Skip to main content

RISALA KWA MGENI RASMI KWENYE SEMINA YA MAFUNZO KWA MABALOZI WA KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA JANUARI 27 2018.

RISALA KWA MGENI RASMI KWENYE SEMINA YA MAFUNZO KWA MABALOZI WA KAMPENI YA BINTI AMKA TANZANIA JANUARI 27 2018.

MHE; Mgeni Rasimi, Wadhamini, wakufunzi, Wakuu wa taasisi mbalimbali, Viongozi wa YOPOCODE, viongozi wa kampeni. Wajumbe wa kamati ya fedha na maandalizi, Ndugu Mabalozi wenzangu, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana.       

Bwana Yesu asifiwe!                                                                       

Asalaam Alaykum                                                                       

Habari za mchana     

Mhe; Mgeni Rasimi, Ndugu Viongozi na Ndugu Mabalozi nitumie fursa hii kumshukuru MUNGU mwingi wa rehema kwa kutujalia kufika hapa tukiwa wazima wa afya tele.

Pili, tunapenda kukushukuru wewe Mhe; Mgeni rasmi kwa kukubali kwako kuwa mgeni rasimi katika siku hii na pia tunakukaribisha sana ushiriki pamoja nasi katika siku hii muhimu na kusikiliza mafanikio yetu pamoja na changamoto mbalimbali tunazopata katika uendeshaji wa kampeni yetu hii ya BINTI AMKA TANZANIA 

Tatu,tunawashukuru wakufunzi wetu makini na wageni wetu waalikwa na viongozi wa shirika la vijana Tanzania la YOPOCODE kufanikisha maandalizi ya shughuli hii pevu.                          

Mhe;Mgeni rasmi, Ndugu viongozi na Ndugu mabalozi wa BINTI AMKA. BINTI AMKA TANZANIA ni kampeni mahususi inayolenga kumsaidia mtoto wa kike Tanzania kufikia malengo yake kielimu, kiuchumi na kisiasa. Kampeni hii imeasisiwa na viongozi wakuu wa shirika la vijana Tanzania YOPOCODE lenye makao makuu mkoani Mbeya na  Matawi yake mikoa mbalimbali ikiwemo Singida, Njombe na Dar es salaam.

 Kama timu waliibuka na wazo la kumkombowa mtoto wa kike Tanzania baada ya kubaini kwamba watoto wa kike wanapitia changamoto nyingi sana wakati wa kupigana kufikia malengo yao. BINTI AMKA ni jina rasmi la kampeni yetu BINTI AMKA TANZANIA .                                     

 KWA KIFUPI Balozi wa kampeni ya BINTI AMKA ni mtu yoyote aliyekubali na kuwa tayari kusimama kidete kuhakikisha mtoto wa kike Tanzania anafikia malengo yake kielimu, kiuchumi, kisiasa. Wajibu wa balozi wa BINTI AMKA nchini Tanzania ni pamoja na, kukubali kuwa sehemu ya watu waliojitowa kusaidia watoto wa kike.

 Pili, kukubali kufanya kazi na shirika letu kupitia  kampeni hii.

Tatu,kuwajibika kusema uzuri wa kampeni kwa namna yoyote bila kuogopa.

Nne, kushiriki mikutano yote ya mabalozi wakuu bila kubaguliwa.

Tano, kukubali kutoa mchango wake wa hali na mali kufanikisha kampeni yetu.

 Pia kuingia mahali popote na kusema ukweli kuhusu hali ya mtoto wa kike Tanzania, tena anapaswa kufanya utafiti na ripoti mbalimbali kuhusu hali ya mtoto wakike Tanzania,

Na mwisho anapaswa kuunda vikundi mbalimbali vinavyolenga kumsaidia mtoto wa kike Tanzania.                                                                  

   Mhe; Mgeni rasmi ilimtu awe balozi wa kampeni ya BINTI AMKA anapaswa awenasifa hizi, awe tayari kufanya kazi, awe na akili timamu na hamasa ya kujitolea kusaidia watoto wa kike Tanzania, awe mtanzania mzalendo mwenye uchu na maendeleo ya nchi.          

Kuna changamoto nyingi zinazowaathiri watoto wakike Tanzania zilizopolekea kuunda kampeni hii ya BINTI AMKA TANZANIA. Baadhi ni kama ndoa na mimba za utotoni, mfumo dume wa familia, manyanyaso kwa baadhi ya mabinti kutoka kwa walezi wao na kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu na ajira ngumu za utotoni na chanzo cha haya yote kwa mtoto wakike yaweza kuwa ni wazazi au walezi, marafiki au jamii inayomzunguka, hali ngumu ya maisha kiuchumi, umbali mrefu wa kwenda kupata huduma za kijamii kama shule, hospitali na maji na pia yawezakuwa ni taama mbaya kwa mabinti wenyewe                                                                                                                  Mhe;Mgeni rasmi, kwa sehemu tumefanikiwa kufanya vitu kadhaa ilikuakikisha kampeni yetu inafanikiwa, tumefanikiwa kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni yetu kwa mkoa wa Singida, tumefanikiwa kupata mabalozi wasiopungua 50 kwa mkoa wa dar-es-salaam na mabalozi wasiopungua 200 mikoa mingine, tumefanikiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wakuu wa kampeni yetu kwa mkoa wa DAR ES SALAAM,

 VIONGOZI WALIOCHAGULIWA NI MADAM HAPPYNESS SWAI KAMA REGION PROJECT COORDINATOR, MADAM UPENDO MINJA KAMA PROJECT GENERAL SECRETARY PAMOJA NA MADAM BERTHA KAMA REGIONAL PROJECT FINANCE MANAGER NA MADAM HAPPINESS EMANUEL BAKUZA KAMA AFISA MAWASILIANO NA MIPANGO.

