kufikiria
kuajiriwa au kurudi nyumbani na kuwategemea wazazi.
Nchi yetu kwa sasa
imeathiriwa sana na siasa, hususani zisizo na tija. Wito wangu kwa wanasiasa
wote ni kuwa, wanapaswa watambue kuwa wana jukumu la kuwajenga vijana, na siyo
kuwatumia kwa maslahi yao binafsi kama vile kuwashawishi kufanya vurugu,
maandamano yaliyo kinyume na sheria, n.k.
Mwisho, Kuna misemo
inayosema kuwa "ukishindwa kupanga, unapanga kushindwa" na mwingine
ukisema "vijana ni taifa la leo na kesho". Kama kweli vijana ni taifa
la leo na kesho, basi leo ndio muda muafaka wa kuliandaa hilo taifa. Na kama
tutashindwa kupanga kuliandaa leo taifa la kesho, basi tutapanga kushindwa
katika taifa la kesho.
NAFASI NA MAJUKUMU YA VIJANA KATIKA UCHUMI NA MAENDELEO YA TAIFA
Serikali na Jamii ya Watanzania tunalo jukumu la kuwajengea Vijana uwezo wa
kuwawezesha kuwa Viongozi wa baadaye.
Vijana wanatakiwa kuwa wenye maono na ubunifu katika kukuza Uchumi
wa Taifa. Vijana wanapaswa
· Kuwa
na mawazo mapya, mbinu mpya na kuwa chachu ya mabadiliko chanya ya kimaendeleo;
Vijana wanatakiwa kuwa Wajasiriamali wazuri wenye ujuzi mbalimbali (Young
Enterprenuers Skills), na
· Kuwa
Wavumbuzi wa vitu mbalimbali vitakavyoweza kukuza uchumi wetu; Vijana
wanatakiwa kuwa na mahusiano chanya na marafiki wa Mataifa mengine katika Nyanja
· Mbalimbali
za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, kama vile Michezo, Sanaa na Tafiti
mbalimbali za Kimaendeleo; Vijana
wanapaswa kuwezeshwa, kupewa nafasi waonyeshe vipaji vyao na kushirikishwa
katika shughuli
· Mbalimbali
za Uchumi na Jamii kwa ujumla; Vijana
wanapaswa kushiriki katika Uongozi;
· Vijana wanapaswa kupata elimu bora.
HISTORIA INAONYESHA NI VIONGOZI VIJANA NDO WENYE UWEZO WA KUFANYA
MABADILIKO YANAYOTEGEMEWA NA VIJANA WENZIO.
Yesu kristo alianza shughuli zake rasmi akiwa na miaka 30 tu, na mpaka leo kila mmoja anakubali mafanikio ya kazi yake iliyodumu kwa takriban miaka mitatu hivi
Julius ceaser mwasisi wa roman empire akiwa na miaka 29 tayari alishafanikiwa kutengeneza taifa kubwa na lenye nguvu la roma, pia kuasisi milradi mikubwa iliyosaidia vijana wa roma kuwa na nguvu kiuchumi na kijeshi.
Alexander the great akiwa na miaka 30 tu tayari alishafanikiwa kupanua dola yake kuanzia greece mpaka egypty, huku akihamasisha vijana kuwa magavana na mageneral katika kila kona ya dola hiyo.Kijana huyu alitengeneza mpaka irrigation scheme kwa wakati huo ili vijana waweze kulima
Julius Nyerere akiwa na miaka 42 tu alikuwa kiongozi wa nchi hii na kwa mafanikio makubwa kabisa alihamasisha vijana wenzie kusoma na kushika uchumi wa nchi na akawapa kazi mbalimbali katika serikali yake, mfano mzuri ni DR. SALIM aliyeteuliwa kuwa balozi akiwa na miaka chini ya thelathini.
Wakati marekani ikiwa na population zaidi ya nusu vijana, wakamchagua kennedy akiwa na umri wa miaka 45 tu, kennedy anakumbukwa mpaka leo kwa mambo makubwa aliyofanya katika kipindi kifupi. Hasa katika sela zake zilizotoa kipaumbele kwa vijana
Pia baada ya kuchoswa na sela za kizee za BUSH yule mzee, wamerekani wakaona ni muhimu kumchagua kijana ili kuleta mabadiliko ya msingi, na hapo William Jefferson (Bill clinton) alichaguliwa akiwa na umri wa miaka 47 tu.Nani asiyejua jinsi Clinton alivyoshughulikia suala la ajira nchini marekani.
Yesu kristo alianza shughuli zake rasmi akiwa na miaka 30 tu, na mpaka leo kila mmoja anakubali mafanikio ya kazi yake iliyodumu kwa takriban miaka mitatu hivi
Julius ceaser mwasisi wa roman empire akiwa na miaka 29 tayari alishafanikiwa kutengeneza taifa kubwa na lenye nguvu la roma, pia kuasisi milradi mikubwa iliyosaidia vijana wa roma kuwa na nguvu kiuchumi na kijeshi.
Alexander the great akiwa na miaka 30 tu tayari alishafanikiwa kupanua dola yake kuanzia greece mpaka egypty, huku akihamasisha vijana kuwa magavana na mageneral katika kila kona ya dola hiyo.Kijana huyu alitengeneza mpaka irrigation scheme kwa wakati huo ili vijana waweze kulima
Julius Nyerere akiwa na miaka 42 tu alikuwa kiongozi wa nchi hii na kwa mafanikio makubwa kabisa alihamasisha vijana wenzie kusoma na kushika uchumi wa nchi na akawapa kazi mbalimbali katika serikali yake, mfano mzuri ni DR. SALIM aliyeteuliwa kuwa balozi akiwa na miaka chini ya thelathini.
Wakati marekani ikiwa na population zaidi ya nusu vijana, wakamchagua kennedy akiwa na umri wa miaka 45 tu, kennedy anakumbukwa mpaka leo kwa mambo makubwa aliyofanya katika kipindi kifupi. Hasa katika sela zake zilizotoa kipaumbele kwa vijana
Pia baada ya kuchoswa na sela za kizee za BUSH yule mzee, wamerekani wakaona ni muhimu kumchagua kijana ili kuleta mabadiliko ya msingi, na hapo William Jefferson (Bill clinton) alichaguliwa akiwa na umri wa miaka 47 tu.Nani asiyejua jinsi Clinton alivyoshughulikia suala la ajira nchini marekani.
NIMEIPENDA KWA KWELI......
ReplyDeleteVijana ni chachu ya maendeleo KWA jamii yoyote.
ReplyDelete