SEMINA YA MAFUNZO KWA MABALOZI WA BINTI AMKA TANZANIA
SOMO: MAADILI YA KUFANYA UTAFITI
MKUFUNZI NI:Basiliana Emidi, PhD
Yaliyomo
1. Muingiliano wa kimaadili na washiriki wa utafiti
u Wajibu wa mkusanyaji taarifa
u Umuhimu wa Heshima
u Ushiriki wa hiari
u Ridhaa ya kushiriki katika utafiti
u Watu waliokaribú kuathirika na masuala yafanyiwayo utafiti
u Faragha binafsi
u Kuhifadhi kwa usalama taarifa binafsi
u Kujibu maswali ya washiriki
} 2. Usahihi wa taarifa za utafiti
Kuheshimu sayansi ya utafiti
Kukusanya, kunakili/kuandika na kuhifadhi taarifa
Ukiukaji wa mwongozo wa utafiti
Maadili ni nini?
} Maadili ni kanuni adilifu zinazoelekeza tabia zetu katika mahusiano yetu ya kila siku na wenzetu.
} Katika utafiti, maadili ni uwajibikaji na uwelekevu kitabia kuhusiana na haki za wale wote tunaotangamana nao katika utafiti, uwelekevu katika nia na malengo ya utafiti na jinsi ya kutumia matokeo kwa uadilifu ili yaweze kuwa na faida kwa jamii ya binadamu.
1. Muingiliano wa kimaadili na washiriki wa utafiti.
2. Wajibu wa mkusanyaji taarifa
} Anayekusanya taarifa kwa niaba ya timu ya watafiti ni ”balozi” wa utafiti husika na mara nyingi hukutana moja kwa moja na mtafitiwa.
} Kwa hiyo ndie atakaeashiria kwa watafitiwa kuwa utafiti huu utafanikiwa ama la, kutegemea na jinsi atakavyojieleza mbele ya watafitiwa.
} Mkusanya taarifa ana wajibu wa kuhakikisha kuwa taarifa zilizokusanywa ni zile ambazo na mtafitiwa ambae amekubali kushiriki katika utafiti.
} Mkusanya taarifa ahakikishe kuwa taarifa zilizopatikana ni sahihi
} na zihifadhiwe zisivuje, kinyume cha hayo,malengo ya utafiti hayatafikiwa.
ii.Umuhimu wa Heshima
} Ina mlazimu kila muhusika katika timu ya watafiti aheshimu yafuatayo:
ü Malengo ya utafiti.
ü Viongozi wa utafiti.
ü Mshiriki mmoja mmoja wa utafiti.
ü Jamii ya watafitiwa.
ü Taarifa zilizokusanywa ambazo zitasaidia kufanikisha malengo ya utafiti.
} Utafiti unakusudia kusaidia jamii inayohusika, ambapo timu ya watafiti watafanikiwa kukamilisha sehemu zote zinazohusika katika utafiti.
Ø iii. Ushiriki wa hiari
Hakuna mtu anaelazimishwa kushiriki katika utafiti.
Kama utafiti umehusisha kuomba ridhaa ya kushiriki, basi kila mtafitiwa atakayefuatwa na mtafiti atakuwa na haki na kukataa kushiriki katika utafiti.
Hata kama mtafitiwa atashiriki katika utafiti, bado atakuwa na haki ya kujibu au kutojibu swali moja au jingine, atakuwa na haki ya kukataa kushiriki katika jaribio la utafiti au atakuwa na haki ya kujitoa katika utafiti wakati wowote.
Watafiti ambao wataomba ridhaa ya kushiriki kutoka kwa washiriki, wana wajibu wa kuhakikisha kuwa watafitiwa wana uelewa wa kutosha juu ya utafiti.
iv. Ridhaa ya kushiriki katika utafiti
u Kupata ridhaa ni mchakato unaoendelea ambao unaanzia pale watafiti wanaanza kuelezea washiriki kuhusu utafiti.
u Hata hivyo ridhaa ya kushiriki haziishii tu kwa washiriki kusaini fomu za ridhaa na kukubali kushiriki, bali huendelea kwa muda wote wa Utafiti.
u Hakuna ridhaa ya kweli kama mtafitiwa atakuwa haelewi vya kutosha juu ya utafiti unaofanywa. (Timu ya watafiti ni lazima ihakikishe kabla ya utafiti kuwa ”taarifa za kutosha” ni kiasi gani, na vipi taarifa hizo zitatolewa kwa watafitiwa).
u Ni kazi ya muhusika ambaye atachukuwa ridhaa ya kushiriki na kuwasilisha taarifa za utafiti kwa watafitiwa katika lugha ya kueleweka. Taarifa hizo ni lazima zijumuishe malengo na umuhimu wa utafiti, faida za utafiti wenyewe pamoja na madhara yanayoweza kutokezea.