Tumefanikiwa pia kuwatembelea na kuwasaidia watoto wa kituo cha watoto waliookolewa katika mateso na manyanyaso kwa mkoa wa Mwanza, tumefanikiwa kufunguwa mitandao ya kijamii kama instagram, facebook na blogspot ili kuwahabarisha jamii kuhusu hali ya binti zetu                                                          

Mhe;mgeni rasmi si hayo tu pia tumefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali kuhusu hali na maendeleo ya mtoto wa kike tukagundua kuwa kwa mjibu wa shirika la watoto duniani UNICEF kumekuwa na ongezeko kubwa la mimba mashuleni kutoka 23% hadi 26% yaani takribani watoto 8000 hapa Tanzania kila mwaka hukatisha masomo kwa ajili ya ujauzito na ndoa za utotoni ambazo lkwa kiasi kikubwa huathiri ndoto zao za kielimu, kiuchumi na kisiasa.

Vilevile idadi kubwa ya watoto wa kike wamekuwa wakimaliza elimu ya msingi lakini upoteza nafasi ya kujiendeleza kielimu hata pale wanapokuwa wamechaguliwa kujiunga na sekondari nayo imekuwa ikiongezeka,pia kushuhudia kuongezeka kwa vitendo vya kikatili wa kingono kama ubakaji na ulawiti kwa watoto wakike na chakusikitisha zaidi vitendio hivyo vimekuwa vikifanywa na ndugu wa karibu sana wa watoto hawa wakiwemo wazazi,walezi, majirani na hata walimu uko mashuleni matukio haya yamekuwa hayaripotiwi kwenye vyombo vya sheria kwani mengi huzungumzwa kifamilia na kuwaacha watuhumiwa wakiendelea na maisha yao. JE, MIMI NA WEWE TUKAE KIMYA NA KUENDELEA KUTAZAMA HILI?


Mhe;mgeni rasmi, pamoja na mafanikio haya pia tumekuwa tukikumbana na changamoto mbalimbali katika kuendesha kampeni hii. Changamoto ambazo tumekuwa tukikumbana nazo ni pamoja na ukosefu wa ufadhili mpaka sasa hatujapata mfadhili yoyote na hivyo kulazimika kuomba michango kwa mabalozi wenzetu ilikufanikisha shughuli zetu, vitendea kazi navyo vimekuwa changamoto kubwa hasa vifaa vya stationary ambavyo vinarahisisha shughuli zetu, usafiri nao umekuwa changamoto nakuwalazimu viongozi wetu kutumia gharama zao wenyewe kwa shughuli za kiofisi, changamoto nyingine ni kukosa mawasiliano na taasisi mbalimbali zinafanya shughuli zinazofanana na pia kukoseka kwa utayari wa moja kwa moja kutoka kwa wadau mbalimbali

Comments

Popular posts from this blog

WITO NI NINI?

MJUE ALIYEKUITANA KUMTUMIKIA WITO NI NINI? Kila mtu Mungu amemwita kwa nafasi yake amtumikie.Hata kama kwa nje wito utaonekana kufanana haina maana wito wa mtu mmoja na mwingine unafanana. Wito unatokana na kuitwa. Kila mtu Mungu amemwita amtumikie katika eneo Fulani.  Wito : Ni sauti au agizo analosikia mtu likimwelekeza nini cha kufanya.Katika wito wowote ukiwa umeitwa na Mungu atakuelekeza nini cha kufanya.Na unapoitwa na Mungu jitahidi kutenda sawa na wito wako ulivyo. NITAJUAJE NIMEITWA? 1.Utaisikia sauti ya Mungu ikisema na wewe: Kama kuitwa kwa kawaida kulivyo ndivyo mtu uisikia sauti ya Mungu  ikisema nae. Ebu angali mifano ya watu mbalimbali waliowahi kuisikia sauti ya Mungu ikiwaita kwa ajili ya kutekeleza agizo fulani. MUSA kabla ya kuanza kumtumikia Mungu alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwe Yethro kuhani wa Midiani.Katikati ya uchungaji Mungu alimwita Musa.Kumbe ili na wewe umtumikie Mungu unatakiwa uisikie sauti yake ikisema na wewe,Ni hatari sana kama uta

KIJANA NI NANI???

KIJANA NI NANI? NA MWANDISHI,  JANEROSA MAFWIMBO Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24. Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. Tofauti kati ya mtoto na kijana, wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mtoto na kijana hasa waliopo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana

MAMBO 12 YA KUFANYA UKIWA KIJANA

Vijana Tanzania Na Alfred Mwahalende Kwa mujibu wa mwandishi wa blog ya Dira Ya Kijana Tanzania  Janerosa Mafwimbo anasema “ Neno kijana limekuwa na maana pana na linakuwa likipata tafsiri mbalimbali kutoka katika kila Taifa, jamii au tamaduni fulani. Kwakuzingatia mifumo au maisha ya jamii tunapata baadhi ya tafsiri za neno kijana kama ifuatavyo: 1.     Kijana ni mtu wa miaka 15-24. Hii ni tafsiri ya umoja wa Mataifa. 2.     Mathalani nchini Tanzania kijana ni mtu wa miaka 18-35 yaani baada ya balehe na mabadiliko ya maumbile toka utoto kuelekea ukubwa, aidha kw mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007, inasema kijana ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15-24.Hivyo basi kijana ni mtu yeyote wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 18-35 ambaye kwa mujibu wa mifumo ya kijamii au kitamaduni, kisiasa na kisheria anauwezo wa kujitegemea na kufanya maamuzi yake binafsi. ” JE, UJANA NI NINI? 3.     Ujana ni hatua ambayo mtu anapi