u Watafiti ni lazima waelewe “lugha za mwili,” kwa vile mara nyengine,
u washiriki huonekana kama vile bado hawajaridhika.
v. Watu waliokaribu kuathirika na masuala yafanyiwayo utafiti
} Baadhi ya watu huhitaji kusaidiwa kwa karibu zaidi wanapoulizwa kuhusu hiari ya ushiriki wao katika utafiti, kwa vile itakuwa vigumu kwao kuelewa wanachoelezwa. Kwa mfano;
ü Wafungwa
ü watoto
ü Watu wazima ambao wamepoteza kumbukumbu au
ü wenye matatizo ya akili
} Timu ya watafiti lazima wawe waangalifu na kufuata maelekezo vizuri wakati watakapohitaji kushirikisha watu kama hawa katika utafiti kwa vile watu hawa hawawezi kufanya maamuzi binafsi.
} Ni lazima kuwe na msimamizi au mwangalizi aliyeaminiwa kuamua kwa niaba yao.
vi. Faragha binafsi
} Watafiti ni lazima watambue na waheshimu kuwa kila mshiriki ana haki ya kupata faragha.
} Uchunguzi wa kimwili ni lazima ufanyike pahala pa faragha.
} Mambo ambayo huwa ni siri kama vile vitendo vya kujamiiana, afya binafsi, ama mawazo ambayo mtu hatopenda aongee hadharani.
} Hii itasaidia mshiriki asipatwe na aibu au fadhaa zisizo za lazima.
vii. Kuhifadhi kwa usalama taarifa binafsi
Ikiwa mtafitiwa ataongea habari zinazomhusu kwa mkusanya taarifa, kuna hatari kwamba habari hizo zinaweza kusikika kwa watu wengine wengi, na hivyo kupoteza ”usiri wa taarifa binafsi.”
Hatari ambazo zinaweza kutokea kama taarifa binafsi zitasikika kwa watu wengine ni pamoja na kufikwa na aibu, kupoteza ajira, kushitakiwa au kutengwa na jamii.
Hivyo, watafiti wana jukumu la kumkinga mtafitiwa kutokana na madhara kama hayo.
Mara nyengine mfumo wa nambari hutumika ili kutobaini wahusika na majibu yao.
viii. Kujibu maswali ya washiriki
} Mkusanya taarifa atakutana na watu mbali mbali wakiwemo;
watafitiwa watarajiwa na
wale wanaoendelea kutafitiwa,
watu ambao hawamo katika utafiti
Lakini watapenda kujua kuhusu utafiti unaofanyika.
} Watu hawa wanaweza kuuliza maswali mengi. Ni muhimu kuwa mvumilivu na kujaribu kujibu masuala yote kadiri iwezekanavyo, ili mradi unafahamu jibu
2. Usahihi wa taarifa za utafiti
i. Kuheshimu sayansi ya utafiti
} Taarifa za utafiti ndio matunda ya utafiti. Ni muhimu sana taarifa ziwe sahihi.
} Watafiti watatumia taarifa hizo ili kujibu masuala ya utafiti. Kama taarifa zitakuwa sio sahihi, majibu ya utafiti pia yatakuwa sio sahihi.
} Kuna watu wataathirika na kuwa hatarini kutokana na kutoa taarifa zisizokuwa sahihi.
ii. Kukusanya na kuhifadhi taarifa
u Mkusanya taarifa lazima aelewe vizuri jinsi ya kukusanya taarifa na vipi taarifa hizo zitaandikwa.
u Mkusanya taarifa ni lazima aandike kwa uangalifu, uaminifu na uhakika.
u Kusiwe na taarifa za kubuni na zihifadhiwe vizuri.
u Karatasi za taarifa ni lazima akabidhiwe anaehusika kuzihifadhi na muhusika ni lazima afuate maelekezo yote ili taarifa ziwe siri.
iii. Ukiukaji wa mwongozo wa utafiti
n Mara nyengine mkusanya taarifa hataweza kufuata muongozo wa utafiti kutokana na sababu mbali mbali zilizo nje ya uwezo wake, na mara nyengine hutenda makosa.
n Hata hivyo, ni muhimu kujulisha wasimamizi na viongozi wa utafiti na kutoa taarifa kwa Bodi ya Mapitio ya Kitaasisi (Institutional Review Board – IRB).
u Mkusanya taarifa mahiri ni yule ambaye anamuelezea msimamizi wake matatizo yanayojitokeza, msimamizi huyo ndie atakaeamua nini kifanyike.
• Asanteni sana
YOUTH POTENTIALS FOR COMMUNITY DEVELOPMENT (YOPOCODE TANZANIA)
P.O BOX 78409 DSM
Lufungira/Sam Nujoma Road Kinondoni.
Dar Es Salaam And Coastal Region
E-mail:yopocode@gmail.com
Blog: https://yopocodetanzania.blogspot.com
You tube:@yopocodechannel
Facebook page:@Binti Amka Tanzania
Comments
Post a Comment